Baadhi ya wahindi na hizi biashara

Baadhi ya wahindi na hizi biashara

Duh!!!kwa namna hiyo bora tu niendelee kuwa na hichi kidogo nilichonacho.
Duh wahindi wana Imani za kishirikina sana huwa kuna majani wanayaning'iniza juu ya milango yao ya biashara mara wanachoma mavitu flani fulani ila hili la kugeuza ndugu zao mandondocha ndio hatari.
 
Kuna muhindi mmoja ana filling station ina wateja sana huwa anamleta baba yake kila jioni kwa siku maalum katika week mzee ni zezeta anakuja hapo anajipiga vibao weee analia kama masaa mawili kisha anapakiwa kwenye gari anarudishwa nyumbani
Hahahahahahaha mkuu hii siyo chai kweli?
 
Watahama nchi tu kwa hii huu utawala wa sasa mbona maji wataita mma.
Si unamuona Manji alivyonyooka Manji alikua na dharau mpaka kinyaa alikua anajiona yeye ndio Tanzania Duh ila kwa kweli Magufuli kamnyoosha Manji,

Dewji katumbuliwa kwenye ulanguzi wa korosho wakulima walikua wananyonywa mpaka ukurutu ila msimu uliopita korosho imetajirisha watu hatari bado sasa kwenye viwanda na mashamba ya mkonge aliyonunua bila ya kuyaendeleleza ama kweli kanjubhai number wanaisoma
 
Jamaa alifukuzwa kazi kisa kaanza kuingia ndani kabla ya muhindi, jamaa akakuta kimdoli akakisogeza muhindi kukuta kimdoli kimesogezwa wacha alie hadi kamasi zikamtoka,, jamaaa akaona eeh makubwa si akakishika tena kimdoli akirudishe alipokitoa, mhindi fasta katoa Bastola ntakuua, Juma ikabidi atoke nduki na kazi basi.
Ohooooo mkuu hii kweli au unatuchangamsha hapa.?[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ninadhani swala ni kupinga dharau, hata ya kumiliki uchumi mbona wanawezeshwa na system yetu mbovu ya rushwa ? Marekani imepiga hatua kiuchumi kwa kukaribisha multicultural society
Lakini hutaamini baadhi ya miji marekani kwa sasa wahindi wamevamia na kufungua maduka kwa wingi sana wamerekani wanachukia sana .
 
Tena mumshukuru Magufuli kulikua kuna kikundi cha waasia hawazidi 8 walikua wameshainunua hii nchi yote, unakuta mtu mmoja ana maelfu ya hekari prime areas kwenye kila mkoa mfano ile kigamboni ilikua inamilikiwa na kanjubhai mmoja robo tatu Magufuli akishirikiana na Lukuvi wamewaliza hawa watu hamu nao hawana.
 
1. Wazuri sana ktk Biashara za Magumashi!

2. Kule India kuna wahindi weusi, walivo na roho mbaya hata wahindi wenzao weusi pia wanawabagua, sembuse mimi na wewe wamatumbi!

3. Yote kwa yote, wahindi wanaogopa dola kuliko! Ukifankkiwa kumfikisha ubaoni lazima atakuheshimu tu!
Wapo hata waafrika hasa nchi jirani, wanajiita watanzania huku mioyo yao iko nchi zao. Hao hawana faida nchini.
 
Nathubutu kusema wana tecnic nyingi na uzoefu wa kufanya biashara LAKINI wahindi ni watu wasio na faida hapa nchini, ni bora waondolewe. Kwasababu:-

- Wana Madharau sana na ni Wabaguzi.

Kuna mmoja maarufu Arusha aliwahi kusema kuwa yeye hawezi kushitakiwa na manyani (akimaanisha watu weusi watanzania)

- Wahindi kamwe hawadeposit pesa zao katika local banks za kitanzania na hivyo kuzuia mzunguko wa pesa ndani ya nchi.

Imagine katika matajiri wakubwa sana hapa nchini wengi wao ni wahindi na wameekeza kila mahali kwenye kilimo, madini, viwanda, shule zao, mahosipitali yao n.k lakini pesa zao wanaziweka katika benki za huko India, Canada, Pakistan na Uingereza.

Wanachuma pesa hapa kwetu na kupeleka kwao.

Wanachokifanya ni kuwahonga viongozi wachache wa serikali na mapolisi wenye vyeo kisha wao wanatutreat sisi kama nyani tu.

Wahindi hawana faida katika nchi hii kwani hata kodi wanababaisha kulipa.

-
Yule wa Toyota hapa Arusha?
 
Duh wahindi wana Imani za kishirikina sana huwa kuna majani wanayaning'iniza juu ya milango yao ya biashara mara wanachoma mavitu flani fulani ila hili la kugeuza ndugu zao mandondocha ndio hatari.

Hawawageuzi ndugu zao mandondocha bali hii tabia yao ya kuozana binamu na binamu walio karibu ndio inayoletea kuzaa mataahira (inbreeding).
 
Si unamuona Manji alivyonyooka Manji alikua na dharau mpaka kinyaa alikua anajiona yeye ndio Tanzania Duh ila kwa kweli Magufuli kamnyoosha Manji,

Dewji katumbuliwa kwenye ulanguzi wa korosho wakulima walikua wananyonywa mpaka ukurutu ila msimu uliopita korosho imetajirisha watu hatari bado sasa kwenye viwanda na mashamba ya mkonge aliyonunua bila ya kuyaendeleleza ama kweli kanjubhai number wanaisoma
Kwani Dewji ni mhindi au mbohora?
 
Nashauri haya maneno ya kibaguzi (nani afukuzwe nchini na nani abaki) tuyaache. Athari ya ubaguzi ni kubwa sana. Mwalimu Nyerere alikwisha tuonya kuwa (I paraphrase) "dhambi ya ubaguzi haijamuacha mtu salama".

Wahindi wanatoka kwenye mila na desturi za kibaguzi (caste system). Na kule India kadri ngozi yako inavyokuwa nyeupe ndivyo unavyopanda ngazi katika caste system yao.
Wahindi walipoletwa Afrika mashariki na wakoloni, mambo mawili yalitokea. Kwanza waliungana pamoja kama wageni kati ya wenyeji weusi. Kilichofuatia ilikuwa ni kufuata utashi wao wa caste system na kuwaona weusi wote ni duni. Wao walikuwa wanamsikiliza mkoloni wa kizungu na kuwatuma waafrika. Mpaka leo hii ni nadra sana kukuta mhindi kutoka familia iliokaribu kuoa au kuolewa na "low caste" mweusi.

Nitaendelea..........

Baada ya uhuru wahindi walibaki na nafasi yao ileile ya katikati. Yaani mkoloni chini, mweusi juu (kama mtawala), na mhindi katikati. Lakini wakati wote huu wahindi walijiweka katika makundi yao kama wageni ingawa wengi wao wamezaliwa hapa hapa.

Kupitia sehemu zao za ibada waliendesha banking au financing system bubu. Kijana mgeni au anaeinukia kama anataka kuanzisha biashara alipewa ushauri na hili kundi (kama chamber of commerce bubu) na kupatiwa mtaji (mkopo) na hili kundi. Walimchaji riba mkopo huu kama benki za kawaida na akishindwa kufanya biashara alifilisiwa.

Lakini wale waliopata financing na ushauri kutoka hili kundi lao walikuwa watiifu sana kutimiza masharti kwa sababu kama akiwarusha basi sio tu itafilisiwa biashara bali anatengwa kundini. Ni huu woga wa kutengwa uliowafanya hawa wakopeshwaji kufanya bidii kubwa sana walipe lile deni na kushamiri peke yao katika biashara.

Kitu kingine wanachokifanya wahindi ni kuhakikisha vijana wao wote wanapata mafunzo ya ujasiriamali. Hata kama mtoto atakwenda kusomea udaktari, uinjinia, au sheria, lakini tangu akiwa mdogo atapelekwa kwenye masomo ya jioni ya bookkeeping, accounting, banking, taxation, financial systems, portfolio analysis, n.k. Hivyo basi hata akiwa daktari, ni rahisi kwake kutafuta mkopo na kuanzisha hospitali yake mwenyewe, kama anataka. Au hata kama yeye ni muajiriwa wa kawaida ni rahisi kwake kuona fursa za kibiashara (kupitia mtandao wao wa wahindi au yeye binafsi) na kujua cha kufanya ili azifanyie kazi hizo fursa.

Kukwepa kodi na kuhonga ni sehemu mojawapo ya mbinu za kufanya biashara. Hii sio kwa wahindi tu.

Itaendelea.........

Tunaweza kujifunza mengi kutoka kwenye hizi jamii za kihindi. Tusichukue ubaguzi wao (caste system) huu hauna tija nasi.

Tunaweza kuhakikisha kuwa vijana wetu wanapata elimu ya ujasiriamali toka elimu ya msingi hadi chuo kikuu badala ya kusubiri mpaka mtu anamaliza shule au chuo na kukosa ajira ndio aanze kufikiria mbinu za ujasiriamali.

Vitu viwili vinatuangusha sisi waafrika katika biashara navyo ni 1.) Mtaji au financing na 2.)Uaminifu.

Mtaji
Mara nyingi kijana aliemaliza shule anakosa sifa za kupata mkopo (collateral, credit) kutoka benki hata kama ana mchakato mzuri wa hiyo biashara (business plan) anayotaka kuianzisha. Tofauti na wenzetu wahindi wanavyokopeshana misikitini kwa kuaminiana tu.

Uaminifu
Waafrika ni kundi moja ambalo watu hawaaminiani sana. Si rahisi kuona mfanyabiashara wa kiafrika kwenda kumpa mtaji kijana aliemaliza shule tu (labda kama ni ndugu wa karibu au mtoto wa rafiki wa karibu) kwa hofu ya kurushwa. Kwa hiyo njia pekee za kupata mtaji ni kukopa benki (ambayo ni ngumu sana) au kukwapua hela serikalini na kuanza biashara.

Kwa mwendo huu utakuta vijana wengi wa kitanzania wanashindwa kuanzisha biashara wakati mwenzie wa kihindi waliomaliza pamoja shule anaanza biashara kiulaini sana.

Labda uzi huu utatupa mikakati ya sisi weusi kupanda juu kibiashara.

KUWAFUKUZA WAHINDI SIO JAWABU.
 
Wahindi wazee wakutakatisha pesa,wanaweka viduka duka uchwra ili viwe kwenye system halaf wanakua na account za biashara hyo hata 5,so wanacheza dili wanazozijua wao hela ikipatkana wanaizungusha kwenye biashara zao,so inaonekana kama viduka ndo vinaingiza pesa,wahind wanauza madini bila kulpa kod,wanauza unga,wanauza mazao,etc usione kiduka kinauza matoy au pen ,vile ni vya kuzugia tu
 
Wadosi bwana unaweza kuta dukani anauza sijui peni za bic,rula,sijui udi na marashi kumbe chaka ana vitu kama 20 vya ngada..unafkiri atakuwa na tatizo gani?ni nwendo wa bata kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom