Baadhi ya Watanzania wanashangaza sana

Baadhi ya Watanzania wanashangaza sana

Wasalaam wana JF!

MOLA tuepushe na janga la Corona Amina.

Kuna watu huwa wanasema wakiwataja baadhi ya wanasiasa hususani wapinzani, kwamba watukomboe dhidi ya utawala uliopo wakimaanisha CCM.

Huwa najuliuliza huwa wanamaanisha kitu gani hasa? Kwa kuwa wanaotawala ni Watanzania wenzetu, wenye familia na mfumo wa maisha kawaida kabisa na sisi.

WanaCCM, WanaCHADEMA, wana CUF, ACT na vyama vyote, wote ni Watanzania wenye akili tofauti, imani tofauti, mitazamo tofauti, chama chochote kinachopata nafasi kutuwala kitawatumia watanzania hawahawa katika administration yake.

Hakuna chama kitakuja na brand ya Watanzania tofauti na sisi tuliopo, kitatawala na hawahawa tuliopo.

Wezi watakuwepo, mafisadi watakuwepo, waadilifu watakuwepo pia.

Binafsi sioni chama ambacho mtu atanishawishi kusema eti kitaleta ukumbozi, ni uongo!

USHAURI WANGU:

Ikiwa tutakuwa na KATIBA ambayo itaweka malengo ya Tanzania mbele kwamba chama chochote kitakacho tawala, basi kielekeze katika malengo MAMA.

Tusitegemee ILANI ZA VYAMA pekee, So kama taifa tufikiri katika kuboresha katiba YETU.

Tujiwekee malengo ya muda mrefu kama taifa, KATIBA bora ndio dili kwa mtazamo wangu.

JITAHIDI KUWA MWAMINIFU KWA NAFASI YEYOTE UNAYOPATA KUTUMIKA, SIKU MOJA UTATOA HESABU KWA MUNGU. USILAUMU MTU, WEWE KATIKA NAFASI ULIOPO NI MWAMINIFU KIASI GANI?

KILA MMOJA WETU AKIWA MWAMINIFU TUTALIJENGA TAIFA LETU PAMOJA

Hata hivyo naukubali utendaji wa mh John P. Magufuli.

Ni hayo tu....

Sent using Jamii Forums mobile app
Big up mkuu umeongea point nzuri Sana watu Kama wewe ndo walitakiwa kuwa wengi humu jamiiforum you're great thinker
 
Sijui hata kama unaelewa ukisemacho mkuu! Anyway mh Magufuli ndio amri jeshi mkuu! Kumbuka hilo, binafsi sio mwanachama wa chama chochote, naipenda nchi yangu tu
Inaonekana ww ni muabudu sanamu, unataka kumgeuza kuwa yeye ndio mwenye ruhusa ya kupatikana kwa katiba. Kwahiyo mpaka hapo alipo hajaafiki kwakuwa hajafanyiwa approach nzuri? Hatuhitaji hisani yake ili kupata katiba mpya, hata tusipoipata chini ya utawala wake, tutaipata tu. Kama ww unahitaji hisani yake kamuombe kwa hiyo approach yako nzuri. Sisi tunataka katiba mpya kwa amani, ikishindikana kwa njia ya amani, tutaipata kwa njia nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simtegemei mtu, ila mh John P Magufuli ndio amri jeshi mkuu, tukiwa na approach nzuri tutakuwa na KATIBA bora katika wakati wake, hio ndio idea yangu mkuu
Yeye ana imani na chama cha ACT, ila ww una imani na mtu! Miaka hii dunia inaoongozwa na mifumo, ww bado uko kwenye dunia ya kusujudia mtu! Mkuu endelea kuvuta shuka kwenye huo usingizi wa kuamini katika nguvu ya mtu. Alaaniwe amtegemeaye mwanadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ub
Inaonekana ww ni muabudu sanamu, unataka kumgeuza kuwa yeye ndio mwenye ruhusa ya kupatikana kwa katiba. Kwahiyo mpaka hapo alipo hajaafiki kwakuwa hajafanyiwa approach nzuri? Hatuhitaji hisani yake ili kupata katiba mpya, hata tusipoipata chini ya utawala wake, tutaipata tu. Kama ww unahitaji hisani yake kamuombe kwa hiyo approach yako nzuri. Sisi tunataka katiba mpya kwa amani, ikishindikana kwa njia ya amani, tutaipata kwa njia nyingine.
Mkuu, huo ubavu wa kufanya chochote, unapowatathimi Watanzania unauona kweli ndani Yao kwamba wanaweza kufanya hivyo?

