Baba Mbasha: Flora alichoka kuishi na mwanangu

Baba Mbasha: Flora alichoka kuishi na mwanangu

palalisote

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2010
Posts
8,335
Reaction score
1,463
Baba mzazi wa Emmanuel Mbasha, Mzee Maneno amefunguka kuwa mwimbaji wa Injili Flora Mbasha alichoka kukaa na mwanaye ndiyo maana mgogoro wao umefika hatua hii.

Last edited by a moderator:
oneni nyuso za binadamu zinang'aa mchana na matabasamu kibao LAKINI usiku/kwenye giza ni nyuso za simba/chui/mbweha/fisi asubiriaye ujikwae AKUMEGeeee

....kugombana sio lazima kuanikanaaa....mlikuwa kiyoo cha jamii lakini sasaaa ni mfano wa watenda uovu
 
Gwajima ajiandae kukumbana na laana ya Baba wa Mbasha. Anadhani kufufua misukule feki ndio kunampa uhalali na kupora mke wa kijana
 
kweli kama Flora amefanya hayo yanayosemwa,Mungu atajua adhabu yake ila sisi yetu macho kuangalia move itaishia wapi.
 
Sasa si ana tuhuma za kubaka, kwani alimbaka flora? Ajibu tuhuma mahakamani
 
Ama kwa hakika, mzee Maneno kanena tena kwa yakini kabisa. Hivi kumbe kuimba nyimbo za injili siyo ishara kwamba mtu keshampokea bwana kiukweli na kuachana na maovu! Ikiwa mzee Mbasha alivyoongea ni vya ukweli na kweli tupu, basi Flora ana laana. Halafu niliwahi kuona ktk mitandao mdogo waki akifanya ngono na Mrisho Ngassa wa Yanga. Ama kweli kunguru hafugiki
 
Flora tapeli tu
kuna mwaka alikwepo singida mjini,pale kanisa la roma,alikuwa akizindua album yake km sikosei
kabla ya kuimba akasimama jukwaani na kuahidi eti atajenga hospitali,aliongea kwa bashasha kweli,yapata miaka karibu mitano sasa hata kiwanja hajapata

flora ni tapeli tu,hata sura yake inajieleza
 
Kuhusu Flora Mbasha naomba niseme ukweli, nilishawahi kugombana na mlokole mmoja siku ya kwanza tu kumuona akiimba kwenye mkutano wa The Big November Cruisade pale jangwani. Nilisema pale hakuna mlokole, ndipo yule mama wa kilokole alipoanza kunishambulia bila kujua kuna mlango wa fahamu wa 6 ambao huona hata kilichojificha hata kwa miaka ishirini ijayo...
 
Gwajima ajiandae kukumbana na laana ya Baba wa Mbasha. Anadhani kufufua misukule feki ndio kunampa uhalali na kupora mke wa kijana

na wewe THE ....NDIO NIINI KUBADILISHA MAJINA
 
Kuhusu Flora Mbasha naomba niseme ukweli, nilishawahi kugombana na mlokole mmoja siku ya kwanza tu kumuona akiimba kwenye mkutano wa The Big November Cruisade pale jangwani. Nilisema pale hakuna mlokole, ndipo yule mama wa kilokole alipoanza kunishambulia bila kujua kuna mlango wa fahamu wa 6 ambao huona hata kilichojificha hata kwa miaka ishirini ijayo...
Dhana ya ulokole aisee ni pana na wengi tupo kwenye dini na madhehebu yetu kutokana na mapokeo yaani kama wazazi walikuwa ELCT, PAG, EAGT, SABATO, CATHOLIC na wewe mtoto unajikuta upo dhebu hilo ni wachache sana ama kwa kushawishiwa au maamuzi yao huamua vinginevyo. wengi wa tunaowaita walokole ni kwa kuwa wamelelewa katika makanisa ya kilokole hivyo unakuta zile taratibu za kilokole wamezizoea na mwisho wa siku wengi wanawaona ni walokole kumbe wengine si walokole ila wamelelewa ndani ya makanisa ya kilokole.
 
Hawa wazazi naona kama ndio wanaharibu kabisa!
 
Sina hamu na makanisa ya kilokole, yaani siku hizi nimesimama mimi kama mimi.
Sio kwenye makanisa ya kilokole tu popote pale unatakiwa usimame wewe kama wewe, kuna mabadiliko kila sehemu kutokana na wakati tuliopo ndio maana mlokole wa miaka 20 iliyopita alikuwa tofauti na wa sasa hivyo hivyo hata katika maisha ya kawaida pia watu walikuwa tofauti pia
 
Hawa wazazi naona kama ndio wanaharibu kabisa!
Hii inaitwa ukimwaga ugali mie namwaga mboga, huo muda aliokimbilia kwenye vyombo vya habari angetumia kukutana na wazazi wenzake kuangalia namna ya kutatua tatizo unless kama wameamua kupiga chini moja kwa moja hapo hata wakiongea inakuwa poa
 
Dhana ya ulokole aisee ni pana na wengi tupo kwenye dini na madhehebu yetu kutokana na mapokeo yaani kama wazazi walikuwa ELCT, PAG, EAGT, SABATO, CATHOLIC na wewe mtoto unajikuta upo dhebu hilo ni wachache sana ama kwa kushawishiwa au maamuzi yao huamua vinginevyo. wengi wa tunaowaita walokole ni kwa kuwa wamelelewa katika makanisa ya kilokole hivyo unakuta zile taratibu za kilokole wamezizoea na mwisho wa siku wengi wanawaona ni walokole kumbe wengine si walokole ila wamelelewa ndani ya makanisa ya kilokole.
Yaani mkuu umeongea yote ukweli mtupu, mimi mwenyewe nilizaliwa kwenye familia ya waumini wa TAG enzi zile Askofu Lazaro ndiyo amechukua madaraka. Enzi hizo huwezi kumshabikia muimbaji mpaka kwanza ufahamu undani wa ulokole wake tofauti na siku hizi, nakumbuka aliyekuwa anatamba sana ni Pastor Munisi, Nkinga christian Choir, Ulyankulu Barabara ya 13 nk.

Mpaka waimbaji wengine akina Mzungu 4 wanaibuka waliibukia kwa Moses Kulola baada ya kanisa la TAG kumeguka kutokana na mgogoro kati ya Askofu Lazaro na Moses Kulola, mimi nilikuwa katika familia hiyo lakini kilichoniondoa huko ni baada ya kupata ufahamu mkubwa na kuona uchafu unaoendelea chini kwa chini baina ya watoto wa waumini na upendeleo uliopo katika kanisa. Mtoto wa fulani anafanya dhambi ya uzinzi anatengwa lakini wa mzee wa kanisa hatengwi kw adhambi ile ile.

Huko kwenye kwaya ni madudu matupu hasa kwenye mikesha ya mazoezi, mpaka mzee wa upako amefuta kwaya ili kuepuka mambo kama hayo..
 
Inasikitisha sana hasa wanyonge na family zetu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Sina shaka hapa ile laana ya Moses Kulola inawatafuna.:embarrassed:
 
Back
Top Bottom