Baada ya ripoti ya Makinika kutikisa, Executive Chairman wa Barrick atua Tanzania kutuliza mambo

Ni TZ tu wezi wanakaribishwa mezani kwa mazungumzo. Tutaibiwa sana kama huo utaratibu wa kukaa na wezi mezani hautakoma.
Sasa wewe ulitakaje? Tuwafukuze? Je kama wanaweza kutulipa walichotuibia kwanini tusikae nao kwenda nao sawa
 
mi namuunga mkono lákin pia nawashangaa wabunge wa C.C.M nao wanamuunga mkono!!!!wakati wao ndo waliopitisha Sera na sheria za madini kwa kura ya NDIOOOOO

Pale Kafulila aliposema kuna haja ya kupitia upya sheria hizoo,wabunge wa C.C.M walizomea!
Sipendi na ninamchukia sana mtu anayetaja CHADEMA au CCM kwenye hili jambo.Sijui kuna vichwa gani humu ndani siku hizi
 
Wenzetu wako vizuri sana kiuwajibikaji wanaangalia wasijichafue utakuta uchafu wote unafanywa na wa chini wa juu hawajui,hela wanazo cha msingi walipe tu uenda tukaacha kula maramoja kwa siku. JPM kaba koo walipe tu hela yetu, mikataba ifanywe upya.ikibidi tukachukue wa Botswana nusunusu madini hayazai, pia ingia kwenye almas na tanzanite,mafuta na gas,tumechoka kupiga pasi ndefu.
 
Sipendi na ninamchukia sana mtu anayetaja CHADEMA au CCM kwenye hili jambo.Sijui kuna vichwa gani humu ndani siku hizi

sema hupendi kujua chanzo cha nchi yetu kufika hapa!!!!
huwezi ukatatua tatizo bila kujua chanzo cha tatizo!kwenye huu mjadala ni ngumu C.C.M kutokutajwa!!!!
 
Sasa wewe ulitakaje? Tuwafukuze? Je kama wanaweza kutulipa walichotuibia kwanini tusikae nao kwenda nao sawa
Yaani unataka kuniambia hujui ni hatua gani mwizi anatakiwa achukuliwe? Kama tunataka kukaa nao mezani tufute kabisa hiyo kauli ya kuwa ni wezi. Labda tuseme walikuwa wanatupunja tu. Kwa vile tumekuwa wastaarabu sana wa kukaa nao mezani basi tutumie ustaarabu huohuo kutowaita wezi. Tuwaambie tu kwamba kuna pesa walisahau kutulipa kwa hiyo watulipe sasa.
 
View attachment 523207
Mkuu usatrumpjr
Mimi huwa sina tabia ya kuleta udaku au majungu,ukiona nimeandika jambo hapa,ujue nina uhakika

Kwa taarifa yako tu,Mr.Thornton naambiwa kaingia Dsm usiku,akiwa na ndege mali binafsi ya Barrick Gold Corporation.Ndege hiyo aina ya GulfStream IV yenye usajili wa Canada wa C-FHPM imembeba yeye peke yake toka huku mpaka huko.Jambo la Makinikia si dogo hata kidogo.

Tazama ndege hiyo kwenye "Flight Radar" utaona kwa mara ya mwisho inaonekana ipo Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kuanzia jana majira ya 2300hrs kwa saa za Afrika Mashariki.
Mkuu barafu nimekukubali
 
Wakuu nawasalimu

Juzi niliandika uzi huu Vita dhidi ya mabepari wa madini inahitaji umoja, ilimshinda Dr Williamson wa Mwadui na Mwl Nyerere nikiwa Toronto Canada,hapo nilikuwa nyumbani kwa Mzee mmoja aliyeishi Mwadui miaka ya 1970's kabla ya kuondoka na kurudi huku.

Alinipa habari nyingi sana za "fitna" za mabepari wa madini katika dunia hii.Tunapaswa kuungana katika vita hivi,tusimuache Rais peke yake,na wala Rais asiibebe vita hii peke yake.

