Baada ya kuhitimu chuo uliendeshaje maisha?

Mleta mada, hongera sana kwa kuendea kilimo... Ila kwa uelewa wangu ni kwamba mtu yeyote ategemeae kilimo kuwa ndio biashara yake pasipokuwa na kazi nyingine imleteayo kipato ama kila siku au kila mwezi, mtu huyu atabaki kuwa masikini mpaka kufa kwake. (Kilimo ni biashara ya msimu). Binafsi baada ya kuhitimu chuo nilijiingiza mchanganyikoni mtaani kisha kuendesha bajaji, saizi nafanya ishu zangu tu freely
Nimekuelewa mkuu.
 
Nilivolunteer 1 year bure ila nilipata uzoefu mkubwa sana wa nilichosomea nikawa navifanyia kazi kuna siku napata pesa siku nyingine kapa nikaacha nikahamia pengine kuvolunteer nikavolunteer kama miezi tisa ndipo ikapatikana nafasi moja nanikawa peke yangu niliefanyiwa interview nikapata kazi hiyo nikapanga nyumba double self fasta coz hakuna kitu kilikua kinaniuma kama unakuta picha kwenye group imeandikwa kama ulitumia let say chupa flani za soda na bado unaishi nyumbani inabidi uhame daa nilikua najisikia vibaya sana au kwenye group wanaulizana vp mshahara ushatoka kwan hapo nilikua nasema lini itakuja kuwa ila kila mtu ana muda wake Mungu amempangia so tusiache kumuomba na kumshukuru kwa kile kidogo alichotujalia
Hongera sana mkuu.
 
Mungu hutenda kwa wakati wake..kikubwa usikate tamaa..nakumbuka nimemaliza coz ya afya 2015..2016 jiwe kapiga ban ajira mpka uhakiki wa watumishi uishe..nikaona isiwe tabu nikajichanganya kitaa nikawa nachukua karanga vijijini naleta mjini nakoboa kisha nauza..nililima dengu nazo zikaniweka mjini..nikapata kazi za tempo shirika fulani nikawa napiga maisha yakasonga..tempo ikazingua nikajitolea mahali flan..kwa kifupi nimegusa kwingi..ila nashuru mh baada ya kuruhusu mambo yakakaa sawa now napambana nakazi.

Never give up in life.
Hongera mkuu endelea kupambana.
 
Shinda aibu,shida uvivu,shinda maumivu,shinda macho na mitazamo ya watu.

Hakika ukifanya hivyo utafika mbali,naamini mtaani hakuna siku ukakaa bila kupata deal la aina yeyote isipokuwa ni mitizamo yako na fikra zinavyo kuongoza,mkuu shinda moyo wako nitakushangaa sana kama ukisema mtaani maisha magumu yamkini ni kijina uliekamilika,stick to your basic weka nia focus kwenye mambo yako usitizame mtu wala fursa itakayo jitokeza mbele yako, kila cha mbele yako kiwe halali.kama ukishindwa hivi basi nenda kasemezane na kanji(1xbet),

1xbet hii ni kampuni ambayo kwa 70% itapunguza kupata loss kutokana na ugeni wako.
 
Mkuuu kubet???? aisee hii kitu inaweza kukuua
 
Ngoja tuchangie mawazo kwa vijana, kwanza kabisa kipindi nipo chuo niliwaza nikimaliza chuo tafanya nini, hii nawapa haya ambayo bado wapi vyuoni kwa sasa waza utafanya nini ukimaliza chuo kabla ujamaliza chuo

Kwakua nilipata wasaa wakuwaza basi nikamua kuwa mtumwa wa boom langu sikuitaji kabisa kukaa hostel za chuo nilipanga mtaani, tena nikawa nalipa nauli kwenda chuo Siku nimefulia natembea

Kwaiyo boom likitoka nikawa natoa kidogo nanunua assets za ndani, mda wa field pesa ikitoka hivyo hivyo nanua vitu vya ndani hii ndio ilikuwa njia yangu ya kusave pesa ingawa nilijua siwezi kuuza TV zaidi ya being niliyonunulia lakini sawa haya ikiwa being ya chini tapata pesa kuliko kukosa kabisa

