Hakuna kitu ambacho sikielewi kama unakuta mtu amekaa chuoni miaka 3 au zaidi kapata hicho alichopata let's say ni u-injinia au udaktari au ualimu halafu anakuja mtaani anauza supu au nguo,
Sisemi kua ni vibaya kufanya hivyo ila kinachonishangaza ni kwamba sasa kama dream ilikua ni hiyo kwanini kuhangaika kwenda kusomea kitu ambacho hakina relation na ulichosomea? Haumuoni huko ni kupoteza muda? Mana kama vision ilikua kuja kufanya biashara baada ya kuhitimu sasa si ungesoma business related courses basi (ambazo zingekusaidia unachokuja kutaka kufanya hapo baadae baada ya masomo)
Mi nachokiona wengi wetu tunaenda vyuoni tukiwa hatujui tumeenda kufanya nini. I mean mtu anafanya maamuzi ya kusomea kozi fulani ili hali hajui ataenda kuifanyia nini mtaani!.