Baada ya Kikwete sasa kiongozi wa EAC ni Kenyatta

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Baada ya Kikwete kuondoka kiongozi wa EAC kwa wenzetu wanamwona ni Kenyatta. Magu jitahidi kuchukua nafasi hii Kenyatta akiondoka. Kikwete alijitahidi na kuheshimiwa sana. Sasa mambo ya nje tumebaki na vikwazo kila siku hakuna hata statement ya kinachoendelea

 
Maisha kwa zamu Kaka. Nakumbuka jinsi jk alivyokuwa mashughuri nje ya nchi. Jk hakuwa Kiongozi wa mfano EAC tu..jk alikuwa Africa nzima. Yaani Rais wa china ameingia tu madarakani 2012 ziara ya Kwanza ameifanya Tz. Tanzania tulipokea maraisi wa 3 siku 1.. Rais Obama..na Bush one day. Jk alikuwa anaonewa Wivu hadi na wenzake Africa Mashariki. Mungu akupe maisha marefu jk..
 
Halafu Magufuli akimshinda Kenyata ndo aweze kukupata? Mara ya mwisho demu alinifanyia hivyo nilimpiga chini, mambo ya kuchonganisha Wanaume wawili eti mshindi akuchukuwe nilikataa, na mara nyingi unakuta demu mwenyewe anayechonganisha Wanaume wala siyo mzuri.
 
Ila huu ni ujinga sana. Kila mara Kenyatta akienda US hakanyagi red carpet . Sijui kunashida gani.

Mi nazani kuna haja ya kumuelimisha. Hilo rsd carpet ni lake sio la trump na mkewe.
 
Kipimo cha kuwa "kiongozi" ni kutangatanga, kujikomba, kuwa mnafiki na kuwazunguka viongozi wenzako?

Hicho kipimo cha uongozi kitakuwa na hitilafu kubwa.

"Prayer Breakfast"...hizi hizi zilimtoa kimasomaso Robert Ouko! Hivi pale Nyayo hamuwezi mkafanya breakfast na kusali hadi kufunga safari za kila mwaka?
Watu wa ajabu sana!
 
Kipimo cha kuwa "kiongozi" ni kutangatanga, kujikomba, kuwa mnafiki na kuwazunguka viongozi wenzako?

Hicho kipimo cha uongozi kitakuwa na hitilafu kubwa.

Dunia ya siku hizi huwezi kufanikiwa kwa kujitenga mifumo yote Duniani inafanya kazi pamoja hivyo kwa watu wanajua na kuona mbali kujitenga ni kujirudisha nyuma mwenyewe. Kenyatta mfano ame sign mkatapa wa pesa za kujenga Highway kubwa EAC nzima ya juu kutoka Mombasa mpaka Nairobi $3B project. Vilevile kampuni nyingi za technologia ni za nchi nyingine kuanzia technologia za kilimo, simu na hata elimu. Wanasema Kikwete alikuwa anatanga hawajui wanalo ongea maana kasaidia sana mpaka sasa wakina Bill gates waliletwa na Kikwete na kuna mambo mengi sana hata ya usalama huwezi kufanya wenyewe. Hata Tanzania hizo world bank tunazoomba mkopo makao makuu yako wapi? IMF ? UN etc. Kujenga mahusiano ni kitu kizuri sana. Nchi inayo ongoza kwa kulima ni US na sisi tunategemea kilimo kwa mfano. Watalii wanao ongoza kuja Tanzania ni US na ndiyo ina ongoza kutuingizia pesa. Sasa kuna ubaya gani Magu akiwa na uhusiano mzuri na Trump kwa faida ya nchi. Haya ni mambo ya nchi sio Chama

"Prayer Breakfast"...hizi hizi zilimtoa kimasomaso Robert Ouko! Hivi pale Nyayo hamuwezi mkafanya breakfast na kusali hadi kufunga safari za kila mwaka?
Watu wa ajabu sana!
 
Halafu Magufuli akimshinda Kenyata ndo aweze kukupata? Mara ya mwisho demu alinifanyia hivyo nilimpiga chini, mambo ya kuchonganisha Wanaume wawili eti mshindi akuchukuwe nilikataa, na mara nyingi unakuta demu mwenyewe anayechonganisha Wanaume wala siyo mzuri.
Sasa nawe umeandika nini hapa? Hoja hujaipitia vizuri?
 
Kama kawaida, hukuelewa nilichoandika. Badala yake unazunguka porini na maneno chungu nzima!.

Niliandika wapi kuwa Tanzania isiwe na mahusiano mazuri na nchi ziingine?
 
Kuna wengine wameweka utamaduni wa kupinga kila kitu. Tuwasifie Kenya na kuiga mazuri kwa faida ya nchi yetu. Yaani Kenya hawako kwenye list wakati wana vita na magaidi wa somalia. Sisi ni malumbano tu tuangalie kwa mapana tusipoteze muda kulumbana bila sababu. Hapa kuna mpaka usalama wa taifa 😂 eti na wenyewe wanajifanya wanajadili! Kwa manufaa ya nani taifa?. Usalama wa taifa unatakiwa kusaidia nchi ambayo inawezekana kabisa kuongia pabaya baada ya chaguzi na sio kushinda kwenye mitandao kuwinda Watanzania. Usalama mnajijua na watu wanawajua hapa
 
Back
Top Bottom