Baada ya kuhitimu chuo uliendeshaje maisha?

Maccavelli

Senior Member
Jul 18, 2018
173
174
Habari za wakati huu wadau wa JF, natumai muwazima, binafsi niko poa..

Kama Mada isemavyo hapo juu naomba kapata uzoefu wenu wadau baada ya kuhitimu chuo kikuu uliendeshaje maisha bila ya kuwa na shughuli yoyote rasmi?

Uzoefu na changamoto ulizozipitia hadi ukamudu kusimama kimaisha wewe binafsi maana kama tujuavyo ajira kwa Sasa sio rahisi kupata wadau, hivyo mchango wako ni muhimu kusaidia sisi wengine

Binafsi ni muhitu pia nimejikita ktk kilimo lakini mambo hayakwenda sawa kabisa mpaka sasa,
 
Pole mkuu, labda ungesema umesoma coz gani na chuo gani ingesaidia kidogo...
Nakumbuka nikiwa mwaka was pili nilihamia mtaani nianze maisha taratibu, Mungu si athumani nilipomaliza Tu wiki inayofuata nilipata kibarua...

Nirudi tena kwako, nikiwa mtaani nilijiandaa kwenda kufundisha tuition kama nisingepata ajira... Wakati huo hui nikiomba kaz za sales kwenye makampuni ya bidhaa mbali mbali... Kama upo Dar nenda Urafiki, Azam, Mo, Kariakoo nk.... Lakini pia tafuta watu wanaojulikana mjini wakusaidie kutafuta pa kujishika...
Kamwe usikae nyumbani kumsubiria MTU au kazi.....
 
Ni kweli mkuu kukata tamaa ni dhambi Kubwa, mimi ni muhitu wa fani ya ualimu (bachelor of education in special needs)mkuu.
 
Nilipohitimu bachelor yangu nilihama na vyombo vyangu vyote kutoka maeneo ya chuo nilipokua nimepanga na kupanga mbali na chuo ili kuendelea na maisha.

Siku moja ktk kutafuta sehemu ya kujishikiza nikapata ofisi ya kulipwa buku 2 kwa siku nami sikukataa maana nilikuwa najua nini maana ya kuanzia chini, japo kulikuwa na viposho vya msimu vya hapa na pale ambavyo vilinisaidia kulipia pango na kuweka akiba kwa kununua asset ndogo ndogo zenye capital gains na siyo cash flow.

Baada ya muda fulani nikaendelea kutafuta kibarua kingine ndipo siku moja nikaunganishwa na best yangu mmoja tuliyesoma chuo kimoja, kibarua hicho ni cha kawaida lakini kilinipatia hela ya kunitunza, kutunza wazazi wangu, kununua mahari ya kuolea na hatimaye muda fulani baadae nikalipa mahari na kuoa kwa neema ya MOLA.

Mimi ni mtaalamu wa ubahiri ndiyo maana nikaweza kutumia vyema hela kidogo kufanya mambo makubwa kwa muda mfupi lakini pia heri ya MOLA ilinitangulia sana.

Jifunze sana jinsi ya kuanzia chini, jifunze na ubahiri pia, jifunze na networking kwa kuwa karibu na marafiki wa faida, jifunze kuwa na malengo ya kuoa mwanamke sahihi ili akili yako itulie, ishi na siyo kujiandaa kuishi.
 
nialianza nunua gododro mwaka wa kwanza mpka nafika mwaka wa tatu nkawa na vitu vyote vya ndan mpka friji nkapanga makumbusho mkopo wa mwsho nkalipa pango mwaka mzima pesa ilyobak nkaanza uza viatu vya kike makumbsho stand.kuanzia july ikawa biashara yangu mwez wa kumi nkapata kaz
 
Tafuta sehemu ya kujitolea walau miezi kadhaa baada ya kumaliza ili upate ka uzoefu halafu ndo uchakarike mtaani waajiri wengi wanahitaji mtu mwenye uzoefu walau kidogo. Usimalize tu chuo na kuingia mtaani moja kwa moja fanya internship walau miezi mitatu kisha fanya hustling zako
 
Mimi nakumbuka wakati namaliza chuo, niliamua kwenda kijijini nikajitolea kufundisha Masomo ya Sayansi Hisabati na Fizikia.Uzuri nilikuwa na Mzazi mwenzangu/Mke ambaye nilikuwa nimemkatia Boom kimtaji cha tubiashara tudogo, hivyo alisaidia baadhi ya mahitaji baada ya kuhitimu chuo. Ulipofika msimu wa kilimo niliamua kuacha kufundisha nikaingia shambani.Nilipiga alizeti na karanga kiukweli zilitoka vizuri sana.Kumbuka wakati huo wote nilikuwa siachi kupitia website za ajira na kutuma maombi sehemu mbalimbali.Katika maombi 50 niliyofanya niliitwa usaili maombi 15 na niliweza kuhudhuria saili 5 pekee kutokana na ukosefu wa fedha kushiriki.Hata baada ya kukosa kibarua katika saili hizo 5 nilianza tena kutuma maombi sehemu mbalimbali hata kama hawakutangaza nafasi,mwishowe Utumishi wakatoa tangazo la kuhitaji kada yetu niliomba na niliitwa usaili baada ya miezi 5 na kufaulu usaili hatimaye kuitwa kazini baada ya miezi 3 ndiyo nikajiunga na kuhudumia umma.
 
Tafuta sehemu ya kujitolea walau miezi kadhaa baada ya kumaliza ili upate ka uzoefu halafu ndo uchakarike mtaani waajiri wengi wanahitaji mtu mwenye uzoefu walau kidogo. Usimalize tu chuo na kuingia mtaani moja kwa moja fanya internship walau miezi mitatu kisha fanya hustling zako
Good idea nimesomea community development je naeza jitolea katika taasisi zipi
 
Habari za wakati huu wadau wa jamii forum, natumai muwazima, binafsi niko pw.

Kama Mada isemavyo hapo juu naomba kapata uzoefu wenu wadau baada ya kuhitimu chuo kikuu uliendeshaje maisha bila ya kua na shughuli yoyote rasmi?

Uzoefu na changamoto ulizo zipitia hadi ukamudu kusimama kimaisha wewe binafsi maana kama tujuavyo ajira kwa Sasa sio rahisi kupata wadau, hivyo mchango wako ni muhimu kusaidia sisi wengine

Binafsi ni muhitu pia nimejikita ktk kilimo lakini mambo haya kwenda Sawa kabisa mpaka sasa,
Mim baada ya kumaliza chuo mwaka.2016 nikajiajiri kupitia kampuni ya urembo asilia ili kuijiongezea kipato kwa kweli namshukuru mungu kwani bila hivyo life kita ingekuwa ngumu
 
Pole mkuu, labda ungesema umesoma coz gani na chuo gani ingesaidia kidogo...
Nakumbuka nikiwa mwaka was pili nilihamia mtaani nianze maisha taratibu, Mungu si athumani nilipomaliza Tu wiki inayofuata nilipata kibarua...

Nirudi tena kwako, nikiwa mtaani nilijiandaa kwenda kufundisha tuition kama nisingepata ajira... Wakati huo hui nikiomba kaz za sales kwenye makampuni ya bidhaa mbali mbali... Kama upo Dar nenda Urafiki, Azam, Mo, Kariakoo nk.... Lakini pia tafuta watu wanaojulikana mjini wakusaidie kutafuta pa kujishika...
Kamwe usikae nyumbani kumsubiria MTU au kazi.....
wazo zuri sana
 
Back
Top Bottom