Baba kususa kuhudhuria harusi ya mwanae

connections

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
1,737
2,325
Wajameni Jumamosi nilihudhuria harusi ya rafiki yangu pale KIRAMUU Hall, Mbezi sasa kabla bwana harusi hajaingia ukumbini nilimsikia akihaha kumpigia simu Baba yake (Baba Mzazi) ambae anaishi hapo Mbezi Tangi Bovu ambae alikataa uja kanisani pia ukumbini, bwana ilibidi baada ya kutoka kanisani apitie nyumban kucheck kulikon baba hajaja kanisani akamkuta mzee anaangalia TV comfortably kama hakuna kilichotokea.

Pamoja na kumsihi bado mzee hakutokea.

Hii ni sawa wajameni.

Au ndo ukauzu
 
Tatizo ni nn mpaka baba asitokee,tuelezee tatizo kwanza ndio na sisi tushuke,lakin sio mbaya kama kasha funga,baba yeye sio padri wakufungisha ndoa

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
Inauma kwa kweli lakini maisha inabidi yaendelee. Hao maharusi washikamane kwa kweli wajue baba hayupo upande wao so wakipambana wajue ni wao peke yao. Lakini ipo siku huyo mzee atakuja kujua kosa alilofanya.
 
Cheki masuala ya dini/imani, isije ikawa bwn harusi kabadiri dini tofauti hili limeisha wahi kunitokea kwenye familia yetu, mtoto/binti wa bro, bro aligoma kabisa kuja kwenye harusi hata mahari aligoma kuchukua so ikabidi mimi na dada zake ndio tu take cover! Ni noumer.
 
think TWICE thinks beyond

hapa tupo kweny giza nene maswali bila majibu

mzazi ndo watu wanaofurahi pindi kijana anapooa /kuolewa

sasa ukiona kinyume jua kuna jambo zito

hueda baba na mtoto wana bifu kubwa na kama utaelezewa utaona ni sahihi hakuja kwenye ndoa
au baba ndo mwenye makosa

tungepata background ya story hadi kufika hapo tungeweza kujadili kwa kina kwanini baba mzazi hakuja
 
The same happened to my sister (mtoto wa baba mkubwa). Alisusiwa harusi na wazazi na ndugu eti kwa sababu familia ya mwanaume wana kasumba ya kutelekeza wake!Walifunga ndoa bila ndugu za mke lakini baadae walisuluhishana maisha yakaendelea. Mungu nae ana yake, sister alifariki akabaki mumewe, hajaoa huu karibu mwaka wa 10 na anawalea wazazi wa mkewe kama wazazi wake!Yaani sijui baba mkubwa akikumbukaga ubaya alomfanyia huwa anaajisikiaje!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom