Baba kususa kuhudhuria harusi ya mwanae

Baba kususa kuhudhuria harusi ya mwanae

Ushirikishwaji ni muhimu sana.Kama mzazi unamshirikisha tangu mwanzo,mipango yote anaijua na kuibariki hata iweje hawezi kukosa kuhudhuria shughuli ya mwanae.Tabu watu wengine wakipata vijisenti mke hamjui mme na mtoto hamjui baba.Baba unamshutikiza .Watu unaalika mwenyewe.Yeye unataka aje tu
 
Wanasemaga mwisho wa ubaya aibu. Hilo ni jiwe walilolikataa waashi.
Kama wazee ni waungwana walipaswa kumuomba radhi bila chenga, kwamba tusamehe mwenetu hatukuwa na imani na huku kwenu sio kwa ubaya bali kwa mapenzi mema kwa binti yetu.

Bora hao sasa, kuna mambwiga wanamkataa mkwe kisa hana hela. Mungu sio Athumani, hamna kitu kibaya kama kumuevaluate mtu kwa mali. Aibu sana.
The same happened to my sister (mtoto wa baba mkubwa). Alisusiwa harusi na wazazi na ndugu eti kwa sababu familia ya mwanaume wana kasumba ya kutelekeza wake!Walifunga ndoa bila ndugu za mke lakini baadae walisuluhishana maisha yakaendelea. Mungu nae ana yake, sister alifariki akabaki mumewe, hajaoa huu karibu mwaka wa 10 na anawalea wazazi wa mkewe kama wazazi wake!Yaani sijui baba mkubwa akikumbukaga ubaya alomfanyia huwa anaajisikiaje!
 
ni upuuzi wa kishamba kususia harusi ya mwanao (wa kumzaa) hata kama angekuwa kafanya nini. Kwa kuitwa Baba alipawa kubeba majukumu halafu kama ana ishu aiseme baada ya tukio (Harusi)

Msilaumu bila kujua sababu na bila shaka Bw Harusi alishaambiwa na alikaidi. Kueni muyaone.
 
Kwa nn yy kamuoa mama mdogo ake unadhani baba abaki kushabikia mkwanja wake kwa bebi wako khaa.
 
Hahahah kuna mengi huwa yanaendelea katika familia, ukiwa nje ni ngumu kuelewa.
 
ujui unachosema wazaz ni miungu wanaweza kukulaani au kukubariki kumbuka yakobo,ruben so baraka za mzaz muhimu na ni amri ya Mungu atakama ajafika basi atoe baraka zake kama ajafika lizima ujue reason uombe radhi unless unaweza pata laana

Hiyo yako mkuu...ni kwa wanaoamini imani hiyo* Kwa mm ninayeamini jua na mwezi unanipa rejea gani ya kuniongoza ambayo nitaikubali??? KISAYANSI.....kwa tafiti, na mifano anuai nipe muongozo!
 
Nadhani kuna mambo mawili yanweza kuwa sababu kubwa.

Mosi,Unaweza kukuta Bibi Harusi alikuwa mchepuka wa Baba

Pili unaweza kukuta Bwana harusi si mtoto wake Baba kashtuka dakika za mwisho.
 
Angemlazimisha sana yangekuwa kama haya ImageUploadedByJamiiForums1432016785.029524.jpg
 
awezi kukataa kwenda bila ya sababu,hapo kuna kitu si bure
 
Kumdharau aliyekuleta duniani ni uhayawani wa hali ya juu. baba sio mjinga asihudhurie arusi ya mwanawe lazima kuna sababu.

Kufulia sio dhambi kama baba kafulia kama wanavodai baadhi ya wachangiaji humu hilo sio kosa ila kuwa na pesa ambazo ni matokeo ya wizi na uharamu mwingine ndio kosa. kabla mtu hujajidai na kudharau wengine kuwa una pesa jiulize hizo pesa ulizonazo ni matokeo ya shughuli halali?

Mtoto akishakua ana uhuru wa kutowasikiliza wazazi wake ikiwa yeye anaona hilo ni busara kwake. Baba/mzazi ana haki ya kusimamia jambo analoliamini ndio sahihi wewe mtoto kama hutaki basi songa mbele lakini usimlazimishe mzazi akubaliane na jambo analoliona ni upuuzi/ukosefu wa adabu.

Mzazi ana haki ya kuingilia ndoa ya mwanae. Bila mchango wa mzazi usingekuwa hapo ulipo ila kama unamuona kapitwa na wakati kama mnavyodai wewe songa mbele kistaarabu bila kashfa.

Huko mbele ya safari utajua kuwa Mzazi ni Mungu wa dunia.
 
None Sense!! utakuwa ni mzee uliyechezea maisha.
 
None Sense!! utakuwa ni mzee uliyechezea maisha.

Hiyo ni hoja mufilisi inayotokana na uvivu wa kufikiri.
Kwa nini ulazimishe baba fafanye kitu ambacho hataki? kama unadhani unafanya jambo sahihi kwa nini ulazimishe kuungwa mkono?
 
Mzazi hawezi kuwa Mungu maana kuna Mungu mmoja tu.
Kama waabudu shetani basi mzazi wako atakuwa mungu wako.
We are all made of God's image Baba na mtoto wote hufa na huko mbinguni hapatakuwa na Baba wala Mtoto
 
hao wazee sometimes wanazingua wengi wao ni wastaafu sasa hana hela kama zamani, so kila kitu anaona amedharauliwa, matokeo yake misuso holela kama hiyo

Kama hana hela, wewe mtoto aliyekuzaa na kukusomesha si ndiyo unapaswa kurudisha fadhila, hata kama hajakuomba?!
 
Kwa Baba anayejitambua hapaswi hata kufikiria kukosa harusi ya mwanae wa kumzaa, hiyo ni siku muhimu kwa maharusi, wazazi na jamii kwa ujumla (Hasa ya Kitanzania) kutohudhuria bila sababu ya msingi ni kutafuta doa kwa maharusi kwa kipindi kirefu cha maisha ya hao maharusi. Nilichogundua maharusi wa design hii ya kususiwa harusi huwa na mafanikio makubwa sana (nina ushahidi wa Couple 2) maana hushikamana na kuheshimiana maana wao hujiona wakiwa so wanaona bora tukomae kivyetu tu
 
wazee wetu wa kibongo wana mambo mengi hapo ukute alitaka amuonje binti yeye kabla ya kijana ndo maana kasusa
 
my sister hili la kwangu ni more than that, sijawahi kuishi maisha ya beef ila nafundishwa kwa mara ya kwanza.

kuna vitu havivumiliki ila tu kwa sababu mambo yetu serious wengine huwa tunabaki nayo moyoni hatuyaleti hapa kwa sababu hakuna wa kuelewa chanzo cha haya yote, nasikitika sana nafundishwa roho mbaya ambayo muhusika/wahusika haitawahathiri bali innocent people ndio watakuwa wahanga wa hili.

Jitahid tahidi mkuu kupunguza kisasi kidogo.kuna watu wengine wamekuja dunian kwa ajili ya kuumiza watu tu.jitahidi utoe kinyongo mkuu nakuomba
 
aisee mi mambo ya ndugu ndugu kwenye harusi sitaki kabisa, ikiwezekana siku ya kufunga ndoa twende watu wa 4 inatosha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom