Baadhi ya wanaume humu ni wanafiki sana

Baadhi ya wanaume humu ni wanafiki sana

Nilishatoa malalamiko huku kwamba Kuna mtu aliniomba elfu thelathini na mwingine aliniomba elfu tisini eti kakwama mahali hadi vocha wengine elfu 20 so wapo Matapeli humu wengi tumezoea Mimi sio tajiri wajameni hali ni kawaida tu ukiona business whtsupp ni hakunaga kitu mtu karembesha tu anaomba Mungu amfanyie wepesi aipate sio anayo asingekuja huku kupoteza stress ikute mambo mabaya kiukweli kaja huku apunguze stress unampiga na kitu kizito
Polen Sana mlokutana na kadhia Hiyo
Ila twende mbele turudi nyuma, Unique Flower pesa unazo[emoji12]
 
"Mimi nilisema nafanya kazi kwa hiyo nahitaji mume wangu mtarajiwa pia awe anafanya kazi” Hii namaanisha kuwa sitegemei pesa za mume wangu mtarajiwa kuwa nina zangu, kwa hiyo na yeye pia awe anafanya kazi/biashara ili tusaidiane maisha kwa pamoja ili pia asitegemee pesa zangu mimi tu!!"

.........
Ama kweli Mwafrika hapotezi asili.

Pamoja na kwamba umeishi London toka ukiwa mdogo lakini bado una hulka ya umimi.

Ninakushauri uachane na mpango wako wa kutafuta mume maana unathamini mali na pesa zako kuliko mume.

Ungekuwa na tabia njema hakika ungepata mume maeneo yako ya kazi.
Hapo tayari una helakwa hiyo huon unuhimu mume.
Nakuunga mkono mkuu
 
Shukuru kwa yoote\ kwenye msafara wa Mamba kenge pia hawakosekani, na mijusi pia. kwa fikra zangu na jinsi ninavyoyaona Maisha ya Kibongo bongo kwanza Wanaume wengi wana matatizo ya Afya ya Akili, kwanza sio wanaume, wanawake, watoto, vijana na wazee au kwa Lugha nyepesi Watanzania karibia wote tushavurugwa hatupo sawa, hivyo inapokuja fursa ni fursa kwa wote, inaweza kuwa ni fursa ama fursana kutokana na tulipofikia unaweza pewa fursa huku wewe muhusika ukiwa ndio fursa yenyewe, watu wana bet, hivyo ndugu tegemea lolote katika hitaji lako, unaweza mkataa mtu ambae ndio sahihi kwako kutokana na situation anayopitia, watu wengi waamini na wachamungu hapa Bongo hawana nafasi ya kumiliki hata 5000 kwa siku, sembuse na kuwa na kazi ama kumiliki passport. Husband material wote choka mbaya. kuna kundi flani ambalo kidogo ndio lonaweza hata kumiliki Mwanamke na kumtunza\kumjali lakini nao washakutana na vitu vizito. hapa Mtandaoni kinachofanyika ni mind game, unaweza pata hitaji lako ama unaweza pata Tapeli moja International, lenue vigezo vyoye unavyotaka alafu baadae ukaja lia kilia cha Mbwa mwizi. jaribu njia hii, japo nayo si asilimia 100 lakini inaweza kusaidia kujua kama chaguzi hii uliyoifanya ni sahihi, ukipata likizo Tembelea nyumbani kidogo( Tanzania ) imawezekana tangu ulipoondoka huku ni Miaka mingi imeshapita. kuna Mengi yametokea ambayo yamebadilisha mfumo mzima wa Maisha ya Watanzania kwa Ujumla. njoo nyumbani hapo utajua mengi ambayo nina hakika kwa sasa hujui chochote kuhusu wanachopitia Wanaume wa kitanzania kipindi hichi. karibu Nyumbani ndipo pana jibu la hitaji lako, kuliko hichi unachofanya unaweza kuja kujutahapo Baadae. kila la kheri Mkuu.
 
Humu hakuna watu wakuoa ni bahati sana kama ameamua kuja ila kama hajaamua basi watakutesa kama Nini mie sipo humu kwakuolewa Kwa kusocialize tu nakufurahia
 
Kiukweli jf Kuna Wanaume Wana roho ngumu Sana aisee[emoji848]
mleta mada ni miongoni wa wale watu waongo waongo, wazee wa chai kama ni kweli amtaje!

wanawake kwa uongo wako mstari wa mbele kabisa!
angalia uandishi wake + anachokisema = uongo
 
Humu hakuna watu wakuoa ni bahati sana kama ameamua kuja ila kama hajaamua basi watakutesa kama Nini mie sipo humu kwakuolewa Kwa kusocialize tu nakufurahia
hata hii stori ni ya kufurahisha tu hakuna uhalisia wowote ni uongo
 
Landani kuna wachambaji pia, kama Buguruni kwa mnyamani!!?

Anyway, aina za wanaume hao uliokutana nao wapo wana exist hasa Kinondoni,…

Ila ungekuwa na marafiki wa kiume at least usingeshangaa aina hiyo ya wanaume, kwa usijifungie sana panapowezekana ruhusu marafiki kwa sheria zako.

Kila la kheri.
Tyrone
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sijakataa kumsaidia lakini nilipo muuliza atanilipaje kuwa tuko nchi mbali mbali,
hakuwa na jibu sahihi ndio hapa nikawa na hofu.

Chengine mimi simjui kabisa, kaniomba pesa siku ya pili baada ya kuchat nae.
Isitoshe nilipomwambia sina, kapotea kabisa.

