Ni kweli Nyerere alikufa tarehe 14/10/1999 au tunafichwa uhalisia wa kifo chake?

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,264
5,403
Mwamba wa Afrika Mwalimu J.K Nyerere pumzika kwa amani huko aliko, umefanya makubwa katika hii nchi
wewe ndio kielelezo cha uzalendo, Pale Butiama familia yako inaishi maisha ya kawaida kabisa huwezi
kutofautisha familia yako kwa maisha wanayoishi na mkulima wa kawaida, RIP babu.

Swali la kujiuliza, ni kweli Nyerere alikufa tarehe 14 Oktoba 1999? kama ni kweli zile nyimbo za maombolezo za Kapteni Komba alizitunga na kuzirekodi kwa muda gani?, maana kumbukumbu zangu zinanionesha mara tu baada ya Rais wa wakati huo, Mzee Mkapa kutangaza kifo cha Nyerere, vituo vya habari vilianza kupiga nyimbo za Komba. Au walihisi hatapona hivyo wakaandaa nyimbo za maombolezo mapema?

Bado najiuliza ina maana tunaomboleza siku ya kifo cha Baba wa Taifa isiyo sahihi? Ni baadhi ya
vitu ninavyojiuliza na kukosa majibu na nikifahamu kuwa kwa Afrika haya yote yanawezekana lakini je kama ni kweli ni kwa manufaa gani?

Mawazo yenu wanajamvi.
 
Vifo vya watu wazito nadhan tunafichwaga sana hadi watakapo andaa mazingira wanayo ona ni sahihi kwao. Kama kifo cha Mandela sina iman ilikuwa ni siku ile wametangaza au cha ndugu Ruge. Hayo ni mawazo yangu tuu
 
Labda kapteni alijua jamaa amekaribia kufa, kwani kwenye zile nyimbo kuna sehemu wametaja tarehe?
 
Huwa wamekufa wiki moja kabla ya tangazo ili kujipa muda wa kujipanga na maandalizi ya msiba, ni kama tu misiba ya wakristo wa kawaida #Streets say
 
Back
Top Bottom