Uhuru wetu Sisi tuliupata Kwa kuomba tena tumeweka mikono nyuma mgongoni,. Leo tunaweza kweli, binafsi Nataka iwepo katiba mpya tutakayoipendekeza Sisi raia lkn ikiwa ni kuipata Kwa njia hiyo nyingine, mkuu, Niko tayari kuitwa mwabudu miungu,
 
Sijui hata kama unaelewa ukisemacho mkuu! Anyway mh Magufuli ndio amri jeshi mkuu! Kumbuka hilo, binafsi sio mwanachama wa chama chochote, naipenda nchi yangu tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli ni Amiri jeshi mkuu hilo sipingi, lakini hicho cheo ni tunda la katiba. Naona unadhani hicho cheo ni zaidi ya katiba ndio maana unadhani ni hisani yake kupatikana kwa katiba.
 
Simtegemei mtu, ila mh John P Magufuli ndio amri jeshi mkuu, tukiwa na approach nzuri tutakuwa na KATIBA bora katika wakati wake, hio ndio idea yangu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio lazima tuipate kwa hisani yake, kama alikuwa anaitaka leo hii tungekuwa nayo. Huu ni mwaka wa tano, na iwapo atapata muda mwingine atakuwa kabakiza mitano, kama hatukupata ndani ya hiyo miaka mitano, hatuoni shida sana kuisubiri lakini sio kutegemea hisani yake. Hii kutegemea hisani ya mtu, ndio hutoa mwanya wa kuingiza mambo yenye maslahi binafsi ya watu.
 
Sio hisani najua, lakini katiba inampa mamlaka, sisi na yeye kwa pamoja tunaweza kufanya jambo jema katika kusikilizana na amani
Ni kweli ni Amiri jeshi mkuu hilo sipingi, lakini hicho cheo ni tunda la katiba. Naona unadhani hicho cheo ni zaidi ya katiba ndio maana unadhani ni hisani yake kupatikana kwa katiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisona psychology vema utajua namna ya kudeal na watu pasipo kuwakwaza, jusyan advise mkuu
Sio lazima tuipate kwa hisani yake, kama alikuwa anaitaka leo hii tungekuwa nayo. Huu ni mwaka wa tano, na iwapo atapata muda mwingine atakuwa kabakiza mitano, kama hatukupata ndani ya hiyo miaka mitano, hatuoni shida sana kuisubiri lakini sio kutegemea hisani yake. Hii kutegemea hisani ya mtu, ndio hutoa mwanya wa kuingiza mambo yenye maslahi binafsi ya watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ub
Mkuu, huo ubavu wa kufanya chochote, unapowatathimi Watanzania inawaona kweli wanaweza kufanya hivyo?

Uhuru wetu Sisi tuliupata Kwa kuomba tena tumeweka mikono nyuma mgongoni,. Leo tunaweza kweli, binafsi Nataka iwepo katiba mpya tutakayoipendekeza Sisi raia lkn ikiwa ni kuipata Kwa njia hiyo nyingine, mkuu, Niko tayari kuitwa mwabudu miungu,

Inaonekana unadhani machafuko tu ndiyo njia ya kuipata. Njia zipo nyingi tena za amani. Moja ni kutokutoa ushirikiano kwa serikali iliyoko madarakani, na kuomba msaada wa jumuiya ya kimataifa kutoa Mbinyo. Kwa sasa tumeanza njia hizo zisizoleta machafuko, kama hii ya kususia kupiga kura, hivyo tutakuwa na serikali iliyo kisheria lakini isiyo na uhalali wa umma. Unapokuwa na serikali ambayo haina uhalali wa umma, ni dhahiri itakuwa ngumu kuwa na ushirikiano. Katika mazingira hayo ni kupandikiza chuki ya kijamii mpaka suluhu ipatikane. Kuna kitu kinaitwa nguvu ya umma, nguvu ya umma maana yake sio machafuko tu, bali umma karibia wote kusimamia jambo fulani mpaka lifanyike. Mbinu hii haitaleta machafuko wala kumuacha mtu yoyote na kilema.

