Baada ya kutangazwa kifo cha J.K. Nyerere mwaka 1999, ulifanya nini (first reaction)?

Mimi nilivyosikia tu nikakimbia toka shule kurudi nyumbani na cha kwanza kupanga nguo zangu kwenye mfuko wa kwechekweche na kuamini kuwa ndio mwisho wa tanzania na mzee ataondoka na nchi yake soon so nikawa nasikilizia inze kuondoka tu nikimbie kusikojulikana.
Utoto bhna yaani sijui hata nilikuwa na mawazo ya namna gani
mkuu Wa nyamadyaki na Honey Faith kwa hiyo ilikuwa hata ukisikia mtu karusha jiwe juu ya bati unahisi kama ndio hao wamefika tayari.....teh teh teh teh teh teh teh
 
Just kidding. Nilikuwa chuo mwaka wa kwanza na kulikuwa na masomo magumu mno ambayo yalikuwa yakitishia sana amani yetu. Hapakuwa na nafasi ya kustarehe wala ku-miss starehe. Kifupi mwaka huo colleagues wengi walikimbia shule baada ya kuona hali ni mbaya. Ndiyo maana nikaita hali hiyo "terrorism" maana kiuhalisia, we lived in "terror" those days.
poa poa kaka
 
weird? why?
Quite frankly naichukia sanaa ccm,na yeye nyerere kama mwanzilishi wa hicho chama,look at the misery and sufferings of the Tanzanian people incurred under the rule of this party.it was Nyerere's ideologies that brought the economy to the total shambles,the poverty,lack of education,lack of infrastructure,no water and sanitation and the list goes on.so I.put a blame on this individual
 
Quite frankly naichukia sanaa ccm,na yeye nyerere kama mwanzilishi wa hicho chama,look at the misery and sufferings of the Tanzanian people incurred under the rule of this party.it was Nyerere's ideologies that brought the economy to the total shambles,the poverty,lack of education,lack of infrastructure,no water and sanitation and the list goes on.so I.put a blame on this individual
upo sahihi sana
 
Kifo cha Nyerere kilileta na kukata disco mwezi mzima
na TV zilikuwa hazitangazi chochote kingine zaidi ya msiba
kifo cha Nyerere kinamna fulani ndo 'kilianzisha' bongo fleva

watu waliboreka mno na nyimbo za huzzuni ikawa ruhusa kwa kila msaniikutunga nyimbo yake kwenda kwenye tv na redio

ndo kina Jaydee wakaibukia pia...na wengine....

kabla ya hapo hakukuwa na nguvu sana kwa mziki wa bongo fleva...

binafsi walinifurahisha Club Bilicanas.....wao walijifanya kuna 'Tamasha la kumkumbuka baba wa Taifa'
hapo ikawa fursa ya watu kula debe siku hiyo baada ya kukosa burudani karibu mwezi mzima....

mimi nilipata mateso ya kuikosa CNN kupitia CTN kwa mwezi mzima
am curious to know more abt u The Boss, yan wengine kipind icho tuko primary wewe unaangalia CNN kweli JF
 
ME NAKUMBUKA NILIKUWA NASOMA FORODHANI PRIMARY STD 7 TUKATANGAZIWA NYERERE AMEFARIKI BANA KUNA WANAFUNZ WENZETU WAKATUAMBIA MWILI WAKE UPO PALE IKULU WANAFUNZ TU NDIO WANARUHUSIWA KWENDA KUAGA WACHA TUCHAPE MIGUU TUKO LUNDO MPAKA IKULU ETI KUONA MWILI WA MAREHEMU:D:D:D TULITIMULIWAJE SASA NA MAASKARI SITASAHAU
 
Duh! Aisee.... Nilikuwa darasa la Sita Shule ya Msingi Wilolesi Iringa mjini.... Nakumbuka baada ya kutangwa tu nilirudi nyumbani Fasta sana na kipindi nikatafuta funguo ya chumbani kwa mzee funguo alikuwa amesepa nayo..... Nilichofanya ni kuchokonyoa kitasa hadi kikafunguka nikawasha TV nikawa nacheki walikuwa wanaonesha maombelezo tu.... Wakati naendelea kuangalia gafla aisee Kuna shangazi yangu mmoja naye akawa amerudi aisee nilikula bakora sana kwa nini nimeharibu kitasa chumbani kwa mzee na kuingia kuangalia TV!?.. Maana Nakumbuka tulipangiwa ratiba ya kuangalia Tv.. Na baada ya hapo TV inarudi chumbani kwa mzee.... Lakini sijui kwa nini Ile siku ni kama nilipagawa na sikujali chochote.... Ila kufika usiku aisee nikawa nawaza kweli badae nitasemaje kwa mzee!?... Ila Mungu Sio Mbowe bwana wala Tundu Lissu.... Kufika usiku baba na mama walikuwa wamekuja na mgeni nyumbani... Nakumbuka yule mgeni akikuwa anaitwa DR. Kapwani.... Aisee yule shangazi akaanza umbeya kwa mzee... Mzee alinisema Lakini yule mgeni... Alinitetea sana.... Na alimwambia mzee huyu mtoto anaakili na inabidi umpongeze kwa kufuatilia jambo kubwa kama Hilo ni kaonesha ni mfuatiliaji mzuri wa mambo...... Yule Dr. Nakumbuka alinipa Sh.Elfu Ishirini kama kunipa faraja ya kichapo cha mchana cha Shangazi yangu...... Kwa hiyo mkuu uliyeanzisha hii mada aisee Umenikumbusha Mbali sana kiukweli..... R. I. P. Baba wa Taifa Mwalimu Jk. Nyerere... Ni hayo tu.
 
Nilikuwa A level , MUDA WA SAA 4 TULIKUWA MAPUMZIKONI, TUKAWA TUNASISKILIZA REDIO , LIKATOLEWA TANGAZO RAIS ATAONGEA, KISHA WIMBO WA TAIFA, NDIPO RAIS ALIPOTANGAZA, TULISHTUSHWA SANA.
 
Naomba niongee ukweli kwenye hili binafsi sikushtuka kwakuwa nilishajua wiki moja kabla kwamba mzee mchonga hatunaye tena
Kweli mshana jr siku BBC walipomhoji makongoro akasema watanzania tujiandae na msiba, then kawawa akarudi toka uingereza magazeti yakaandika simba wa Vita arudi na kitu kizito moyoni, uwanja wa taifa ukaanza kupakwa rangi, na nyumba yake msasani ikafanyiwa ukarabati wa dharura, mtu yeyote mzima na Akili zako hujiulizi mara mbili mbili
 
Mimi nilivyosikia tu nikakimbia toka shule kurudi nyumbani na cha kwanza kupanga nguo zangu kwenye mfuko wa kwechekweche na kuamini kuwa ndio mwisho wa tanzania na mzee ataondoka na nchi yake soon so nikawa nasikilizia inze kuondoka tu nikimbie kusikojulikana.
Utoto bhna yaani sijui hata nilikuwa na mawazo ya namna gani
we jamaa umenifurahisha sana
 
Back
Top Bottom