mi nina story moja ya mshikji wangu flani hapa kitaa. yeye alitokea kumpenda dada mmoj hivi ambaye alikuwa anajiuza, jamaa seriously akampenda kutoka moyoni. basi jamaa akaona si mbaya kama akimwambia!! yule dada hakuamini kabisa kama anaweza kuja kuwa mke wa mtu, kwanza alimkataa yule jamaa, kwa ajili ya hali aliyonayo!
basi jamaa akakomalia mzigo, hatimaye yule dada akakubali!! jamaa akafanya mpango, akamwachisha kwanza ile kazi yake, then akakaa nae kwa muda then akamuoa!!!!
yule dada alipatwa na furaha ya ajabu, na wala hakuwa n tamaa ndogondogo za labda kutoka tena kwenda kuuza!
alichofanya, ili kuvunja mahusiano na mashoga zake(si alishakuwa mke wa mtu bwana!!!!!!), akaamua kubadili laini ambayo alikuwa akiitumia na kununua nyingine, akapiga biti mashoga zake (waliokuwa wakijiuza nae) kufika home kwake!!
basi dada kwa sasa yuko kwenye ndoa yake na kadumu mpaka sasa!!
via
emperor