Adimu
JF-Expert Member
- Aug 22, 2013
- 678
- 308
- Thread starter
- #41
Adimu:
Huu Ujumbe Print kisha mpelekee mkeo(Shemeji yetu)
Hallo Mrs:Adimu
Ninakupa pongezi sana na mungu akubariki kwa kuvumilia ndoa ya mumeo kwa kipindi kirefu katika hali ya Ulevi.
Mungu akubariki na atakupa njia ya mafanikio na ndoa yenye amani na furaha kati yako na mumeo.
Na pi mungu awajaalie awape kizazi chema chenye kujitambua.Nakushauri kama unawatoto jaribuni kuwa nao pamoja na karibu ili kufuta makosa ambayo Mumeo alikuwa akiyafanya mbele ya watoto ili watoto waweze kujua kwamba baba yao sio yule wa zamani na hii itawajenga kisaikolojia na kuwa na furaha nahat kuweza kufanya vizuri kwenye masomo yao.
Fanyeni sana ibada kumuomba mungu nakumshukuru kwa hili na awalinde na kizazi chenu,maana walevi wengi uzeeni inakuwa ni tatizo,na Pombe inafuata kizazi kama hakitajitambua.Kuna watu wanalewa Babu,bibi hadi wajukuu.Ikifika umri fulani hakuna hata mmoja mwenye kujitambua kimaisha.
Wapo wanaoenda na watoto wao Bar huku wakijua kabisa kwamba ni kutengeneza kizazi kiharibifu na laana mbele ya Mungu.
Ulevi ni chanzo kikuu cha maasi,ikiwemo Uzinifu,magonjwa ya Zinaa hasa Ukimwi ambao wengi walevi umewapeleka na wanao,maradhi ya Sukari,ini,figo nk.Kwa ufupi ulevi ni Laana.
Mungu awabariki katika ndo yenu na kizazi chenu(AMEEN),ibada muhim sana
Ni ujumbe mzuri sana huu hakika mwenzangu ataufuraia! Shukran