Baba Askofu Bagonza: Jina la Edward lina maana kubwa Monduli

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
Tar 17/2/2024 tumemzika EDWARD Lowasa. Miaka 40 iliyopita tulimzika EDWARD Sokoine eneo hilohilo la Monduli. Tulivyomzika Edward yule ndivyo tulivyomzika Edward huyu. Jina “Edward” lina maana kubwa katika eneo hilo.

Yalikuwa mazishi yenye hadhi. Usingejua kama ni ya Waziri Mkuu Mstaafu. Hata Waziri Mkuu aliye madarakani bado yangemfaa. Hisia za Huzuni, furaha, fahari, aibu na fundisho zilitawala msiba.

Niliyotafakari;

1. Aliondoka Monduli akiwa amesimama. Amerudi amelala. Kulala na kusimama vina nguvu na hadhi sawa. Tuwe wanyenyekevu.

2. Ameunganisha taifa japo kwa siku moja. Wote tulikaa kwa adabu na utulivu na kusahau kwa muda tofauti zetu.

3. Mitandao inamsema vizuri na kuwazodoa "wabaya" wake. Fupisheni hukumu zenu. Yawezekana alishawasamehe.

4. Nimeshangaa kutowaona niliodhani wangekuwepo na kuwaona niliodhani wasingekuwepo. Nimeshangaa wandaaji kupopoa historia yake iliyobeba haiba yake ya MAAMUZI MAGUMU.

5. Nilitamani aliyemteua Waziri Mkuu atusalimie. Hakupewa nafasi. Ukisikia msiba, hiyo ndiyo maana yake. Lakini pamoja na yote bado alihudhuria mazishi. Ishara ya uungwana.

6. Nilihesabu mizinga 16, jirani akahesabu 17. Mwingine akasema ilitakiwa 21. Timu ya itifaki ilitoa tahadhari kwa wenye mimba; ikatusahau tusiojua mizinga 16/17 na 21 ina maana gani? Akifa mwingine mtuelimishe.

7. Mbowe “aliiba onyesho” msibani. Alipata fursa kusalimia kama mwanafamilia. Akainadi Chadema. Akaboresha historia ya Edward. Samia akaikamilisha. Siku yenye huzuni ikaisha vizuri. Tukasikia makofi msibani.

8. Tulipomzika Sokoine, tulizika darasa la uongozi. Lowassa, tumezika maabara ya uongozi. Mmoja aliamini ktk ufukara mtakatifu mwingine ktk utajiri-uzalendo. Tusihemke. Tutafakari.

9. Lowasa ameacha msiba mkubwa kuliko msiba wa kifo chake. Kizazi cha viongozi ambao Mungu wao ni tumbo na mbingu yao ni madaraka.

10. Monduli ilikuwa ndogo siku ya mazishi. Waliozoea kula nyama alipokuwa hai, wamekula zaidi alipokufa. Wengine hatukusikia njaa pamoja na kutokula. Kwaresima ya 2024 tutaikumbuka kwa kushinda njaa tukizika. Fredy muenzi babako kwa kuwapa watu nyama walizozizoea alipokuwa hai.!
 
Mwambieni Askofu Bagonza kwamba ..Tofauti ya mazishi ya kiserikali na Kitaifa ni Hadhi/ Itifaki- ambapo Jeshi la wananchi linahusika, Mizinga 21 hupigwa Kwa Rais aliyeko madarakani au Mstaafu, Makamu wa Rais aliyeko mdarakani au mstaafu ni mizinga 19, Waziri Mkuu ni mizinga 17.. tofauti ipo kwa siku za maombolezo ambapo Waziri Mkuu aliyeko Madarakani siku 7 za maombolezo na Mstaafu 5, Rais aliyeko Madarakani ni siku 21 mstaafu ni siku 14. Makamu wa Rais aliyeko madarakani ni -Siku 14 mstaafu 7.
 
Back
Top Bottom