Baba bado anaendelea kuchukuliwa poa kwenye jamii

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Screenshot_20240311-120412.jpg


"Formula yangu ni ile ile mwaka wa 7 sasa. Nikimtumia baba pesa X mama 2X" - Idriss Sultan

Vijana kama hawa wakizeeka ndio wanaongoza kutoa lawama kwa watoto wao wa kiume kuwa wanaegemea sana kwa mama wakati utaratibu waliuanza wenyewe.
 
Hizi mambo mkuu zisikie tu. Mimi huwa hata sijui wanawake wana nini aisee, sijui huwapa nini watoto ila kuna kitu huja automatically tu inakua hivyo.

Mimi mwenyewe naweza kuwa mfano kwenye hili. Mimi wazazi waliyengana nikiwa niko darasa la 2 hivi. Sisi tukawa tunaishi na mama. Nilipofikabla nne mimi na mdogo wangu wa kiume tulienda kuishi na baba hadi namaliza la saba nikaenda sekondari hadi advance ni baba ndio anapambana kwa kila kitu. Wakati tunaishi na baba akili zilianza kuelewa mambo na kujuabkuwa mama ndio alikua adui mkubwa sana wa baba. Kuna series ya matukio nikiandikabhapa hapatoshi ambayo mama alikua akimfanyia baba kwa sababu ya ubinafsi wake hadi wakaachana.

Baada ya kumaliza chuo kwa nguvu na kupambana kwa baba nilianza kujitegemea hapo ndio niliuona utofauti wa mama na baba. Hadi hapa mama alikua akiishi kwenye nyumba ya nyasi na udongo, ila baada ya kuanza kupata vicenti mzee alituambia watoto wake wote tumjengee mama etu tusimwangalie yeye, yeye bado anajiweza. Kimsingi huu ujumbe ulikua unakuja kwangu direct kwa sababu mm ndio kidogo nilionekana naweza fanya jambo.

Nilimjengea mama baada ya miaka miwili akahamia kwenye nyumba ya tifali na bati. Nilifanya hivyo bila kujali laana alizowahi nitamkia mama. Yaan mama ilikua kila mkipishana hana lingine zaidi ya kukulaani. Wakuu duniani hakuna laana lawa baraka. Kungekua na laana mm nisingefika nilipobjapo ni padogo.

Baada ya kumjengea mm ndio nilikua msaada mkubwa kwa mama kwa mahitaji yake kwa zaidi ya 70% hizo nyingine ndio yeye na watoto wake wengine. Ila mama alikua mtu wa drama sana kwa baba hadi sisi watoto na ilifika hatua akaanza kuingiza drama hadi kwa wajukuu.

Kutu ambacho baba yangu alifaidi kwangu ni kumnunulia shamba na labda vi mavazi tu, ila ndio mtu aliyenipambania shule yangu A-Z mama hajawani ninunulia hata penseli ya shule ya kuchorea panzi.

Itoshe kusema wanawake sijui huwa wanatupa nini hadi inakua ilivyo, japo naamini wapo wamama wanaojali watoto kuliko baba, ila sikuiona kwangu.

Kwa mantik hii, ninaona umuhimu wa wanaume kujiandaa wenyewe bila kutegemea kuwa wana watoto aisee, watoto huegemea kwa mama no mara waa.
 
View attachment 2931262

"Formula yangu ni ile ile mwaka wa 7 sasa. Nikimtumia baba pesa X mama 2X" - Idriss Sultan

Vijana kama hawa wakizeeka ndio wanaongoza kutoa lawama kwa watoto wao wa kiume kuwa wanaegemea sana kwa mama wakati utaratibu waliuanza wenyewe.
Ndoo maana Mimi nawekeza sana kwenye vitega uchumi vyangu binafsi zaidi kuliko nnavyowekeza kwa wanangu maana ndugu wa kweli wa mwanaume pale anapozeeka ni akiba yake tu.
 
View attachment 2931262

"Formula yangu ni ile ile mwaka wa 7 sasa. Nikimtumia baba pesa X mama 2X" - Idriss Sultan

Vijana kama hawa wakizeeka ndio wanaongoza kutoa lawama kwa watoto wao wa kiume kuwa wanaegemea sana kwa mama wakati utaratibu waliuanza wenyewe.
Baba Hana thamani hadi Afariki, ni kama Tamaduni Baba kutokupewa uzito

Utatafuta ela watoto watakula na kushiba kisha watasema "Nani kama Mama"😎😎
 
Back
Top Bottom