Ila cha muhimu mkuu ukiona umepata unayempenda basi anza kuwaza ndoa.
Siku zote hali uliyokuwa nayo haikatiki kirahisi kama unavyodhani.
Nina mengi ya kuandika kutokana na uzoefu wangu ila wacha niandike machache huwenda yakakusaidia.
Unajua kaka kitu kizuri huzidiwa na kizuri ili kiwe kizuri zaidi ya kizuri.
Yaani ukiwa na gari kali ukaipenda,utakuja kuona gari kali zaidi ya hiyo mkuu alafu utaanza kuidharau hii ya mwanzo wakati ulishaipendaga sana.
Hapa ni kuonyesha tu kwamba nafsi zetu zinatoa nafasi kupokea mapenzi na machukizo.ukijikuta umependa mtu fulani saaaana.basi jua utaendelea kumpenda mpaka atakapokuja mwingine wa kuziba hiyo nafasi ya huyu au ukafuata njia ambazo zinasaidia kukupelekea kutokumpenda mtu huyo.
Hali yako ya sasa nadhani kila mtu mzima alopitia hali hiyo anaijua sana.la muhimu kumbuka tu kwamba ukiona umeenda michezo mara mziki huku akili yako inajua kwamba unaenda kupoteza mawazo basi jua tu akili yako nayo itasema kwamba napoteza mawazo ambayo hayakupotelea humu kichwani.
Hivyo utatafuta mziki,au timu au pombe lakini huwenda ikawa isisaidie sana mkuu.
Mimi nakushauri endelea na ratiba za kawaida tuuu mkuu wala usikifanye kitu ambacho hakiko katika mapenzi yako eti kisa tu upoteze mawazo,nakuambia ikiwa unasema unaenda mpirani kupoteza mawazo sasa vipi ushindwe kupoteza mawazo pasi na kwenda mpiran?
Mawazo hayapotezwi mkuu nakuambia endelea na ratiba zako za kawaida tu hiyo ni hali ya kawaida tu ambayo moyo wako umeshtuka kupokea majibu ambayo asili yake sio maswali.
Utakaa sawa mkuu endelea na ratiba zako,ukianzisha katabia kengine ili uondoe mawazo utakuwa unaipa akili kazi mbili.
1.kuondoa mawazo
2.kuzoea hicho ambacho umeanza kukifanya.na mwanzo mgumu tu.hivyo utakuwa na kazi mbili.
Lakini ukiwa unaendelea na ratiba zako tu huku unaumia kiuanaume basi jua unaioa akili kazi moja tu ya kupambana na maumivu.
Nakutakia siku njema bado nafatilia coment niendelee kujifunza kutoka kwa wenzangu.