saidi kindole
JF-Expert Member
- Sep 21, 2012
- 310
- 792
Wakati huu dondoo kubwa ya taifa na ambayo serikali yetu inaipa msukumo mkubwa ni mapambano dhidi ya kirusi corona. Mapambano haya hayana mzaha wala kebehi na yanadai umoja na mshikamano wa kitaifa. Usemi wa Ndg. Polepole kwamba corona ni sawa na wapinzani ni lugha ya mtu anayeligawa taifa katika kipindi hiki kigumu.
Malezo yake mengine juu ya corona na madhara yake sina shida nayo. Bali kauli hii ya kebehi na kugawa watu katika makundi ya kisiasa wakati huu inamuonyesha yeye ni mtu wa jinsi gani. Kauli hiyo japo ya maneno machache imechujua hata mambo mengine aliyozungumza.
Wakati mwingine tunatamani kuwa mbali na baadhi ya watu kwa sababu uwepo wao huongeza mahangaiko ya mioyo. Mtu ni utu. Na utu ni kutambua uwepo wako na uwepo wa wengine hali tukitambua kuwa kila mtu anayo nafasi yake ya kuishi na kuitawala himaya yake ya maisha (personal doom).
Haya twaweza kuyatambua ama kwa akili au kwa hekima ambapo vyote viwili ni vipawa tulivyopewa na Mungu. Wakati mwingine akili zetu zaweza kushindwa kuchambua na kufikia maamuzi ya nini cha kusema au kufanya. Katika hatua kama hiyo ndipo huruhusu hekima kuingilia mchakato wa kufikiri kwa akili na kutupa mwongozo. Mara nyingi hekima hutuambia kwamba tutulie kwanza na kuahirisha maamuzi. Hekima hukinga maangamizi yawezayo kusababishwa hata na akili zetu.
Tunapomuomba Mungu atupe vipawa iwe pamoja na kumuomba kwamba vipawa anavyotupa vifanye kazi kwa ushirikiano. Kwa akili na hekima ushirikiano huo huwa wa kwenda sambamba pale tunapoamua mambo mema. Lakini pia wakati mwingine vipawa hivyo hufanya kazi pamoja kwa kutofautiana. Pale akili zinapofanya maamuzi kwa pupa hasa katika mambo ya maangamizi ni vema hekima ipewe nafasi ya kukataa ili kuepusha madhara.
Wakati huu wa kupambana na janga la kirusi corona tutapingana na mtu yeyote anayethubutu kutugawa na kuhangaisha mioyo ya watu kwa maneno yake. Tayari hofu ya corona inaleta mahangaiko mioyoni mwa watu. Taifa halihitaji kuongezewa hofu. Kinachohitajika sasa ni faraja na kuwapa watu matumaini ya kuishi. Sasa tunapambana na janga hili kama Watanzania na wala sio kama CCM na wapinzani. Pale akili zetu zinaposhindwa kufikiri au zinapofikiri vibaya basi tuipishe hekima itupe muongozo wa mambo ya kuzungumza na kufanya.
Mungu ibariki Tanzania!
Mungu tupiganie kama taifa