Ngoja kwa kumalizia nikupe maana ya nguvu ya umma isiyo na machafuko lakini yenye impact. Mfano ww ni mwanajamii lakini mwenendo wako hauridhishi, siku ukiwa na msiba, sherehe nk watu hawaji kama kawaida, na hata wakija ukiwa umeandaa chakula watu hawali, hizi ni mbinu tu ambazo zitakuridisha kwenye mstari. Huko tuendako tutatumia mbinu hizi ambazo hazitaharibu usalama wa nchi, lakini itatuacha na jamii isiyo na umoja. Hakuna namna utafanya jambo lisilokubalika na baadhi ya wanajamii, tena wakiwa na sababu za msingi kisha watu wasichukue hatua, eti kwa sababu una majeshi basi watokaodai utayatumia kuwaua au kuwatia vilema. Hatubembelezi mtu yoyote kupata haki yetu, ni wajibu wake kutekeleza mahitaji ya umma, na sio utashi wa mtu binafsi.
 
Sio hisani najua, lakini katiba inampa mamlaka, sisi na yeye kwa pamoja tunaweza kufanya jambo jema katika kusikilizana na amani

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kipi hakijafanyika mpaka sasa kinachopelekea hiyo katiba kutokupatikana? Ni amani ipi ambayo haijapatikana mpaka tuone chaguzi za nchi hii zikinajisiwa kwa faida ya chama cha rais?
 
Tuwe na approach vizuri tu, mzee Magufuli anaweza kufanya maamuzi sahihi yatakayopelekea kuwa na KATIBA bora. Busara inahitajika katika hili, tuachane na mihemko ya kisiasa, tuwe na mtazamo wa kuijenga nchi yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwamba tukampigie magoti kiasi kwamba yeye haoni umuhimu wa kua na katiba mpya? Kama anaitaji kubembelezwa na wananchi waliompatia ajira kwa kumpigia kura basi nakosa jina nzuri ya kumpatia.

Yaani wananchi wakatafute njia nzuri ya kumpembeleza mtumishi wao? unayo shida sehemu kwenye utambuzi wa utawala na uongozi ndugu.
 
Ukisona psychology vema utajua namna ya kudeal na watu pasipo kuwakwaza, jusyan advise mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Nakuelewa sana boss, ila hiyo psychology ndio imetufanya tukae miaka dahari tukidai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. Kwa maneno marahisi akitokea mwingine wa hivi tutakuwa tunasoma psychology tu? Kama ni hivyo ww msoma saikolojia, kwanini huendi kumuomba hiyo katiba bora kwa approach yako nzuri?
 
Vema mkuu, machafuko na wazo la mtu muovu, amani ni wazo la mtu mwenye mapenzi mema na nchi yake.

Watu husema machafuko kirahisi ila huwa hawaangalii impact yake, hilio ndio tatizo, imagine majeshi yanzagaa mitaani, mnaambiwa kulala saa 12 jioni, kuna raha tena hapo?

Sisi ni wamoja, na tunaweza kuleta maridhiano sisi wenyewe katika amani na upendo.

Mungu ibariki Tanzania
Inaonekana unadhani machafuko tu ndiyo njia ya kuipata. Njia zipo nyingi tena za amani. Moja ni kutokutoa ushirikiano kwa serikali iliyoko madarakani, na kuomba msaada wa jumuiya ya kimataifa kutoa Mbinyo. Kwa sasa tumeanza njia hizo zisizoleta machafuko, kama hii ya kususia kupiga kura, hivyo tutakuwa na serikali iliyo kisheria lakini isiyo na uhalali wa umma. Unapokuwa na serikali ambayo haina uhalali wa umma, ni dhahiri itakuwa ngumu kuwa na ushirikiano. Katika mazingira hayo ni kupandikiza chuki ya kijamii mpaka suluhu ipatikane. Kuna kitu kinaitwa nguvu ya umma, nguvu ya umma maana yake sio machafuko tu, bali umma karibia wote kusimamia jambo fulani mpaka lifanyike. Mbinu hii haitaleta machafuko wala kumuacha mtu yoyote na kilema.

Ngoja kwa kumalizia nikupe maana ya nguvu ya umma isiyo na machafuko lakini yenye impact. Mfano ww ni mwanajamii lakini mwenendo wako hauridhishi, siku ukiwa na msiba, sherehe nk watu hawaji kama kawaida, na hata wakija ukiwa umeandaa chakula watu hawali, hizi ni mbinu tu ambazo zitakuridisha kwenye mstari. Huko tuendako tutatumia mbinu hizi ambazo hazitaharibu usalama wa nchi, lakini itatuacha na jamii isiyo na umoja. Hakuna namna utafanya jambo lisilokubalika na baadhi ya wanajamii, tena wakiwa na sababu za msingi kisha watu wasichukue hatua, eti kwa sababu una majeshi basi watokaodai utayatumia kuwaua au kuwatia vilema. Hatubembelezi mtu yoyote kupata haki yetu, ni wajibu wake kutekeleza mahitaji ya umma, na sio utashi wa mtu binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umewahi kugombea nafasi yeyote na ukakutana na unajisi wowote, au unasikia tu?
Ni kipi hakijafanyika mpaka sasa kinachopelekea hiyo katiba kutokupatikana? Ni amani ipi ambayo haijapatikana mpaka tuone chaguzi za nchi hii zikinajisiwa kwa faida ya chama cha rais?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kwenye marketing kuna strategy mkuu, na swala la katiba inabidi tuwe na strategy, sio watu kujitafutia umaarufu kisiasa.

