Elections 2010 Baada ya kushindwa, apewa m15 na kuukana ushindi wake huko Rombo...

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Inasikitisha na inamaanisha kuwa CHADEMA watafute watu wenye mismamo katika chaguzi zijazo. Taarifa niliyoipata toka Tarakea Rombo hivi punde ni kuwa aliyekuwa ametangazwa diwani wa Tarakea (eneo la mjini), amekana matokeo yake, na kwa kushirikiana na msimamizi wa uchaguzi kata hiyo na aliyekuwa mgombea wa CCM, inasemekana matokeo hayo yamebadilishwa na sasa mshindi atakuwa huyo wa CCM. Taarifa kutoka kwa watu wa Rombo zinasema kuwa hizo ni juhudi kubwa (za kifisadi), alizofanya Ndg. Maulid Swai, tajiri wa eneo la Tarakea, na inasemekana ametoa sh m15 kwa diwani huyo ndipo akakubali kukana ushindi wake. Inasemekana pia baadhi ya waliokuwa mawakala wa CHADEMA maeneo hayo nao 'wametolewa' kwa kiasi fulani cha hela, na kukana matokeo yaliyoonyeshwa kwenye fomu.

Kutokana na utata wa hali hiyo, inasemekana wanaharakati wa chadema eneo la Tarakea, wawakamate makada wao waliohusika na dili hilo, lakini inasemekana hadi sasa ni wawili wamekamatwa, na wengine wamefanikiwa kutoweka, akiwepo huy aliyekuwa diwani! Huyo jamaa ambaye kwa asili yake ni mtu wa Tanga, inasemekana kwa sasa ameshatoroka, kurudi kwa usambaani. Pia taarifa zinasema kuwa Bw. Maulid na Bw. Mhindi (ambaye mke wake alikuwa anagombea udiwani kwa CCM), wanajitahidi kwa nguvu zao za fedha kumshawishi aliyeshinda udiwani kata ya Nanjara-Reha naye akane ushindi wake lakini inasemekana hadi sasa jamaa amekataa, pamoja na kuwa dau analoahidiwa limeshafika m30.

Naomba walioko Rombo, kna Paygod, tupeni habari zaidi...
 
hao nadhani slaa atawashughulikia coz hapendi ujinga kabisa
 
Kazi ipo. Naambiwa hata TAKUKURU ni walaji rushwa wazuri sana, hawali shilingi moja, wanaongea lugha ya mamilioni. Sijui kama ni kweli, lakini kuna mtu mmoja alikuwa analalamika kwamba ukiwaita TAKUKURU uwe na balance ya uhakika mfukoni kumzidi mtuhumiwa unayemuitia jamaa hao.
 
Ndio maana nimekosa imani na watu wa Tanga kabisa, wametuangusha sana hata kwenye Ubunge, hawana muamana hawa...how come uuze udiwani kwa 15m?
Huo ni ufisadi, apatikane mara1 na kuwekwa panapostahili!
 
inasikitisha na inamaanisha kuwa chadema watafute watu wenye mismamo katika chaguzi zijazo. Taarifa niliyoipata toka tarakea rombo hivi punde ni kuwa aliyekuwa ametangazwa diwani wa tarakea (eneo la mjini), amekana matokeo yake, na kwa kushirikiana na msimamizi wa uchaguzi kata hiyo na aliyekuwa mgombea wa ccm, inasemekana matokeo hayo yamebadilishwa na sasa mshindi atakuwa huyo wa ccm. Taarifa kutoka kwa watu wa rombo zinasema kuwa hizo ni juhudi kubwa (za kifisadi), alizofanya ndg. Maulid swai, tajiri wa eneo la tarakea, na inasemekana ametoa sh m15 kwa diwani huyo ndipo akakubali kukana ushindi wake. Inasemekana pia baadhi ya waliokuwa mawakala wa chadema maeneo hayo nao 'wametolewa' kwa kiasi fulani cha hela, na kukana matokeo yaliyoonyeshwa kwenye fomu.

Kutokana na utata wa hali hiyo, inasemekana wanaharakati wa chadema eneo la tarakea, wawakamate makada wao waliohusika na dili hilo, lakini inasemekana hadi sasa ni wawili wamekamatwa, na wengine wamefanikiwa kutoweka, akiwepo huy aliyekuwa diwani! Huyo jamaa ambaye kwa asili yake ni mtu wa tanga, inasemekana kwa sasa ameshatoroka, kurudi kwa usambaani. Pia taarifa zinasema kuwa bw. Maulid na bw. Mhindi (ambaye mke wake alikuwa anagombea udiwani kwa ccm), wanajitahidi kwa nguvu zao za fedha kumshawishi aliyeshinda udiwani kata ya nanjara-reha naye akane ushindi wake lakini inasemekana hadi sasa jamaa amekataa, pamoja na kuwa dau analoahidiwa limeshafika m30.

Naomba walioko rombo, kna paygod, tupeni habari zaidi...

unafahamu fika kuwa habari za aina hii zisizokuwa na ushahidi ni uvumi tu, nyingi ya habari za aina hii huanzishwa na wanapropaganda wa ili kuwavunja moyo wananchi katika maeneo ambayo yako juu kwa upinzani
.
 
This is incredible, yaani kashinda halafu anaukana ushindi? Hawa ndo hawatufai kabisa!
 

unafahamu fika kuwa habari za aina hii zisizokuwa na ushahidi ni uvumi tu, nyingi ya habari za aina hii huanzishwa na wanapropaganda wa ili kuwavunja moyo wananchi katika maeneo ambayo yako juu kwa upinzani
.
na wewe ndo walewale waliokuywa uji wa mtoto uvumi gani kwani mwanzo wa habari ni nini?
 
Lisemwalo lipo kama halipo..... (methali tu jamani)! Tukumbuke kuwa katika safari yeyote kina Iskarioti wapo....yaani kenge. Hawa mpaka damu masikioni! Slaa kiboko yao....WAKAMATWE MARA MOJA. Kama CCM imeshinda kihalali SAWA. Kama ni ujambazi wa utajiri, NO.
 
unafahamu fika kuwa habari za aina hii zisizokuwa na ushahidi ni uvumi tu, nyingi ya habari za aina hii huanzishwa na wanapropaganda wa ili kuwavunja moyo wananchi katika maeneo ambayo yako juu kwa upinzani.

Hiyo ni stori ya alinacha, kitu kisichowezekana kabisa
 
Mameku ni wafanya besara kweli kweli, kumbe! Inasemekana kuwa Lema wa arusa alishaanza kuona kizungu zungu na udelele mwingi kumtoka kwa mamia ya mil za EL alizomwahidi akimsujudia, lakini wenyeji wa Arusa wakasema safari hii, amazao ama zake, utaenda kula ahera na hukumu ni mara matangazo yanapoenda kinyume. Walizilinda kweli.
 
Nnapopata taarifa kama hizi nnamfikilia mzee wangu Dr. SLAA anavyopigania haki ya wanyonge kwa nguvu nyingi na mazingira yasiyo rafiki afu insue kama hizi zinatokea I don't want to imagine what he is going through. Anyway wakati wengine wanapigania Tanzania yenye neema kwa wote watu wanawaza matumbo yao. THIS WORLD IS NOT FAIR especialy kwa wapenda UHURU WA KWELI. Bora uishi na simba kuliko rafiki mnafiki.
 
Mtu kama huyo kwa kweli hakuwa hata na haja ya kugombea alikuwa napoteza muda tu bora angelala nyumbani na mke wake atengeneze watoto zaidi....aaaarggg :A S angry:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom