Baadhi ya Viongozi waliokufa vifo tata

Baadhi ya Viongozi waliokufa vifo tata

1. Dr. Omary Ali Juma
Huyu alikuwa ni Makamu wa Rais katika Serikali ya Rais Benjamin Mkapa. Alienda kufungua maonyeshi ya sabasaba akiwa na Rais Kabila wa Kongo, kesho yake tukapata tanzia.

2. Benjamin Mkapa
Rais wa awamu ya tatu, jioni moja ya mwezi july mwaka 2020 ikiwa imebaki miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 tulitangaziwa kifo chake cha kushtusha. Maswali yakawa mengi

3. Edward Sokoine
Waziri Mkuu mzalendo pengine kuwahi kutokea. Alifariki katika ajali ya gari huko Dumila. Mpaka leo watu wanajiuliza gari ya Dumisan Dube iliwezaje kuifikia gari ya Sokoine?

4. Horace Kolimba
Alikuwa ni katibu mkuu wa ccm, akateleza kwakusema ccm imepoteza dira. Akaitwa Kizota Dodoma kujieleza mbele ya CC ya CCM baada ya kumalizia kuongea akadondoka na kufariki dunia.

5. Mchungaji Christopher Mtikila
Mwenyekiti wa chama cha DP, zikiwa zimebaki siki chache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 alipata ajali huku mkanda wake ukikutwa shingoni mwake.

Itaendeleaaaa....
Ongeza na Jiwe
 
Mchungaji Christopher Mtikila inasemekana PK anahusika.
Siyo kweli hata kidogo.
Hiyo ilikuwa ni Spinning Conspiracy Propaganda.
Ukweli ni kwamba Harakati zake za kupigania HAKI ndio zimesababisha kifo chake.

Kuna gharama kubwa sana za kulipa katika Harakati za kudai na kupigania HAKI.

RIP Mchungaji Dkt. Christopher Mtikila.
RIP Dkt. Sengondo Mvungi.
RIP Prof. Juan Mwaikusa.
RIP Stan Katabaro.
RIP Prof. Chachage.
RIP Dkt/Prof. Luviga.
 
Lissu ilibaki nukta apitishwe hivi. Ben saane, japo hakuwa wa sirikali ya ccm lakini duniani hayupo na mbinguni hajaoneka. Azory gwanda hakuwa kiongozi lakini hajulikani alipo mpaka kesho. JIWE LINAUNGUZWA SANA SAA HII.
Sasa Duniani Hayupo Na Mbinguni Hajaonekana Yupo Wapi
Wewe Ndio Malaika
 
Kumbe hata John Kennedy Rais wa Marekani alijiuwawa eti .... KARUME, Gandhi, si ndio unachokisema hapa...ficha ujinga huo ...vipo vifo vya kuamini matendo ya Mungu na vipo vifo binadamu wanawatanguliza wenzao...Lumumba!!
Kennedy alipigwa risasi live on TV
 
Back
Top Bottom