Baada ya kuoa/kuolewa, nini umeacha kukifanya?

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Pia inawahusu wale ambao hivi karibuni watafunga ndoa. Nawafahamu baadhi ya watu wameacha kufuatilia michezo, kuhang out na mambo mengine kwa sababu wapo kwenye ndoa.

Mwana MMU vitu gani ambavyo ulivi sucrifice na kuviacha baada ya kuwa upo kwenye ndoa? Na ambao upo njiani kufunga ndoa, vitu gani umepanga ku give up after marriage?

Asanteni
 
kwamtoro umesema kwa wale wanaotarajia ina maana na sisi ambao tupo kwenye ndoa haturuhusiwi kuchangia
vingi sana aise outing zisizo na mpango
kulala kokote kule unakotaka
kurejea nyumbani majogoo kutokana na kwenda club japo club tunaenda ila sio tena kurudi majogoo
kula popote unapotaka ukirudi nyumbani tumbo limejaa
 
Last edited by a moderator:
Nimeacha kabisa kuhudhuria music shows, vilevile mambo mengi kufanya sijiamulii mara nyingi ni lazima tujadili kwanza!
 
binafsi nilipunguza idadi ya mitoko isiyo na mpango maalum hiyo ndo ilikuwa
ishu nyeti kwangu, kwani mwandani wangu angenishangaa kila wakati
nikimuaga kuwa naenda shangazi mara hoo! kesho kutwa kwa rafiki
yangu yuko kibaha, mtondogoo kwa rafiki aliyeko libumbashi si ataona
sasa huyu mwanamke hamfai kwani sikai naye na kufurahi naye ni mitoko
tu ndo maana niliipunguza ili kuwa bize na yeye tu laazizi wangu
Pia inawahusu wale ambao hivi karibuni watafunga ndoa. Nawafahamu baadhi ya watu wameacha kufuatilia michezo, kuhang out na mambo mengine kwa sababu wapo kwenye ndoa.

Mwana MMU vitu gani ambavyo ulivi sucrifice na kuviacha baada ya kuwa upo kwenye ndoa? Na ambao upo njiani kufunga ndoa, vitu gani umepanga ku give up after marriage?

Asanteni
 
Kiwa wewe ni balaa
inaelekea ulikuwa unalikung'uta sana aise

Ili kuepukana na vishawishi na magonjwa,
Ni nzuri kwa afya hasa ukitumia kwa kiwango kilichothibitishwa na daktari.
"Upigaji wa nyeto kupita kiasi ni hatari kwa afya yako"
 
Last edited by a moderator:
Nimeacha kabisa pombe,japo nilikuwa nakunywa mara chache sana yaweza kuwa mara tatu au nne kwa mwaka. Nilivyoona na yeye anapasha tu ikabidi nijitoe tusije kukosa wa kumuonya mwenzake akizidisha.
 
Nimeacha vifuatavyo
1.pombe kali nimebakia kunywa wine tu tena nyumbani
2.matembezi na mashost /kuzurura
3.nimecut off marafiki wote wa ujanani nimebaki na decent tu na sio ukaribu kama zamani
4.nimebadili mavazi yangu ya ujanani nimeacha kabisa
5.kwenda kule new afrika hotel upande wa kushote nimeacha kabisa nilikuwa napenda sana mazingira yale japo sio mcheza kamari
6.na mambo mengine mengi
 
Nilivyoviacha
1. Kwenda FM academia, japo niliendelea kwa muda flani
2. Kutongoza
3. Kula hotelini
4. Kutumia colgate

vipya
1. Natumia wahitedent
2. Napenda pensi
3. Napenda nyimbo za dini ya kikristu
 
Nimepunguza kabisa ukaribu na marafiki mashosts na nimepunguza outings! Nimepunguza kutoa misaada na kwenda kwetu. Sababu sasa nimebeba pia jukumu la familia yangu.
 
Usanii tu huu, kuacha wapi. tunaona wangapi usela palepale. Halafu ningependa sana kusikia wadada wameacha kuvavaa visketi vyao vipupi ovyoovyo
 
Ili kuepukana na vishawishi na magonjwa,
Ni nzuri kwa afya hasa ukitumia kwa kiwango kilichothibitishwa na daktari.
"Upigaji wa nyeto kupita kiasi ni hatari kwa afya yako"
Mkuu kiwia kiwango kilichipendekezwa na daktari ni mara ngapi kwa wiki au mwezi au mwaka au ni pale unapojisikia
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom