Baada ya ripoti ya Makinika kutikisa, Executive Chairman wa Barrick atua Tanzania kutuliza mambo

Naona alishawahi kua president of Goldman Sachs Group sio wa mchezo mchezo huyo mzee
 
Exactly umefikiria Vizuri sana nahisi hata Mtu wa Kwanza Kukutana naye Airport ni Tundu Lissu!
Nachukia kwa kweli hili suala anaponyooshewa kidole Lisu ,niko pamoha na rais kwa hatua ya sasa sio kwa waliyoyafanya yeye na chama chake kwa hiyo Lisu na wenzake wanahakibya kupiga kelele !Vile vile Lisu hakuna hata sehemu moja alijiunga na acacia au barrick bali alikuwa katika kuonya nini kinaweza kutokea kama hatutofanya mihemko ndi mihemko kwani tumeshapona IPTL na Samaki?
Kilichopo kwenye repirt ya pili serikali akiwemo rais hawakukijua baada ya report walikijua miaka yote kwa hiyo majority ya wapongezi ni waongo na wanafiki wakubwa kwani wengi wao walipiga viti na meza bungeni kushangilia kupitishwa sheria na hatimaye kusainiwa mikataba ya ovyo kabisa!
Niseme tu CCM ione haya kumpongeza Rais wetu,na pia Rais asiwe na ujasiri wa kuwasimanga wapinzani kwenye sakata hili!
 
Aje tuu na pia nikupongeze kabla hujatumia Sigara yako ama Kinywaji chako Unakua na Mawazo Mazuri Sana Big up!

Edit Heading weka "" Apokelewa na Mwenyeji wake Tundu Lissu'''
Nyie ndo mnakosea kwa kuwatenga weledi kama akina tundu lisu katika vita muhimu kama hizi. Raisi alitakiwa awaite weledi kama hao akae nao meza moja kuona namna ya kushinda pamoja hii ni mama Tanzania tutakufa na kuwaachia watoto wakitusoma kama sie tunavyowasoma akina chifu mangungo. Hebu punguza ubinafsi
 
kwani wakihusika ndio nini...kuna public interest yoyote kwa mawaziri wakuu kutokushtakiwa...?

Du siasa ni kazi...

..na wapinzani wakikubaliana na hoja ya Ndugai watakuwa wapumbavu kwelikweli.

..kinga ya Raisi kushtakiwa haimlindi Waziri Mkuu.
 
Huu ulikuwa ni usiku?

d6.jpg


Baadaye...

3571707_orig.jpeg
mkuu ina maana we huoni kama huo ni usiku??!!
 
Watu mmehama toka kwenye mantiki ya uzi huu na kuanza mambo ya siasa. Non sense. Hapa masuala ya Tundu Lissu yaingiaje. Ndugu yangu barafu pole hapa kuna baadhi ya wapuuzi wanaharibu maana ya uzi wako.
Tulitakiwa tujadili na kutahadhalisha juu ya huyu mtu CEO wa ACACIA na kuona ni jinsi gani tufanye kukabili hujuma zake au zao. Natamani Rais angemgomea kwanza na angesitisha uzalishaji na usafishaji wa dhahabu hadi watupe chetu kama alivyosema jana. Madini hayaozi hayana expiry date. Huyu CEO mtakao kutana naye mpe kavu mwizi mkubwa
 
Kumbe..mzalendo..alijua jamaa yupo njianii
ndiomaana akakazia swala la kukaa kitako Mezaniii..!!!
Mwizii karibu..nchinii..tukutane mezanii
Ataweza kutema yai? Au ndo ya mambo ya yes, yes, yes, yes!!
 
UFAFANUZI MUHIMU KUHUSU USAJILI WA ACCACIA.
Ni,
Waraka wa BASHIR YAKUB

Kwa kutumia kigezo cha usajili, Tanzania tunazo aina kuu mbili za kampuni. Kampuni za ndani(Local companies) na kampuni za kigeni ( foreign companies).

Kampuni za ndani ni zile zote zilizoanzishwa hapa nchini na kusajiliwa hapa nchini. Hata kama wanahisa wake wote ni raia wa kigeni kwasababu tu ya kuanzishwa hapa na kusajiliwa hapa zinakuwa ni kampuni za ndani.

Kampuni ya kigeni ni ile iliyoanzishwa na kusajiliwa nje ya Tanzania lakini ikaanzisha ofisi/biashara/tawi hapa Tanzania. Sheria Na. 12 Sheria ya Makampuni kifungu cha 433 kinasema hivyo. Kampuni kama imeanzishwa nje hata kama wanahisa wake wote ni Watanzania, hapa kwetu hiyo bado ni kampuni ya kigeni.

Kampuni ya ndani inaposajiliwa hupatiwa cheti cha usajili kiitwacho "Certificate of Incorporation" kwa mujibu wa kifungu cha 15(2) Sheria ya Makampuni. Kampuni ya ndani inapopata cheti hiki basi usajili wake huwa umekamilika na inatambulik a rasmi kama kampuni ya ndani.