Imetupasa kuwa wazalendo, watu wanatafuta umaarufu binafsi hapo ndio kwenye tatizo, hebu nambie ni mwanasiasa gani ana mbinu mbadala za kutafuta namna iliyobora ya kupata katiba nzuri? Mtaje.

Waliopo kila mmoja anatafuta personal recognition. Wanasiasa walio wengi ni wachumia tumbo. Trust me
Kwamba tukampigie magoti kiasi kwamba yeye haoni umuhimu wa kua na katiba mpya? Kama anaitaji kubembelezwa na wananchi waliompatia ajira kwa kumpigia kura basi nakosa jina nzuri ya kumpatia.

Yaani wananchi wakatafute njia nzuri ya kumpembeleza mtumishi wao? unayo shida sehemu kwenye utambuzi wa utawala na uongozi ndugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata andiko langu ni strategy mojawapo, naamini wananisoma watanzania wengi
Nakuelewa sana boss, ila hiyo psychology ndio imetufanya tukae miaka dahari tukidai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. Kwa maneno marahisi akitokea mwingine wa hivi tutakuwa tunasoma psychology tu? Kama ni hivyo ww msoma saikolojia, kwanini huendi kumuomba hiyo katiba bora kwa approach yako nzuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam wana JF!

MOLA tuepushe na janga la Corona Amina.

Kuna watu huwa wanasema wakiwataja baadhi ya wanasiasa hususani wapinzani, kwamba watukomboe dhidi ya utawala uliopo wakimaanisha CCM.

Huwa najuliuliza huwa wanamaanisha kitu gani hasa? Kwa kuwa wanaotawala ni Watanzania wenzetu, wenye familia na mfumo wa maisha kawaida kabisa na sisi.

WanaCCM, WanaCHADEMA, wana CUF, ACT na vyama vyote, wote ni Watanzania wenye akili tofauti, imani tofauti, mitazamo tofauti, chama chochote kinachopata nafasi kutuwala kitawatumia watanzania hawahawa katika administration yake.

Hakuna chama kitakuja na brand ya Watanzania tofauti na sisi tuliopo, kitatawala na hawahawa tuliopo.

Wezi watakuwepo, mafisadi watakuwepo, waadilifu watakuwepo pia.

Binafsi sioni chama ambacho mtu atanishawishi kusema eti kitaleta ukumbozi, ni uongo!

USHAURI WANGU:

Ikiwa tutakuwa na KATIBA ambayo itaweka malengo ya Tanzania mbele kwamba chama chochote kitakacho tawala, basi kielekeze katika malengo MAMA.

Tusitegemee ILANI ZA VYAMA pekee, So kama taifa tufikiri katika kuboresha katiba YETU.

Tujiwekee malengo ya muda mrefu kama taifa, KATIBA bora ndio dili kwa mtazamo wangu.

JITAHIDI KUWA MWAMINIFU KWA NAFASI YEYOTE UNAYOPATA KUTUMIKA, SIKU MOJA UTATOA HESABU KWA MUNGU. USILAUMU MTU, WEWE KATIKA NAFASI ULIOPO NI MWAMINIFU KIASI GANI?

KILA MMOJA WETU AKIWA MWAMINIFU TUTALIJENGA TAIFA LETU PAMOJA

Hata hivyo naukubali utendaji wa mh John P. Magufuli.

Ni hayo tu....

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi acha mimi nikufunue mawazo kwa maneno machache sana, na kama utashindwa kuelewa jua moja kwa moja kwamba huna uwezo kamwe wa kuelewa.

Chama chochote cha siasa kikikaa madarakani hata kilete maendeleo ya aina yote, lakini wananchi wakanyimwa haki ya kuamua kiendelee kuwepo kwenye madaraka au wakitoe.

Hapo wananchi wanayo haki ya kudai ukombozi.

Bado huelewi?
 
Back
Top Bottom