Baada ya kusakamwa sana, Dkt. Kigwangalla azindua video ya vivutio vya utalii aliyoibuni, asema sasa watalii wataanza kumiminika Tanzania

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,149
Waziri wa utalii Dkt. Kigwangalla leo amezindua video ya kupromote utalii wetu duniani kote.

Dkt. Kigwangalla amesema video hiyo ambayo itasambazwa dunia nzima ikionyesha vivutio vya utalii nchini itawafanya watalii waanze kumiminika Tanzania licha ya mkwamo wa Corona ulioikumba dunia.

Juzikati bunge lilimshutumu Dkt. Kigwangalla kwa matumizi mabaya ya fedha kumbe hawakujua ubunifu mkubwa uliofanywa na Kigwangalla utakaoliongezea taifa fedha za kigeni.
Chanzo: ITV Habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Nimeiona video ni nzuri sana wamejitahidi katika kuweka vivutio mbali mbali heko katika hilo. Ingawa quality ya picha sio nzuri sana but it's better than nothing
 
Hivi kweli watalii watakuja na corona hii , au tunaaminishwa tu. Kwa siku kumi sijasikia zaidi ya ndege iliyotoka ugiriki na watalii wanne, mi sijui

Tuwe realistic hapa kufungua mipaka these are political gestures that will have little impact on the arrival of the volumes of international tourists required to fire up the engines of this vital industry.....
Kuna issues nyingi sana hazijakaa sawa, mosi international flight kutoka katika nchi zinazoleta wageni, pili uchumi wa hao wageni umeyumba, tatu insurance companies nyingi bado zinahofia kutoa coverage especially kwa nchi ambazo their efforts to manage the crisis zinatia shaka.
 
johnthebaptist,

Bwashee lile dege lililokuwa likivinjari pale KIA lilipotelea wapi? Halafu bwashee juzi gazeti lenu la Lumumba lilikuja na habari ya anga kuchafuka kwa midege ya watalii mbona mnatuangusha? Tuleteeni madege bwashee.
 
Waziri wa utalii Dr Kigwangalla leo amezindua video ya kupromote utalii wetu duniani kote.

Dr Kigwangalla amesema video hiyo ambayo itasambazwa dunia nzima ikionyesha vivutio vya utalii nchini itawafanya watalii waanze kumiminika Tanzania licha ya mkwamo wa Corona ulioikumba dunia.

Juzikati bunge lilimshutumu Dr Kigwangalla kwa matumizi mabaya ya fedha kumbe hawakujua ubunifu mkubwa uliofanywa na Kigwangalla utakaoliongezea taifa fedha za kigeni.

Source: ITV Habari

Maendeleo hayana vyama!
Kwa mawazo yake anafikiri Watalii wanaletwa kwa kuangalia video.....!!?
 
Hivi kweli watalii watakuja na corona hii , au tunaaminishwa tu. Kwa siku kumi sijasikia zaidi ya ndege iliyotoka ugiriki na watalii wanne, mi sijui
Wazungu wengi wamechoshwa na habari za corona,wanataka kupumzisha mwili na akili,nadhani utakua umepata majibu
 
Habari hiyo
20200529_214133.jpg
 
Acheni ujinga. Nani apande ndege kuja Tanzania hata haijulikani jinsi mnapambana na Covid. Hakuna uwazi kabisa. Muwadanganye hao hao vilaza wenzenu.
 
Wazungu wengi wamechoshwa na habari za corona,wanataka kupumzisha mwili na akili,nadhani utakua umepata majibu
Sidhani kama hii ni sababu tosha kaka.... Utalii unaanza pale unapokua na surplus income, pili usalama wa mgeni. Mgeni akishakua na hayo atafikiria kusafiri na si kwa sababu wamekaa ndani mda mrefu
 
Tuwe realistic hapa kufungua mipaka these are political gestures that will have little impact on the arrival of the volumes of international tourists required to fire up the engines of this vital industry.....
Kuna issues nyingi sana hazijakaa sawa, mosi international flight kutoka katika nchi zinazoleta wageni, pili uchumi wa hao wageni umeyumba, tatu insurance companies nyingi bado zinahofia kutoa coverage especially kwa nchi ambazo their efforts to manage the crisis zinatia shaka.
You got it right.
Watalii sio nzi kwamba watadandia tu ndege kesho na kuja.
Ni siasa za kijinga tu mtu msomi to give such a statement.
Na worst, bado balozi za nje hapa wanatoa warning kwa watu wao kuhusu hali halisi na focus zetu za nyungu !!
We messed up sasa tutakula jeuri yetu... !!
 
johnthebaptist,

Bwashee lile dege lililokuwa likivinjari pale KIA lilipotelea wapi? Halafu bwashee juzi gazeti lenu la Lumumba lilikuja na habari ya anga kuchafuka kwa midege ya watalii mbona mnatuangusha? Tuleteeni madege bwashee.
Bwashee vuta subra kidogo......midege itaanza kutiririka kuelekea KIA!
 
Waziri wa utalii Dr Kigwangalla leo amezindua video ya kupromote utalii wetu duniani kote.

Dr Kigwangalla amesema video hiyo ambayo itasambazwa dunia nzima ikionyesha vivutio vya utalii nchini itawafanya watalii waanze kumiminika Tanzania licha ya mkwamo wa Corona ulioikumba dunia.

Juzikati bunge lilimshutumu Dr Kigwangalla kwa matumizi mabaya ya fedha kumbe hawakujua ubunifu mkubwa uliofanywa na Kigwangalla utakaoliongezea taifa fedha za kigeni.

Source: ITV Habari

Maendeleo hayana vyama!
Tupe link ya video tuione tushare iwafikie wengi kusaidia utalii wetu
 
Back
Top Bottom