Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Baada ya klabu ya Yanga Sc kuangukia pua kwenye kesi yake dhidi ya Shirikisho la soka Tanzania TFF, Bodi ya Ligi na klabu ya Simba Sc, Mkuu wa Kitengo cha Sheria klabuni hapo, Simon Patrick ametangaza kuachia ngazi kama Mwanasheria wa Mabingwa hao wa kombe la Muungano 2025.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Adv Simon Patrick ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Mawakili Tanzania (Tanganyika Law Society) pamoja na Chama cha Mawakili cha Afrika ya Mashariki (East African Law Society) amebainisha kuwa sasa anasalia kuwa mwanachama mtiifu wa Yanga kuomba aruhusiwe aendelee kupumzika kwenye soka la Bongo.
"Vita dhidi ya wahuni haijawahi kuwa rahisi. Wanayanga wenzangu, najua maamuzi madogo ya CAS yamewaumiza, ila tuwapongeze viongozi wetu kwa kupinga uhuni kwa vitendo na nina uhakika hawajakata tamaa." Simon Patrick amesema
"Najua hawawezi kujitokeza kuwaeleza wanayoyapitia nyuma ya pazia, ila ipo siku mtawaelewa. Niwaombe wana Yanga muendelea kuwapa moyo na kuwaunga mkono kwa nguvu. Kwa muda niliotumikia klabu, nimejionea jinsi ilivyo changamoto kuiongoza klabu ya Yanga."
"Mwisho, nitumie fursa hii kuwaomba radhi ndugu zangu waandishi wa habari. Nimekuwa sipokei simu zenu, si kwamba sipendi kuzungumza nanyi, bali kwa sasa mimi ni mwanachama mtiifu wa Yanga, Nawaombeni mniruhusu niendelee kupumzika soka la Bongo, Yanga ina watu makini wengi na wenye weredi tuwape muda waendelee kutupambania" amesema Simon Patrick