Baada ya kuachana na matumizi ya pombe

Baada ya kuachana na matumizi ya pombe

---- mlevi mmoja mbwa pale Mwenge baranara ya ITV anatamba kwamba ana zaidi ya miaka kumi hajanywa chai. Utamkuta asbh kwa mama ntilie akinywa viroba na chapati. Afya yake ni mgorogoro tupu

ha ha ha ha ha ha
pombe pombe ukizidisha inakuwa noma
pombe pombe ukizidisha inakuwa sooo

leo naimba tu
 
Ashukuliwe Mwenyezi kwa kutupa pumzi mpaka muda huu! Napenda niwashirikishe katika furaha na maisha mapya tangu nilipotoka kwenye Team gambe!
1: Nawai kuludi kwangu.
2: Pesa ninayoipata naitumia vizuri na kufanya vitu vyenye kuleta maendeleo.
3: Swala la hang over na kuzimua nimeshalisahau.
4: Ugomvi na mavulugu yote kwisha.
5: Maelewano na mama watoto yamekua kwa kiasi kikubwa.
6: Kuchoka choka nikiwa kazini kumekwisha.
na mengineyo meengi!
Wito wangu kwenu; Pombe ni adui wa maendeleo, ukitaka kuishi kwa mafanikio huna budi kuiacha.


...kuludi = kurudi
 
ila unakosa mengi madili kwenye pombe...labda kama wewe si mtu wa dili

pesa unatafuta ili utumie...mie nakushauri uache kunywa chai/ supu asubuhi ili uongeze kipato chako...

pombe inasaidia kujiliwaza kama kwenda disco na kwingineko...usipokuwa makin msongo wa mawazo unakunyemelea...

Kuna vitu vingi tu vyakujiliwaza na vitakavyokukutanisha na watu mbalimbali na ukapata madili si lazima unywe pombe mkuu
 
Umepunzika mkuu
Ngoja nikale viroba mie

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Hahahahahaa next time ntakuja kuelezea madhara ya viloba
 
Nasema kutokana na kapiriensi. pombe ni mbaya kwa ubongo. moyo
maini. figo hata utumbo. Pombe ni mbaya kijamii na ndio inayosababisha asilimia arobaini ya maovu duniani. Nenda vituo vya polisi muda wa saa nne usiku utakuta wengi wa wahalifu ni walevi. Familia nyingi huvunjika na kukosa upendo kisa pombe. Wanawake wengi wanachepuka kwa sababu waume zao wakilewa hawawezi kuwahudumia kindoa.
THE BEST TIME TO STOP DRINKING WAS YEARS BACK. THE NEXT BEST TIME TO STOP DRINKING IS TODAY

Nashukuru sana mkuu naamini watatuelewa tu
 
Pombe Mwanakharamu,pombe Ni Mkojo Wa FIRAUNI,AU SHWETAAAN IBLIS, Bora Umeacha Sasa,mi Mwaka Wa 4 Huu Na Mabadiliko Nayaona,wakat Naacha Wapo Walinibeza,tena Niweka Na Msimamo Simnunulii Mtu Pombe Hata Awe Nani, Huwa Nawauliza Wanaotaka Niwanunulie, Je Unaweza Kumwomba Muislam Akununulie Kitimoto?
 
---- mlevi mmoja mbwa pale Mwenge baranara ya ITV anatamba kwamba ana zaidi ya miaka kumi hajanywa chai. Utamkuta asbh kwa mama ntilie akinywa viroba na chapati. Afya yake ni mgorogoro tupu

Yatupasa kuwaonea huruma watu kama hao, badala ya kuamka nakufikilia kulitumikia taifa na kupigania maisha yake yeye anaamka na viroba???
 