Leo ninapata ujumbe kuwa "Executive Chairman" wa Barrick Gold Corporation Mr.Thornton John Lawson ametua Tanzania usiku kwa usiku ili kuja kutuliza mambo.Hali ya hapa Canada kwa Barrick sio nzuri,wanaharakati na wanasiasa wameanza kuandaa hoja za kuishutumu Barrick(Acacia) kwa "hujuma" walizoifanyia Tanzania toka mwaka 1998.

Kiukweli sakata hili la Tanzania na Accacia sio dogo tena,ni mgogoro mkubwa sana katika ulimwengu wa biashara na mashauriano ya kigeni.Kama nilivyosema juzi katika uzi ule,hii ni vita,ni vita kati ya Rais yeye binafsi na hawa mabepari wa madini,na ni vita kati ya Tanzania kama nchi na makampuni haya.TUSHIKAMANE.

Hata Rais jana alisema,yeye naye ni binadamu,ana damu na nyama,anajua kuwa anapigana na watu wenye nguvu za kiuchumi duniani,tumuombee na tumpe ushirikiano.

Safari ya Mr.Thornton kuja Tanzania ina maana kubwa sana katika kufikia mwisho wa "mgogoro" huu kati ya sisi kama Taifa na kampuni ya Barrick.Ripoti ya pili ya kamati ya Rais iliishitua sana management ya kampuni ya Accacia na kuamuru Executive Chairman apande ndege na kuja Tanzania kuweka mambo sawa.Hisa za Barrick katika masoko ya hisa makubwa duniani kama LSE,NYSE,Australia nk yameshuka kwa kiwango kikubwa sana.Tahadhari inahitajika mapema kwa kumuona Rais na kuweka mambo sawa.

Wakati tukiendelea kujua huko nyumbani,ni nini haswa Mr.Thornton ataongea au hata kupewa nafasi ya kumuona Rais,basi tujue huyu Mr.Thornton J. Lawson ni nani hasa??

Mr. Thornton was appointed Chairman of Barrick on April 30, 2014. From June 5, 2012 to April 29, 2014, Mr. Thornton was Co-Chairman of Barrick. He is also Non-Executive Chairman of PineBridge Investments, a global asset manager.

He is also a Professor, Director of the Global Leadership Program, and Member of the Advisory Board at the Tsinghua University School of Economics and Management in Beijing.

He is also Co-Chairman of the Board of Trustees of the Brookings Institution in Washington, D.C. He retired in 2003 as President and a member of the board of the Goldman Sachs Group.


Huyu ndio Chief Chairman wa Barrick Gold Corporation,mtikisiko wa ripoti ya Rais toka Ikulu ya Magogoni,umetikisa mpaka ardhi na viunga vya London,New York,Toronto na Paris.Tungoje na tusubiri.
Safi sana. U seem to understand what you write. [HASHTAG]#TanzaniaKwanza[/HASHTAG].
 
Lisu kalewa vijisenti alivyohongwa
Magufuli kasomeshwa somo Barrick hawawezi kukubali Tanzania ichafue jina lao ndio maana wameshuka na ukweli makanikia yatendelea kwenda na dhahabu itachimbwa Zaidi kafyatishwa unatamba wakati serikali uliyokuwemo ndio imepelekea mzigo kwa wananchi ccm na magufuli ni mumiani sasa anakimbia eti Mkapa na Kikwete hawamo kwenye ripoti hiyo ni akili kweli au kuchanganyikiwa
 
Magufuli kasomeshwa somo Barrick hawawezi kukubali Tanzania ichafue jina lao ndio maana wameshuka na ukweli makanikia yatendelea kwenda na dhahabu itachimbwa Zaidi kafyatishwa unatamba wakati serikali uliyokuwemo ndio imepelekea mzigo kwa wananchi ccm na magufuli ni mumiani sasa anakimbia eti Mkapa na Kikwete hawamo kwenye ripoti hiyo ni akili kweli au kuchanganyikiwa
Sasa hapa sijui Mkapa na JK anawachomoaje?
 
Back
Top Bottom