Uhuru Kenyatta afutilia Mbali wito wa Kustaafu Siasa baada ya Kutishwa na “Wasiojulikana”

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Rais Mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta, jumatatu hii ametupilia mbali ushauri na maoni ya Viongozi mbalimbali waliotaka astaafu Rasmi siasa za Kitaifa Nchini humo.

IMG_7294.jpeg

Picha: Rais Mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta

Akizungumza kwenye halfa moja ya Kitaifa ya Chama Cha Jubilee iliyofanyika jumatatu ya Mei 22, 2023, Kenyatta amesema alikuwa tayari kustaafu siasa za Nchi hiyo tangu akabidhi madaraka kwa Rais Ruto hadi pale ambapo watu wasiojulikana walipoanza kumtishia usalama wake.

Kenyatta amenukuliwa akisema “Nilikuwa tayari kuachana na siasa ili nifanye kazi zingine, lakini kuna baadhi wameamua maisha yao ni kutosha na kuamrisha wengine. Leo nataka niwaambie kuwa hauwezi kufanya mambo hayo kwa Uhuru Kenyatta. Watafute mtu mwingine”

Mbali na hapo, Kenyatta amenukuliwa pia akisema hakujipa madaraka mwenyewe kwenye Chama chake, bali aliaminiwa na watu wengine. Amewataka wanachama wa Chama hicho kutambua kuwa yeye bado ni kiongozi wao hadi itakavyo amriwa vingine na wakitana kuheshimiwa basi wawe tayari kuheshimu pia wengine.

Chama cha Jubilee kimewafuta uanachama baadhi ya wanasiasa na kuwataka wengine wajiuzuru kama wataona nafasi walizopo haziwatoshi ili kulinda chama hicho.
===

Former President Uhuru Kenyatta on Monday dismissed leaders who have been urging him to quit active politics.

Speaking on Monday during the Jubilee Party National Delegates Conference (NDC) at the Ngong Racecourse in Nairobi, Kenyatta said he was ready to retire from active politics after handing over to William Ruto in September until some unnamed people started intimidating him.

“I wanted to shelve politics and go deal with other things. But there are others who have decided that their work is to force and intimidate. Today, I want to tell you that, you can't do that to Uhuru Kenyatta. Let them look for someone else,” he told delegates.

The Jubilee boss told off leaders who have become disloyal to the party and who were eventually expelled during the NDC, saying he still remains the party leader.

“Jubilee is not Uhuru’s it has owners who gave me the leadership. They already have a successor but they told me to hold until they are ready for another leader. If you want to be respected, respect others,” Kenyatta said.

Some of the Jubilee national executive council members who faced the axe are Sabina Chege, Jimmy Angwenyi, Naomi Shaban, Nelson Nzuya, Joshua Kuttuny, Mutava Musymi and Kanini Kega.

“Kenya is a democracy. The decision by Jubilee Party members is still binding. And until you, the members decide otherwise, Jubilee Party leadership will remain. People who were given small positions by Jubilee Party can't dictate to us what to do. Their work was to champion Jubilee’s interests. They should resign and get us back the small positions we've given them. Our symbol is dove, and that means peace,” added the former president.

Citizen TV
 
Hana ushawishi, na hakua na ushawishi hata hapo awali ispokua mamlaka. Kosa kubwa la kisiasa alilofanya akiwa mamlakani ni kumuunga mkono Raila A.Odinga na kumsaliti W.S.Ruto naibu wake tena kwa fedheha, kebehii na vitisho vingi mno, lakini pia kuwasaliti watu wa kabila lake the likes of RigyG, Zimwi hili la usaliti litamtafuna na litamfedhehesha na kumtesa mno. Nadhani ana hasira sana na kwakweli anajipanga na huyo Raila kwamba nchi isiwe tulivu Rais alieko mamlakani asifanye chochote hadi 2027 wajaribu kumzuia kuongoza kwa muhula wa pili kupitia sanduku la kura kitu ambacho kwa maoni Yangu ni vigumu mno kwa hilo kutokea. Ni vizuri Uhuru kenyata akakubali kukaa pembeni kwa heshima, vinginevyo atafedheheka maisha yake yote ya Siasa.
 
Kumbe Ilikuwa lazima?? kuunga mkono rais aliyepo madarakani ndio democracy hiyo ya kenya ?
 
Hana ushawishi, na hakua na ushawishi hata hapo awali ispokua mamlaka. Kosa kubwa la kisiasa alilofanya akiwa mamlakani ni kumuunga mkono Raila A.Odinga na kumsaliti W.S.Ruto naibu wake tena kwa fedheha, kebehii na vitisho vingi mno, lakini pia kuwasaliti watu wa kabila lake the likes of RigyG, Zimwi hili la usaliti litamtafuna na litamfedhehesha na kumtesa mno. Nadhani ana hasira sana na kwakweli anajipanga na huyo Raila kwamba nchi isiwe tulivu Rais alieko mamlakani asifanye chochote hadi 2027 wajaribu kumzuia kuongoza kwa muhula wa pili kupitia sanduku la kura kitu ambacho kwa maoni Yangu ni vigumu mno kwa hilo kutokea. Ni vizuri Uhuru kenyata akakubali kukaa pembeni kwa heshima, vinginevyo atafedheheka maisha yake yote ya Siasa.
Kama unaishi Tanzania , jikite kwenye siasa za ndani na vitimbi vya wanasiasa wetu. Kenya is a different planet na huna ubavu wa kuwa mchambuzi wa siasa za kikanda. Yale yale ya simba na yanga.
 
Back
Top Bottom