frem zero
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 595
- 875
Jamani mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hapa jirani kuna baba mmoja ambae ana watoto wawili wa kiume. Baba huyu inasemekana ni jambazi wa kutupwa. Aliwafundisha watoto wake ujambazi na namna ya kuua watu. Mtoto wake mmoja yupo gerezani huu mwaka wa 15, na huyu mwingine kamaliza kifungo miezi miwili iliyopita.
Sasa hapo juzi ulitokea ugomvi kati yake na mwanae alietoka gerezani. Mtoto kaamua kumchinja baba yake kisha kumchimbia shimo ili kupoteza ushahidi. Kabla hajatimiza azma yake watu wakatokea na ndipo uovu wake ukawa hadharani. Kijana huyo sasa yupo mahabusu, na taratibu za mazishi zinaendelea.
NB: wazazi waleeni watoto katika njia ipendezayo machoni pa Mungu nao hawataiaacha hadi uzeeni kwao.