Kadi Poa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 2,015
- 1,004
Kifo cha Nyerere kilileta na kukata disco mwezi mzima
na TV zilikuwa hazitangazi chochote kingine zaidi ya msiba
kifo cha Nyerere kinamna fulani ndo 'kilianzisha' bongo fleva
watu waliboreka mno na nyimbo za huzzuni ikawa ruhusa kwa kila msaniikutunga nyimbo yake kwenda kwenye tv na redio
ndo kina Jaydee wakaibukia pia...na wengine....
kabla ya hapo hakukuwa na nguvu sana kwa mziki wa bongo fleva...
binafsi walinifurahisha Club Bilicanas.....wao walijifanya kuna 'Tamasha la kumkumbuka baba wa Taifa'
hapo ikawa fursa ya watu kula debe siku hiyo baada ya kukosa burudani karibu mwezi mzima....
mimi nilipata mateso ya kuikosa CNN kupitia CTN kwa mwezi mzima
The Boss nakumbuka kuna watu walikuwa wanasema nchi ndio itavamiwa baada ya mzee kufa, basi watoto wengi walikuwa wanaogopa muda wote wapo na mama zao....