Kampuni ya kigeni inaposajiliwa hapa Tanzania hupatiwa cheti kiitwacho "Certificate of Compliance" kwa mujibu wa kifungu cha 435(1) Sheria ya Makampuni. Kampuni ya kigeni inapopata cheti hiki basi usajili wake huwa umekamilika na hutambulika rasmi kama kampuni ya kigeni.

Acacia ni kampuni ya kigeni. Kwa maana kuwa ilianzishwa nje ya Tanzania na kufungua shughuli zake hapa nchini. Kwa hiyo ili ihesabike imesajiliwa Tanzania ilitakiwa kuwa na cheti kiitwacho"Certificate of Compliance". Kutokuwa na cheti hiki maana yake ni kuwa haijasajiliwa Tanzania na haitambuliki.

Nimesikia mjadala BBC SWAHILI leo wanaojadili wakijiuliza inawezekanaje kampuni kubwa kama hii ikafanya biashara bila usajili. Watanzania wengi pia wanajiuliza swali hili.

Jibu lake ni hili. Acacia ni kampuni tanzu(Subsidiary Company) ya Barrick. Kampuni inakuwa tanzu pale ambapo zaidi ya nusu ya hisa zake zinamilikiwa na kampuni nyingine. Ile inayomiliki huitwa "holding company" na inayomilikiwa huitwa "subsidiary company". Kwahiyo Barick ni " holding" wakati Acacia ni "subsidiary".

Barrick inamiliki hisa za Acacia 63.9%. Kwa kusema hivi maana yake Barrick ndiye mwenye Acacia. Hata hivyo kwa mujibu wa sheria hizi zinahesabika kampuni mbili tofauti na kila moja inabeba wajibu na hatia zake yenyewe(its own responsibility& liability).

Basi kumbe kilichotokea ni kuwa Acacia walikuwa wakifanya biashara kwa jina la Acacia lakini wakibebwa na mgongo wa Barrick. Walijificha hapa na wakaweza kuishi bila usajili wa kwao kama wao. Walijibeba kwenye usajili wa Barrick.

Barrick wao wanao usajili na wanayo " Certificate of Compliance" ya kwao ambayo tayari wameitoa hadharani. Kwakuwa haya ni makampuni mawili tofauti kila moja inatakiwa kuwa na cheti chake kwa mujibu wa kifungu cha 487 Sheria ya Makampuni na kutokufanya hivyo ni kosa kabisa. Kwa hiyo hivi ndivyo ilivyowezekana kampuni hii kufanya biashara bila usajili miaka hii yote.

Adhabu ya kosa kama hilo ni kifungo jela. Sheria Na. 12 Sheria ya Makampuni iliyofanyiwa Marekebisho mwaka 2002, kifungu cha 472 kinasema hivyo.
 
Nilijua angekuja wa kutoka Acacia....???
Ni hapo sasa?
Itakuwa kama hivi Magufuli:wewe umetoka wapi??
Mwenyekiti:mie nimetoka barroik gold ya canada kuja kumaliza mgogoro wenu na ACACIA PLC.
Magufuli:Mbona nchini kwangu sina kampuni iliosajiliwa kwa jina ACACIA MINING PLC?
Hawa wameingia choo cha kike kwa wizi wao walipe kwanza Trilioni 55 kwanza
 
mi namuunga mkono lákin pia nawashangaa wabunge wa C.C.M nao wanamuunga mkono!!!!wakati wao ndo waliopitisha Sera na sheria za madini kwa kura ya NDIOOOOO

Pale Kafulila aliposema kuna haja ya kupitia upya sheria hizoo,wabunge wa C.C.M walizomea!
Tushikamane jamani. CCM wamekosea sawa. Ebu tuwekeni hasira pembeni kwanza. Tumalize hili likiisha turudi kwenye vyama vyetu
 
Wiki ya pili hii Lumumba mnajadili Tundu Lisu mpaka Rais wenu amemtaja utafikiri yeye ndio anayesaini mikataba.

Hakika Tundu Lisu anawahumiza sana vichwa wengine, na nyie somesheni mitoto yenu ijue sheria.
Hata rais wetu? We si rais wako? Halafu mbona hakumtaja Lissu. Lissu ni wa kawaida sana
 
Huyu jamaa asipewe nafasi ya kuingia ikulu... Ikulu hakuingii wezi... Kama amekuja kuonana na rais wa WCB akaonane nae kwenye ofisi yake huko tandale na siyo rais wa Jamhuri ya watu wa Tanzania...
 
unaposema alishirikiana na wachache kutuibia una maana gani?wakati wabunge wengi wa ccm ndio waliipitisha hii mikataba kwa ndiooo!!!!!!!! ?
Nyie watu mnataka muambiwe vipi. Rais mwenyewe anajua bunge lilichemsha ndiyo maana kaagiza mikataba irudishwe ijadiliwe upya
 
The global ethic of business conduct has shifted in the west, pressure groups and consumers demand fair trades.

Unajua tu kuna watu wakisikia jinsi gani kampuni fulani inainyonya nchi maskini watakuja juu, sasa aina maana na wewe mnyonge utunge story kiasi kwamba wajiulize inawezekana kweli.

Mwisho wa siku unaomba timu itakayoenda kukaa mezani kujadili aina mtu anaeitwa Mruma wala Orero (or something), just unrealistic people.
 
Back
Top Bottom