DOKEZO Baadhi ya Maafisa wa Manispaa Morogoro wanatukamata Bajaj kisha wanataka faini laki 1 au uwatoe 50,000

DOKEZO Baadhi ya Maafisa wa Manispaa Morogoro wanatukamata Bajaj kisha wanataka faini laki 1 au uwatoe 50,000

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Maafisa wa Manispaa Morogoro wanatukamata Bajaj kisha wanataka faini laki moja au utoe Rushwa 50,000

Sisi madereva na wamiliki wa Bajaj Morogoro tumechoshwa na usumbufu wa makundi ya watu wa manispaa. Wanakamata Bajaj bila mipangilio wakidai kuna makosa mbalimbali na faini inaanzia shilingi laki Moja, au uwatoe shilingi 50,000 ili mmalizane, chini ya hapo hawakubali.

Ukiomba control number ya faini waliojiwekea ambayo ni laki Moja hawana, wanaishia kukupa vitisho tu, tunateseka sana.
 
Back
Top Bottom