Baadhi ya misemo ya makapuku wenzangu

Baadhi ya misemo ya makapuku wenzangu

ELI COHEN

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
9,376
Reaction score
28,497
"aah wapi, hayo mapiza na mabaga wanayokula na mimi ninae kula matembele vyote vitaishia kuwa mavi tumboni"

"usione mtu amekuwa tajiri kiasi hicho wewe, watu wanalala na nyoka kitandani, wewe unaweza?"

"usione dar hii watu wengi hali ngumu, lile sanamu la askari pale posta ndilo linalonyonya nyota za watu na kuchukuliwa na freemason, lile bunduki linalenga nyota za watu ukikaa samba samba nayo"

"siku hizi anajikuta mataaawiii, gari lenyewe la mkopo hilo, roho juju juu kila mara anawaza marejesho"
 
Pesa kitu gani cha muhimu uhai tu, kwani utazikwa na hizo pesa 😁
😁 Alafu akisogea pembeni anaanza kukwambia "blooo ebu nitoe basi buku mbili hapo, nitakuridishia jioni"
 
Back
Top Bottom