Kuelekea 14 Oktoba: Kwanini Nyerere Day ni kumbukizi ya siku ya kifo cha muasisi, shujaa na mzalendo wa taifa letu na sio kuzaliwa kwake (Aprili13)?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania kuelekea 14 October.

Kwanini Nyerere day ni kumbukizi ya siku ya kifo cha muasisi, shujaa na mzalendo wa taifa letu na sio kuzaliwa kwake (April 13)?

asasddddddgtgt.jpg


What's the logic behind? Ina maana kifo ni muhimu sana kuliko birthday?

Kwanini Nyerere Day sio April 13 ya kila mwaka kuanzia April 2000 mwaka mmoja baada ya kifo cha huyu baba yetu? Au;

Kwanini Karume day nayo pia ni siku ya kifo April 7 na sio siku ya kuzaliwa August 4?

OMBI LANGU: Ninaomba tuwe na sanamu ya Rais (Statue/Monument) katika makao makuu ya kila wilaya atokayo Rais husika.

images (25).jpg


(1) Wilaya ya Butiama - Mwalimu J.K Nyerere (Nadhani ipo ingawa sina uhakika).

(2) Wilayani huko Pemba - Mzee A.H Mwinyi

(3) Wilaya ya Masasi - Mzee B.W Mkapa

(4) Wilaya ya Bagamoyo - Mzee J.M Kikwete.

(5) Wilaya ya Chato - Mzee J.P Magufuli

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Kumbukumbu ya kifo chake naona imekaa vizuri zaidi kuliko ya kuzaliwa kwake. Kwani inatufanya tukumbuke yale mema ya wakati wa uhai na bado tukijiuliza angekuepo leo kama sio kifo kumchukua angesemaje, angefanyaje. Na zaidi inatukumbusha kuishi katika yale aliyokua akiyasema na pia inatoa nafasi ya kufanya maombi kwa marehemu
 
(1) Wilaya ya Butiama - Mwalimu J.K Nyerere (Nadhani ipo ingawa sina uhakika).

(2) Wilayani huko Pemba - Mzee A.H Mwinyi

(3) Wilaya ya Masasi - Mzee B.W Mkapa

(4) Wilaya ya Bagamoyo - Mzee J.M Kikwete.

(5) Wilaya ya Chato - Mzee J.P Magufuli

Ningeshauri wilaya mpya zinazoanzishwa kwenye maeneo hayo zipewe majina ya viongozi hao
 
Hakuna mtu aliyeandika barua ya kuomba kuwepo duniani (just by chance) kufa ni tukio ambalo halikwepeki, hivyo ni kumbukumbu nzuri likitokea. Japo hakuna anaejua kama roho inaenda wapi ila tunakumbuka mzunguko wake haha duniani.
 
Back
Top Bottom