huku Magufuli unayemkubali akiwa kikwazo namba moja wa katiba bora
Katiba ya wananchi ndio mwiba mkali ambao CCM [ read Magufuli] wanaogopa kwani with a level playing field even within ccm Meko will have a very tough COVID-19 time!!!
huku Magufuli unayemkubali akiwa kikwazo namba moja wa katiba bora
That explains your weird responses!
Katiba ya wananchi ndio mwiba mkali ambao CCM [ read Magufuli] wanaogopa kwani with a level playing field even within ccm Meko will have a very tough COVID-19 time!!!
Akili tofauti = ccm imeshindwa namna ya kufikiri nini kinatakiwa katika muda tuliopo sasa na huko tunako kwenda. Imani tofauti = ccm ina amini katika nguvu ya dola. Bila matumizi ya dola haiwezi kushinda uchaguzi. Mitazamo tofauti = ccm ina mtazamo kwamba kila mwenye mtazamo tofauti na raisi ama serikali basi aidha ni mchochezi ama si mzalendo, na mbaya zaidi ni kwamba hili linawakumba wasio kuwa wana ccm. Kwa wana ccm hali iko tofauti hata kama mtu atakuwa na mtazamo unao pingana hata na haki za wengine utatoka utetezi ya kwamba kauli yake haikueleweka ama imetafsiriwa vibaya. Akili tofauti = Wapinzani wamekaa na kufikiri ya kwamba ili tuondoke hapa tulipo tunahitaji katiba mpya, mambo mengi yanayo turudisha nyuma ni mamlaka makubwa aliyo nayo raisi kwa mujibu wa katiba, ambayo kwa hali ya dunia ilipofikia ni kwamba imepitwa na wakati. Hivyo suala la katiba mpya halikwepeki. Imani tofauti = Wapinzani wanaamini katika nguvu ya umma na uongozi wa kiraia sio nguvu ya dola. Na chanzo chake ni tume huru ya uchaguzi ili kupata viongozi waliochaguliwa na wananchi sio viongozi wakupangiwa kwa nguvu ya dola. Mitazamo tofauti = Wapinzani wanamtazamo wa kwamba siasa si uadui, na kila mtu anayo haki yakutoa maoni yake kwa mujibu wa sheria. Miongoni mwa vipengele ulivyo orodhesha hivi vitatu ni muhimu zaidi na hata huyo unae muamini nakumsifia ameshindwa kuvisimamia chini ya ccm. Hivyo ccm inatakiwa kupumzishwa ili iingie nguvu nyingine tuweze kuendelea.Wasalaam wana JF!
MOLA tuepushe na janga la Corona Amina.
Kuna watu huwa wanasema wakiwataja baadhi ya wanasiasa hususani wapinzani, kwamba watukomboe dhidi ya utawala uliopo wakimaanisha CCM.
Huwa najuliuliza huwa wanamaanisha kitu gani hasa? Kwa kuwa wanaotawala ni Watanzania wenzetu, wenye familia na mfumo wa maisha kawaida kabisa na sisi.
WanaCCM, WanaCHADEMA, wana CUF, ACT na vyama vyote, wote ni Watanzania wenye akili tofauti, imani tofauti, mitazamo tofauti, chama chochote kinachopata nafasi kutuwala kitawatumia watanzania hawahawa katika administration yake.
Hakuna chama kitakuja na brand ya Watanzania tofauti na sisi tuliopo, kitatawala na hawahawa tuliopo.
Wezi watakuwepo, mafisadi watakuwepo, waadilifu watakuwepo pia.
Binafsi sioni chama ambacho mtu atanishawishi kusema eti kitaleta ukumbozi, ni uongo!
USHAURI WANGU:
Ikiwa tutakuwa na KATIBA ambayo itaweka malengo ya Tanzania mbele kwamba chama chochote kitakacho tawala, basi kielekeze katika malengo MAMA.
Tusitegemee ILANI ZA VYAMA pekee, So kama taifa tufikiri katika kuboresha katiba YETU.
Tujiwekee malengo ya muda mrefu kama taifa, KATIBA bora ndio dili kwa mtazamo wangu.
JITAHIDI KUWA MWAMINIFU KWA NAFASI YEYOTE UNAYOPATA KUTUMIKA, SIKU MOJA UTATOA HESABU KWA MUNGU. USILAUMU MTU, WEWE KATIKA NAFASI ULIOPO NI MWAMINIFU KIASI GANI?
KILA MMOJA WETU AKIWA MWAMINIFU TUTALIJENGA TAIFA LETU PAMOJA
Hata hivyo naukubali utendaji wa mh John P. Magufuli.
Ni hayo tu....
Sent using Jamii Forums mobile app