Kwaiyo mwaka wa mwisho tumemaliza mitihani kila kitu nikaita dalali nikampa being nayoitaji kuuza vitu vyangu vya ndani, akatafuta wateja tukauza nikapata kama milioni mbili na nusu, laki tano akachukua dalali million mbili nikawa nayo kesho yake nikabeba mabegi yangu nikarudi kwetu sababu familia ilinituma kusoma nirudi na cheti siyo TV nk kwaiyo niliporudi mtaani bank na million mbili nikawa wiki nzima nifanye nini

Nikapata wazo nikaangalia nini kipo sokoni mda huo na vijana wanaitaji ndio nikafanyia kazi kipindi hicho namaliza chuo nguo aina ya T shirt za kuprint zipo sokoni basi nikawa nachukua T shift manga plan naprint nauza nimeuza sana yani maisha yakawa matamu
Nini sasa nataka kuwambia mlio maliza chuo kwa sasa

Angalia nini kipo sokoni na kina lips kifanyie kazi, mmetoka chuo bado vijana fursa zipo nyingi sana changamkeni, msishinde instance na whatsap tafuta kitu Fanya kipindi unasubilia mambo mazuri.
 
Kuna Dogo kitaa tulikuwa tunapiga nae story akuwa anasema hawezi kufanya kazi ya laki tatu. Kwake yeye kazi ni kuanzia million 3.

Sasa kamaliza chuo mwaka huu, wakongwe tunamuangalia sasa ayaishi maneno yake
 
Atapata tabu sana..kitaa hakijui digirii kinajua uchakarikaji na kujitoa akili ili upate pesa..every shilling counts.
 
Ngoja tuchangie mawazo kwa vijana, kwanza kabisa kipindi nipo chuo niliwaza nikimaliza chuo tafanya nini, hii nawapa haya ambayo bado wapi vyuoni kwa sasa waza utafanya nini ukimaliza chuo kabla ujamaliza chuo

Kwakua nilipata wasaa wakuwaza basi nikamua kuwa mtumwa wa boom langu sikuitaji kabisa kukaa hostel za chuo nilipanga mtaani, tena nikawa nalipa nauli kwenda chuo Siku nimefulia natembea

Kwaiyo boom likitoka nikawa natoa kidogo nanunua assets za ndani, mda wa field pesa ikitoka hivyo hivyo nanua vitu vya ndani hii ndio ilikuwa njia yangu ya kusave pesa ingawa nilijua siwezi kuuza TV zaidi ya being niliyonunulia lakini sawa haya ikiwa being ya chini tapata pesa kuliko kukosa kabisa

Kwaiyo mwaka wa mwisho tumemaliza mitihani kila kitu nikaita dalali nikampa being nayoitaji kuuza vitu vyangu vya ndani, akatafuta wateja tukauza nikapata kama milioni mbili na nusu, laki tano akachukua dalali million mbili nikawa nayo kesho yake nikabeba mabegi yangu nikarudi kwetu sababu familia ilinituma kusoma nirudi na cheti siyo TV nk kwaiyo niliporudi mtaani bank na million mbili nikawa wiki nzima nifanye nini

Nikapata wazo nikaangalia nini kipo sokoni mda huo na vijana wanaitaji ndio nikafanyia kazi kipindi hicho namaliza chuo nguo aina ya T shirt za kuprint zipo sokoni basi nikawa nachukua T shift manga plan naprint nauza nimeuza sana yani maisha yakawa matamu
Nini sasa nataka kuwambia mlio maliza chuo kwa sasa

Angalia nini kipo sokoni na kina lips kifanyie kazi, mmetoka chuo bado vijana fursa zipo nyingi sana changamkeni, msishinde instance na whatsap tafuta kitu Fanya kipindi unasubilia mambo mazuri.
Shukrani kwa ushauri mzuri Sana na hongera sana kwako.
 
Back
Top Bottom