Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 71,727
- 128,690
Umewahi kugombea nafasi yeyote na ukakutana na unajisi wowote, au unasikia tu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani unahisi unaongea na mimi kwa kupoteza muda. Haya ninayokuambia ya kunajisi box la kura sihadithiwi bali nimeyaona kwa macho yangu. Kibaya zaidi mambo haya yanafanyika mbele ya watu wa tume ya uchaguzi, na uratibu wa jeshi la polisi. Huenda ww ni mtu wa ofisini au mtetea uovu, hivyo unadhani yanayosemwa ni mambo ya kutunga. Unapoona wananchi wengi hawajitokezi tena kupiga kura ujue sio wajinga. Na kibaya zaidi mambo haya ya kihayawani na ukatili wa wazi kwenye chaguzi zetu, yamekuwa wazi zaidi baada ya Magufuli kuingia madarakani. Nadhani uliona kilichotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Na hata uchaguzi wa sasa kama hakutakuwa na tume huru vya uchaguzi, hakuna mtu mwenye akili timamu atashiriki huo ushenzi. Rudi nchini uje ujionee mwenyewe, acha mambo ya kuhadithiwa na watu ulio na mahaba nao, maana watakuambia mambo ya uongo.