Ndio sasa nasema kwa kutahadharisha wengine kama hizi tabia wanafanyiwa wanawake wengine pia.

Vile vile mimi sio mtu wa kuhukumu au kutukana mtu bali mimi nilitukanwa na kuhukumiwa mnoooo kisa vigezo vyangu kwa mtu ninae tafuta 🙏🙏
Unataka mume? Kama jibu ni ndio basi rekebisha kipengere cha dini Tu ......then utachagua.......achana na maulamaaa wengi hawana shughuli maalumu .........wewe tafuta upande WA pili ujionee.........WA Kwanza Mimi Ila kupima afya itahusika............na je hauna watoto??
 
Jf never boring. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
mleta mada ni miongoni wa wale watu waongo waongo, wazee wa chai kama ni kweli amtaje!

wanawake kwa uongo wako mstari wa mbele kabisa!
angalia uandishi wake + anachokisema = uongo
Ni kweli ameombwa hela na ushahidi na picha zao wapo wanna waliowahi niomba hela
 
Landani kuna wachambaji pia, kama Buguruni kwa mnyamani!!?

Anyway, aina za wanaume hao uliokutana nao wapo wana exist hasa Kinondoni,…

Ila ungekuwa na marafiki wa kiume at least usingeshangaa aina hiyo ya wanaume, kwa usijifungie sana panapowezekana ruhusu marafiki kwa sheria zako.

Kila la kheri.
Tyrone
Ni noma sana kama mpaka landani kuna habari hizo..
 
Kwanza hali zenu nyote na ni wazima pia,
najitahidi mnooo kuheshimu kila mtu lakini

huu mkasa ulionikuta siku chache tu baada ya kujiunga hapa nahisi bora
niulize kuwa siamini kabisa.

Naombeni mnijuze kama pia mna Wanaijiria humu, mbona naaza kuombwa pesa na mbaba mmoja.

Nauliza kama pia Mnawanaijiria humu kuwa bado siamni kabisa, au hii ni tabia
ya (baadhi) wa kina baba/kaka wa kitanzania, kuwaomba pesa kina mama/dada.

Labda kuwa maisha yamebadilika sasa saana huko nyumbani kwa hiyo (baadhi) ya kina baba/kaka sasa pia wanawaomba pesa kina mama/dada??

Mimi nilisema nafanya kazi kwa hiyo nahitaji mume wangu mtarajiwa pia awe anafanya kazi. Hii namaanisha kuwa sitegemei pesa za mume wangu mtarajiwa kuwa nina zangu, kwa hiyo na yeye pia awe anafanya kazi/biashara ili tusaidiane maisha kwa pamoja ili pia asitegemee pesa zangu mimi tu!!

Lakini sasa nimeanza kuogopa mnooo kwa kuanza kuombwa pesa hapa mtandaoni (kwa mtu ambae simjui kabisa mbali ya kuchat nae hapa jukwaani tu baada ya siku chache nilizomjua na nilipomuuliza kwanza utanilipaje kuwa tuko nchi mbali mbali hakuwa na jibu sahihi na niliposema sina sasa kapotea kabisa na sasa nasema hapa jukwaani kwa kutahatharisha wanawake wengine)
baada ya matusi yote niliyotukanwa na kuhukumiwa mnoooo na ( baadhi ya) kina kaka/baba, hata bila ya kufahamu nini nimewakosea.

Vile vile nashindwa kuelewa sasa kuwa
( baadhi ) ya kina baba/kaka humu wanasema kuwa kina dada/mama wanawafanyeni nyinyi chuma ulete.

Kwa hiyo sasa (baadhi yenu) nyinyi humu mnataka kutufanya sisi sasa kina mama/dada chuma ulete!! Au tuseme bibi kizee mimi tu labda kwa sasa. [emoji1787][emoji23]

Naombeni mnijuze kama pia mna Wanaijiria humu au hii ni tabia pia ya
(baadhi) wa kina kaka/baba wa kitanzania kuwachuna/kuwatapeli wanawake. [emoji120][emoji120]

Chengine jamani mimi siajiri watu kazi na wala sijui sheria za kazi huku niliko London. Mimi ninaukaazi wa huku na nafanya kazi zaidi ya hapo sijui sheria nyengine. Kama nilivyosema mimi nilikuja huku nikiwa mdogo kwa hiyo siwezi kumpa mtu yoyote ushauri kuhusu sheria za huku za kazi, vizuri mutizame nyinyi huko kwenye online au mmuajiri wakili akuelezeeni.
Nasema haya kuhusu sheria za kazi kuwa sitaki kusema kitu nisichokijua au kumpotosha mtu yoyote. [emoji2362][emoji2362]

Vile vile nimeona pia ( baadhi ) ya wa kina kaka/baba kutaka urafiki na mimi sasa, niwe muwazi na kusema la ukweli kabisa ili tusipotezeane muda hapa, hasa kuwa niko bizi mnooo na maisha yangu, mimi sio mtu wa marafiki na sina marafiki wa kiume.
[emoji849][emoji15]

Mimi niko hapa kutafuta mume tu na mwenye vigezo vyote, na kama hamna ni sawa pia hama shida hata kidogo, bali nitabaki kwa kusoma threads za watu wengine nitakapo kuwa na muda
ili kujifuza na kufahamu hali ya huko nyumbani sasa.[emoji120][emoji120]
Alieelewa anielekeze[emoji3]
 
Hadi nimecheka. Lol.

Na walijua kweli kujazana kwenye ule uzi wako wa kutafuta mume kumbe wengine walikuwa na malengo yao mengine. Dooh.
 
Back
Top Bottom