Pakome
JF-Expert Member
- Dec 8, 2024
- 1,541
- 916
Mimi kwa muda mrefu nimekuwa nikifanya kazi za matajiri wengi sana ikafikia mahali Matajiri wale wakawa wananialika kwenye shuhuli zao
Sasa kawaida binadamu kuna wakati tunazungumza mambo mengi
Siku moja nikachomeka swala la Ibada
Nikawauliza kuwa kuna shutuma kuhusiana na matajiri kuwa hawaendi nyumba za Ibada nikama wavivu hivi
Wakanijibu kuwa wanapenda sana na wanatamani sana kuhudhuria nyumba za Ibada lakini tatizo ni moja tu
Wakadai kuwa tatizo hilo linatokana na mafundisho mengi kujaa umbea badala ya mafundisho yakusaidia binadamu kwa maisha haya halisi
Nikawauliza umbea upi huo? Wakanambia idadi kubwa ya viongozi wa dini hawana habari nyingine za kuelezea Waumini zaidi ya umbea wa Shetani wa mamilioni ya miaka iliyopita, umbea ambao ulishatupwa kwenye dampo na maisha mengine yakaendelea, kwamba alifanya haya akafanya yale mara akagombana na Malaika
Wakanambia habari hizo kwao ni umbea wa kijinga ambao ulishatupwa kwenye dampo mabilioni ya miaka iliyopita na wala Shetani haukumbuki tena ni sisi binadamu wajinga na tunaopenda umbea na chokochoko ndio tunahangaika na mambo ya kipuuzi ya kimbea mbea kama wajinga wasiokuwa na akili
Wakanambia wanachotaka kusikia viongozi wakifundisha watu ni namna ya kutafuta maisha na kutoa mbinu za kukabiliana na maisha haya halisi
Mfano wanataka viongozi wawafundishe mambo tunayoyaishi mfano Kilimo, kwamba mvua ya mwaka huu ni ya kiwango gani ili wapande mazao ambayo mwisho wake yatawapa chakula
Wakanambia wanataka kusikia viongozi wakifundisha maswala ya Uchumi kwamba ni biashara zipi watu wakifanya kwa hali ya sasa watapata faida nzuri
Wakanambia wanataka kusikia ni mifugo ipi yenye faida nzuri ili hata kama watafuga wapate fedha za kuendesha maisha yao na familia zao
Wakanambia wakifahamu nyumba ya Ibada inayotoa mafunzo ya maisha haya halisi tunayoishi basi watafurika kwasababu wanachotaka kufundishwa ni reality na sio kujazwa mafundisho ya kimbea mbea ambayo hayawezi kuwapa chakula wala ada za kulipa shuleni
Wakanambia habari za Shetani alifanya hivi mara akafanya vile kwao ni upumbavu na habari za kimbea mbea kwasababu haziwezi kuwasaidia wanachotaka nikusikia viongozi wanaowafunulia biashara nzuri za kufanya, mbinu za kuwekeza na mambo ya kubadilisha maisha yao
Wakanambia hizo habari hata huyo Shetani mwenyewe anaziona takataka kwasababu zilishatupwa mabilioni ya miaka iliyopita na kwanza alishasahau ni sisi binadamu wajinga tunahangaika nazo badala ya kuhangaika na mambo yatakayotusaidia kwenye maisha haya halisi kama kilimo, ufugaji, biashara, uwekezaji, na mambo kede kede
Wakanambia kama hakuna mafundisho hayo hawana muda wa kwenda kusikiliza takataka
Wakanambia kama ni kuhusu Mafundisho ya vitabu vya dini hawana tatizo nayo kwasababu yanaongelea mambo mazuri mfano upendo amani, huruma, msamaha lakini haya ya migogoro huwa hawapendi kwasababu hata kwenye vitabu vya dini hayajaandikwa sana