britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 15,636
- 30,004
Habari za siku nyingi, nimekuwa kimya kidogo tokea sakata la bandari limeanza.
Uwekezaji ni mzuri sana, hasa unapofuata misingi sahihi. Hasa kwa bandari zetu, hizi zinataka mapinduzi makubwa sana kutoa au kuondoa ukiritimba uliopo. Hivyo siwezi kupingana na aliyeleta hoja ya kuwakaribisha wawekezaji, japo naweza pingana naye kwa namna sakata linavyopelekwa au lilivyobebwa.
A. Kwanini naunga mkono hoja?
Bandari yetu imekuwa ni ya hovyo sana kwa miaka mingi mno. Kupotea kwa mali za wateja, kuchelewa kwa huduma, kutozwa tozo zisizo sahihi, kuharibu mali wakati wa utoaji. Kwenye suala la mwekezaji bandarini, isiishie kwenye kuleta mikono ya kupakua mizigo au kuweka tehama tu. Bali hata usimamizi wa mapato na mchakato mzima wa kumtoza mteja uwe wazi na makusanyo yaelekee sehemu husika.
B. Mapungufu katika mchakato mzima
Natambua fika kwamba wenye bandari, sisi ndio ilibidi tuande draft ya jinsi gani tunataka bandari iendeshwe, alafu tumpe anayekuja kuwekeza. Najua hilo litakuwa limefanyika, ila kama yamefanyika, basi zitakuwa zimepitiwa hatua hizi.
Mwenye bandari, sisi ndio ilibidi kuandaa proposal na tena kuna hatua:
1. Unaandaa hadidu za rejea, yaani terms of reference (TOR).
2. Unaandaa tangazo ili wazabuni waombe kufuatana na vigezo vyako kwenye Hadidu za rejea.
3. Unatangaza tenda ili watoa huduma waombe kufuatana na vigezo vya kwenye Hadidu za rejea.
4. Mnafungua tenda mbele ya wazabuni.
5. Mnachuja wazabuni kufuatana na vigezo.
6. Mkimpata anayewafaa, mnamfahamisha kupitia offer letter.
7. Anajibu offer letter.
8. Wewe mwenye zabuni, ambaye ndiye unahitaji huduma, unaandaa mkataba. Unawapa draft upande wa pili, nao wanaupitia. Wakikubaliana, mnasaini.
Nadhani huu utaratibu au unaofanana na huu ulifuatwa. Tunasubiri CAG akija kwenye ukaguzi, asije kusema trilioni kadhaa zilipotea kwa sababu ya kutofuata taratibu za mkataba.
C. Udini na ukanda
Ukiwasikiliza vijana wengi mtandaoni kwa sasa, hawajibu hoja bali hisia zimejengeka tayari ndani yetu au yao. Kwamba Wazanzibar wanauza Tanganyika, wakati huo huo Wazanzibar wanatetea hata kila lisilotetewa kisa watekelezaji wanatoka upande wao. Hapa ningeshauri kwanza vijana wazichambue hoja zote za msingi, tuweke ukanda na udini pembeni ili sasa tuongee points. Juzi kuna sheikh mmoja nimemuona anamparua Prof Issa Shivji, kama mtoto mdogo bila kujua mzee Shivji ni miongoni mwa wanazuoni 7 waliopewa direct approach Ikulu na kutoa maoni. Na katika maoni ambayo huwa yanazingatiwa sana ni ya Issa. Anatokea mtu anajiita Sheikh, bila kujibu hoja, anambagua kwa rangi yake. Hilo suala halikuwa sahihi kabisa. Masheikh na Maaskofu, umakini katika kuyaongelea masuala ya msingi kama haya, hasa nisifiche mme-pwaya.
D. CCM inatumia watu wa hovyo kufikisha ujumbe
Chama changu pendwa cha CCM, mmetumia watu wa hovyo sana kufikisha ujumbe au kuelimisha jamii. Nina mifano:
- Hili suala la uwekezaji au ubinafsishaji kwenye bandari, wapinzani wametupiga bao kwenye kutumia watu wajanja na wajuzi wa mambo kudadavua undani. Na ndio maana kila mwananchi wa kawaida anadhani au anajua bandari imeuzwa tayari, kwakuwa wamejadili masuala ya msingi. Na hata wasio wapinzani wamejadili mambo ya msingi haswa.
Mfano, Mama Anna Tibaijuka alieleza kwa kina juu ya usalama wa anga (airspace). Kwamba mkataba, kwa kipengele alichosoma, kuna sehemu inasema kwamba bandarini pale, sehemu kadhaa ft kadhaa kwenda juu, hatutakuwa na mamlaka nayo. Hili suala halijajibiwa zaidi ya kusema na kushambuliwa kwamba ESCROW ni ya Tibaijuka. Mara anamtetea Karamagi wa TCTS. Je, hoja yake imejibiwa?
Lissu yeye kazungumzia suala la watakapokuwa na bandari kavu, hatutaruhusu kujenga feeder roads. Kashambuliwa kwa matusi. Je, hoja hii imejibiwa?
Mkataba hauna ukomo, ni hoja ya kila mtu. Mbona nayo haijajibiwa?
Mgawanyo wa jinsi gani tutapata share haikuwekwa wazi. Basi inabidi CCM watumie wataalamu kueleza kwamba uwenda itasemwa hapo baadaye au kuna sababu kadhaa kadhaa kutosemwa.
Chakushangaza, watetezi wa CCM ni Steve Nyerere, ambaye hata wasanii wenzake hawamkubali popote, hata kwenye sekta ya usemeji walimkataa. Ndo CCM inampa airtime kusemea mambo mazito.
Mtu kama Manara, huyo ndo karibu kabisa kwa maelezo yake yamejaa na ubaguzi ndani yake, kwamba watu wa mikoani hawaruhusiwi kuhoji bandari. Are we serious?
CCM au Serikali ina watu wengi wa kuweza kueleza jambo likaeleweka. Wapo kama Mzee Adam Simbeye wa "This Week in Perspective" na wazee wa namna hiyo, wengi wasomi wanaoelewa masuala haya ya mikataba.
Linapokuja suala la mambo ya msingi ya nchi, tafadhali, akina Mwijaku, sijui Baba Levo, wakae kwenye miziki na media huko. Mambo ya msingi wataalamu wawaeleze wananchi kinaga ubaga, kuliko kuwatumia watu watakao watibua watu au kuwa misled na serikali ikaeleweka visivyo, kumbe si lengo la serikali waseme hivyo.
Ushauri wangu:
1. Kama tumekaa na TICTS miaka zaidi ya 20, aongezewe mwaka mmoja. Huku serikali na wadau waanze kuufanya mchakato upya kwa kutangaza magazeti ya serikali na kwenye televisheni ya Taifa. Kiwepo kipindi maalumu cha kuuelezea mkataba kwa Kiswahili tu na kidadavuliwe na wataalamu. Ifanyike hivyo kila wiki mara tatu kwa muda maalumu ndani ya wiki 52.
2. Mwekezaji naye aelezwe kwamba kuna ABCD tunataka wananchi waelezwe, ili kuzuia baadae asije kuwa raisi wa kariba ya wale wasiofuata sheria kama fulani, akaufutilia mbali.
Mwisho, Tanzania ni zaidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, Tanganyika, ACT, Uislamu, Ukristo, au Upagani.