mtingi1
JF-Expert Member
- Mar 21, 2020
- 945
- 923
Wasalaam wana JF!
MOLA tuepushe na janga la Corona Amina.
Kuna watu huwa wanasema wakiwataja baadhi ya wanasiasa hususani wapinzani, kwamba watukomboe dhidi ya utawala uliopo wakimaanisha CCM.
Huwa najuliuliza huwa wanamaanisha kitu gani hasa? Kwa kuwa wanaotawala ni Watanzania wenzetu, wenye familia na mfumo wa maisha kawaida kabisa na sisi.
WanaCCM, WanaCHADEMA, wana CUF, ACT na vyama vyote, wote ni Watanzania wenye akili tofauti, imani tofauti, mitazamo tofauti, chama chochote kinachopata nafasi kutuwala kitawatumia watanzania hawahawa katika administration yake.
Hakuna chama kitakuja na brand ya Watanzania tofauti na sisi tuliopo, kitatawala na hawahawa tuliopo.
Wezi watakuwepo, mafisadi watakuwepo, waadilifu watakuwepo pia.
Binafsi sioni chama ambacho mtu atanishawishi kusema eti kitaleta ukumbozi, ni uongo!
USHAURI WANGU:
Ikiwa tutakuwa na KATIBA ambayo itaweka malengo ya Tanzania mbele kwamba chama chochote kitakacho tawala, basi kielekeze katika malengo MAMA.
Tusitegemee ILANI ZA VYAMA pekee, So kama taifa tufikiri katika kuboresha katiba YETU.
Tujiwekee malengo ya muda mrefu kama taifa, KATIBA bora ndio dili kwa mtazamo wangu.
JITAHIDI KUWA MWAMINIFU KWA NAFASI YEYOTE UNAYOPATA KUTUMIKA, SIKU MOJA UTATOA HESABU KWA MUNGU. USILAUMU MTU, WEWE KATIKA NAFASI ULIOPO NI MWAMINIFU KIASI GANI?
KILA MMOJA WETU AKIWA MWAMINIFU TUTALIJENGA TAIFA LETU PAMOJA
Hata hivyo naukubali utendaji wa mh John P. Magufuli.
Ni hayo tu....
Sent using Jamii Forums mobile app