Hukuchanga sababu wenyewe hawatoi ushirikiano/ hawakuchangia kwenye harusiyako au ni kwasababu ulichoka na michango?
my sister hili la kwangu ni more than that, sijawahi kuishi maisha ya beef ila nafundishwa kwa mara ya kwanza.
kuna vitu havivumiliki ila tu kwa sababu mambo yetu serious wengine huwa tunabaki nayo moyoni hatuyaleti hapa kwa sababu hakuna wa kuelewa chanzo cha haya yote, nasikitika sana nafundishwa roho mbaya ambayo muhusika/wahusika haitawahathiri bali innocent people ndio watakuwa wahanga wa hili.
Huyo mzee hana akili hata kidogo Baba ndio Mungu wa dunia. Maadam mzazi alitimiza wajibu wake wa kumzaa na kumtunza hadi akawa mtu mzima kama ukimuona mjinga sawa. Lakini mzazi hawajibiki kusapoti jambo ambalo yeye analiona ni la kijinga sababu tu mtoto anatalika. Hivi wangekuwa wako ulaya na mtoto anafunga ndoa ya jinsia moja na baba anapinga bado ungemlaumu? Maana pia kwa wazungu ni kitu cha kawaida kufunga ndoa ya jinsia moja. Kuna tofauti ya kuoa na kuokotana kwa ajili ya kusukuma. Ndoa ngapi zinazofungwa na kuvunjika kabla hata ya miezi sita.
Tatizo ni kwamba wazee wengi hawatimizi majukumu yako (wanakwepa) sasa watoto wakifanikiwa na kuamua kuoa (kuachana na usela) mzee anaona amedharauliwa na kuweka mgomo baridi. Sasa nyie wazee endeleeni na misuso ya kijinga vijana watawaacha hapo na upuuzi wenu. MTASUSA SANA.
Inawezekana pia kuwa mwenye Kosa ni kijana.Inauma kwa kweli lakini maisha inabidi yaendelee. Hao maharusi washikamane kwa kweli wajue baba hayupo upande wao so wakipambana wajue ni wao peke yao. Lakini ipo siku huyo mzee atakuja kujua kosa alilofanya.
Hii inanikumbusha Harusi ya rafiki yangu ambaye Baba yake hakufika ukumbini kwenye sherehe na wala kanisani hakwenda. Ilibidi tuwadanganye wageni waalikwa kwamba Baba alikuwa safari na wakati wowote ataingia, tukitarajia labda angekuja. Mpaka sherehe inaisha saa 6 usiku hakujitokeza. Angalau tuliijua sababu ya kutokufika kwake, alifungiwa ndani na mkewe kwani baba aliisha achana na Mama wa Bwana Harusi. Mke wa sasa wa mzee alijua hiyo ni nafasi ya mzee kukutana na mkewe wa zamani akaamua kumfungia ndani wakati yeye yuko nje ya nyumba na funguo.
Wivu mwingine mbaya sana.
Tiba
Huyo mzee nae mjinga hajitambui au kalogezewa wanasema.