Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,320
Inasikitisha na inamaanisha kuwa CHADEMA watafute watu wenye mismamo katika chaguzi zijazo. Taarifa niliyoipata toka Tarakea Rombo hivi punde ni kuwa aliyekuwa ametangazwa diwani wa Tarakea (eneo la mjini), amekana matokeo yake, na kwa kushirikiana na msimamizi wa uchaguzi kata hiyo na aliyekuwa mgombea wa CCM, inasemekana matokeo hayo yamebadilishwa na sasa mshindi atakuwa huyo wa CCM. Taarifa kutoka kwa watu wa Rombo zinasema kuwa hizo ni juhudi kubwa (za kifisadi), alizofanya Ndg. Maulid Swai, tajiri wa eneo la Tarakea, na inasemekana ametoa sh m15 kwa diwani huyo ndipo akakubali kukana ushindi wake. Inasemekana pia baadhi ya waliokuwa mawakala wa CHADEMA maeneo hayo nao 'wametolewa' kwa kiasi fulani cha hela, na kukana matokeo yaliyoonyeshwa kwenye fomu.
Kutokana na utata wa hali hiyo, inasemekana wanaharakati wa chadema eneo la Tarakea, wawakamate makada wao waliohusika na dili hilo, lakini inasemekana hadi sasa ni wawili wamekamatwa, na wengine wamefanikiwa kutoweka, akiwepo huy aliyekuwa diwani! Huyo jamaa ambaye kwa asili yake ni mtu wa Tanga, inasemekana kwa sasa ameshatoroka, kurudi kwa usambaani. Pia taarifa zinasema kuwa Bw. Maulid na Bw. Mhindi (ambaye mke wake alikuwa anagombea udiwani kwa CCM), wanajitahidi kwa nguvu zao za fedha kumshawishi aliyeshinda udiwani kata ya Nanjara-Reha naye akane ushindi wake lakini inasemekana hadi sasa jamaa amekataa, pamoja na kuwa dau analoahidiwa limeshafika m30.
Naomba walioko Rombo, kna Paygod, tupeni habari zaidi...