SoC 2022 Baada ya kupelekwa Kigoma kikazi kama adhabu, niliibadili na kuwa fursa kwangu

Stories of Change - 2022 Competition

SOVIET UNION

Senior Member
Sep 2, 2017
165
373
Adhabu ya kupelekwa Kigoma hii ndivyo ilivyotokea kwangu mwaka 2012, mimi na wenzangu tulikuwa tunafanya kazi kwenye NGOs moja hivi , na tukiwa kwenye project moja wapo Mkoani Singida ilitokea matatizo pale na wakaamua kwamba baadh yetu tutoke twende Kigoma kwenye wilaya za Kibondo, Kakonko na Kasulu. Tulikuwa watu 9 ambao tulipelekwa Kigoma.

SAFARI YA KIGOMA INAANZA
, baada ya kila kitu tulianza safari kwenda Kigoma kwa kupitia njia ya Kahama nakumbuka ilibidi tulale Kahama ili kesho yake tuwahi kuingia Kibondo na baadae Kasulu.

STORY ZA KUTEKA TUNAKUTANA NAZO, Ile tumefika Kibondo tu hata hatujala kwanza tunakutana na story za majambazi Guest tuliofika, kwenye chakula ni story za utekaji ambao ulifanyika jana yake jioni tena mbaya ni kwenye hiyo njia ya kuja Kibondo kutoka Kakonko, eneo linaitwa Kasanda, hatujakaa sawa bado hatujamaliza kula story ya pili ya utekaji, kuna Dada mmoja siku hiyo hiyo alikata tiketi ya kuondoka na kweli kesho yake akaondoka kurudi kwao Morogoro.

MILIO YA RISASI MJINI KIBONDO, hii ilikuwa baada ya kama siku 10 tangu tufike, siku hiyo usiku zilipigwa mjini mida ya saa 3 usiku mbaya zaidi sio mbali sana na tuilikokuwa, yaani sitasahu kesho yake stafu wawili waliondoka kabisa.

MAZINGIRA YA KIBONDO/KAKONKO
, Mazingira ya kazi yalikuwa magumu sana kwa sababu hata field tunaenda kwa hesabu kali sana na inabidi tukienda saa 8 mchana tuwe tusha rudi mjini.

TUKANAKUTANA NA WAZEE WA KAZI LIVE, hii siku huwa sitaki kuikumbuka, siku hio tulifanya kazi Kakonko eneo inaitwa Katanga ni moja ya maeneo hatari sana yale, tukiwa tunaondoka Katanga kuelekea Kibondo kupitia njia ya Mabamba tukakutana na wazee wa kazi wako full mashine, kwenye kona wameweka magogo ili kuwa kidogo gari ipinduke make ilipanda yale magogo, tukasimama na baadaye kidogo jamaa wakatokeza huwa wanaweka magogo na kukaa mbali kidogo, jamaa wakatokeza na silaha zao na hapo hapo tukaamuliwa tushuke na kuanza kusachiwa pesa, jamaa walibebe pesa na simu zetu zote, baadae walituachia na hapo watu wamechanganyiwa ni vilio njia nzima kwenda Kibondo na tukaenda kutoa taarifa Polisi, Kesho yake stafu 4 waliondoka tukabakia wa watatu, kumbuka waliongezwa stafu 3 baada ya awali wa 3 kuondoka siku za mwanzo, tuliobakia tuliambiwa tukomae.

KUANZA KUWAZOEA WALE MAJAMBAZ
I, ilifika wakati tukawaozea kabisa make sasa hatuoni ajabu kukutana nao na pia story za kutekwa tushaanza kuona ni za kawaida sana, katika kazi zetu mpaka tunaondoka tulikutana nao mara 7. Ila uzuri na kilichokuwa kinatupa moyo ni kwamba wale majambazi hawaui kabisa ingawa zile silaha zao zinatisha sana, kwanini hawaui? Sijui.

KUANZA KUTAFUTA FURUSA, baada ya sasa kuwa nishazoea mazingira ya Kibondo mimi nikaanza kuwaza cha kufanya pale Kibondo, make kukaa tu kutegemea mwisho wa mwezi sio kabisa, na pia nilitaka kuwa bize hasa siku za weekend na pia hatukuwa tunabanwa .

KUANZA KUFANYA UTAFITI
; Kwa sababu nilikuwa nazunguka sana vijijni ilikuwa rahisi sana mimi kujua fursa ziko wapi, hasa changamoto za jamii ya vijijini, Vijijini fursa zilikuwepo nyingi sana hasa za mazao, ingawa kote huko sikutaka mambo ya pesa hivyo wazo pekee lilikuwa kufanya Baishara ya kubadilishana bidhaa, niliona ni salama sana kwa sababu ya ujambazi pale. Biashara ya kubadilishana bidhaa niliona naweza ifanya kwa urahisi sana, nilichagua bidhaa mbili tu kutoka kwa wananchi kuku na mayai basi, hizi ilikuwa rahisi kuzibeba kwa sabbau pia tulikuwa na pikiki.

Baada ya Mipango nilianza biashara na nilichokifanya niliweka vituo kama vinne Kibondo na vituo viwili Kakonko, huko tulijenga hadi mabanda ya kukusanyia wale kuku na nilinunua madawa na chanjo za kuwapatia hasa chanjo ya kideri.

Hii biashara ilikuwa ni salama sana kulingana na mazingira na pia hata mzunguko wa pesa vijijini kule, na hata wanakijiji nilihoji walipenda sana.

BIDHAA NILIZO ONA ZA KUWEZA KUWAPELEKEA WANAVIJIJI; Sana ilikuwa mahitaji ya shule kama uniform na madaftari, kalamu, viatu na taa za solar ndogo za kuweza kumulikia ndani, sukari, mafuta ya kula na ya taa na vifaa vya baiskeli make wanakijiji walikuwa na baiskeli nyingi sana.

UENDESHAJI, ilikuwa biadhaa nazituma zinaenda kwa pikipiki yetu na kuna mtu alikuwa anapeleka na pia yeye ndo alikuwa anaenda kukusanya kuku na mayai na kuku na mayai nilikuwa siku ya Ijumaa nasafirisha kwenda Kahama, ilikuwa kwa wiki hatukosi kuku 150 ambao tulikuwa tukiwapeleka Kahama tunauza sh 12,000/ hadi 15,000/ na pia mayai kwa wiki tulikuwa hatukosi trei hadi 50. Biashara ilikuwa na faida sana na salama sana na ilikuwa msaada sana kwa wanavijijji pale hasa ambao hawakuwa na cash ambao ni lazima wakauze kuku au mazao ndio wapate pesa.

MAFANIKIO, kulikuwa na mafanikio makubwa sana ya biashara ile kiasi kwamba kuna wakati raia nao walianza kuiga na kufanya mimi nilifurahi kuona wanafanya pia na wao kwa sababu mwanzoni walikuwa ni cash tu na bidhaa zetu zilikuwa hazikai kabisa, ilikuwa ni lazima kila wiki tuwe tunapelekea bidhaa.

Sikuwahi kuvamiwa kabisa ila waliokuwa wanauza cash kuvamiliwa ilikuwa mara kwa mara sana na kama nilivyosema wale jamaa wanavamia hata kama una ash 7000/.

NILICHO JIFUNZA
, vijijini hasa maeneo ya ndani ndani kabisa huko kuna fursa sana hasa hayo maeneo ambayo watu huwa wanayakimbia kuna fursa kubwa za mtu kutoka kabisa kimaisha, mijini kushajaa sana, ni sawa na sasa Wazungu na Wachina wanavyokimbilia Afrika ni kwa sababu wanakimbia ushindani kule kwao, Unakuta kule China kila mtu ni mjanja sana hivyo ili kuendea kuishi lazima wakimbie na kuja Afrika kama wawekezaji.

Maeneo ya pembezoni yana fursa sana, sisi tumekuwa tunalalamika tu mara ohoo hakuna umeme, hakuna maji, mzunguko wa pesa mdogo na kadhakika, hizo zote ndo fursa zenyewe za kuanza nazo kule.

Unaweza pangwa huko kama adhabu ila ukaja kuibadili adhabu kuwa fursa ya kutisha na hadi waliokupelekea kule wakatamani tena wakutoe wakupeleka mjini make wanaona unafaidi sana kule walikokuepeleka kutumikia adhabu.

Wengi tumeishia kuacha kazi, kufanya kila namna hadi kwenda kwa waganga, ili turudi mijini,ila naamii kule kuna fursa za kipekee kabisa na kokote kuliko na binadamu basi maisha yako pale.

USHAURI, yale mazingira magumu ya wananchi kule vijijini ukiweza kuyageuza kuwa fursa utapata sana pesa na mpaka wajanja wengine waje wewe ushatengeneza jina kubwa sana.
 
Upvote 12

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
5,207
11,470
Leo najitaja kama uliwahi kufika vijiji vya kayenze, muhange, kibale, ukaona tandam kama mbili zinapishana zimeandikwa mungu wetu sote, zinapiga exchange ya mazao burundi to tanzania to Uganda na zinapaki gwarama basi ujue ni mwana jf mwenzako hapa mpambanaji hua yuko kote huko, bu the way hongera sana sana,
 

million mile

Member
Aug 27, 2021
5
3
umenikumbusha mbali sana mkuu hayo maeneo hususani kakonko kukaa kule kunajitaji roho ngumu sana ila ukipazoeya panakua pa kawaida.

Fursa kule zipo kama gunia la mahindi kutoka kwa warundi ni 30000 tu..... ukiweza kuleta mjini unapiga pesa ya maana
 
6 Reactions
Reply
Top Bottom