Adimu:
Huu Ujumbe Print kisha mpelekee mkeo(Shemeji yetu)
Hallo Mrs:Adimu
Ninakupa pongezi sana na mungu akubariki kwa kuvumilia ndoa ya mumeo kwa kipindi kirefu katika hali ya Ulevi.
Mungu akubariki na atakupa njia ya mafanikio na ndoa yenye amani na furaha kati yako na mumeo.
Na pi mungu awajaalie awape kizazi chema chenye kujitambua.Nakushauri kama unawatoto jaribuni kuwa nao pamoja na karibu ili kufuta makosa ambayo Mumeo alikuwa akiyafanya mbele ya watoto ili watoto waweze kujua kwamba baba yao sio yule wa zamani na hii itawajenga kisaikolojia na kuwa na furaha nahat kuweza kufanya vizuri kwenye masomo yao.
Fanyeni sana ibada kumuomba mungu nakumshukuru kwa hili na awalinde na kizazi chenu,maana walevi wengi uzeeni inakuwa ni tatizo,na Pombe inafuata kizazi kama hakitajitambua.Kuna watu wanalewa Babu,bibi hadi wajukuu.Ikifika umri fulani hakuna hata mmoja mwenye kujitambua kimaisha.
Wapo wanaoenda na watoto wao Bar huku wakijua kabisa kwamba ni kutengeneza kizazi kiharibifu na laana mbele ya Mungu.
Ulevi ni chanzo kikuu cha maasi,ikiwemo Uzinifu,magonjwa ya Zinaa hasa Ukimwi ambao wengi walevi umewapeleka na wanao,maradhi ya Sukari,ini,figo nk.Kwa ufupi ulevi ni Laana.
Mungu awabariki katika ndo yenu na kizazi chenu(AMEEN),ibada muhim sana
 
poor planing and management ndiyo adui wa maendeleo yako .. kama unabajeti ya hiyo sidhani kama maendeleo yatakimbia kisa pombe.... kama ni hivyo basi nahis chakula ndiyo adui mkubwa wa maendeleo...

Uwezi kuishi bila kula hakika utakufa, je usipokunywa pombe utapoteza uhai?
 
Nakupongeza sana kwa kujitambua na kutambua hilo.
Unywaji wa pombe ni hdmbai kwa Ukristo na Uislam.
Na ndio maana mapadri ukiwauliza suala la Pombe wanakujibu moja kwa moja.

Mungu akusaidie kwa hilo,pia jitahidi sana kuwa mtu wa Ibada ili mungu akusamehe uliyoyafanya,wapo watakaokubeza maana wao Pombe ndi maisha yao.
Kufanikiwa na kutofanikiwa ni majaaliwa ya Mungu,ila hakuna amabe hajui kama Pombe imewapati wengi sana Gonjwa la Ukimwi kwa ngono mbovu,na wengine maradhi tele ikiwemo Sukari,Ini,figo nk.

Walevi sikuzote huwa wanamajonzi sana kuondokewa na Member mwenzao na hiyo ndio kazi ya Ibilisi.
Ubarikiwe

Nashukuru sana kwa kunitia moyo, yatupasa kuokoa na wengine!
 
Uwezi kuishi bila kula hakika utakufa, je usipokunywa pombe utapoteza uhai?

vyote ni vyakula ni muhimu kwa mwili a binadamu kwa wakati wake ..... sema kula ni muhimu ziadi... haya hongera kwa kuacha pombe
 
Pongezi mkuu kwa uamuzi wako mzuri. Hata mimi nilikuwa bingwa wa mambo hayo lakini niliacha zaidi ya miaka 15 uliyopita. Kila mtu alishangaa na waliniuliza nimepata wapi dawa ya kuacha kilaji!
 
Pombe Mwanakharamu,pombe Ni Mkojo Wa FIRAUNI,AU SHWETAAAN IBLIS, Bora Umeacha Sasa,mi Mwaka Wa 4 Huu Na Mabadiliko Nayaona,wakat Naacha Wapo Walinibeza,tena Niweka Na Msimamo Simnunulii Mtu Pombe Hata Awe Nani, Huwa Nawauliza Wanaotaka Niwanunulie, Je Unaweza Kumwomba Muislam Akununulie Kitimoto?

Nakupa hongera sana, ukijalibu kumnunulia mtu pombe nisawa na kumuangamiza!
 
Back
Top Bottom