Baada ya kifo cha Magufuli, Wapinzani walituaminisha chuki zitaisha kumbe bado?

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,391
9,665
Kuna msemo unaosema, asifuye mvua imemnyea.

Wakati wa Hayati Dkt. Magufuli, CHADEMA walikuwa na propaganda kali sana kwamba Magufuli ameshindwa kuleta umoja kwa taifa. Kwa vile Mara nyingi wanalalamika kwenye mitandao mambo yao yakaenda hadi nje ya nchi.

Kuna wengine hadi wakaomba uhamisho kwa mbwembwe kwamba ni wakimbizi wa kisiasa na sababu ni Hayati Magufuli.

Sasa Hayati Magufuli hayupo, Ila bado wanalazimisha chuki miongoni mwa Watanzania.

Mwenyekiti wa chama ana hubiri chuki za ukabila.

Wanachama wanahubiri chuki zaidi ya Diamond asipigiwe kura.

Hawa watu ni watu wa aina gani?

Ungekuwa wewe Ndio Rais wa nchi unawafanya nini Hawa? Unaweza ukawaalika ikulu kula nao mesa Moja na kugonga nao cheers?

Nahisi Dkt. Magufuli alikuwa sahihi kuwatuliza.
 
Kazi nyingine uwe unamwachia mkeo, vinginevyo tunashindwa kukuelewa.

1622466328056.png
 
Uoga wa nini...Diamond ni CCM.. CCM ni wengi kuliko Chadema na Inapendwa so wana CCM nao si wahamasishane Kumpigia kura Diamond na kwa kuwa CCM inapendwa sana basi hata Chadema wapige kampei bado haitafaa kitu. Kulalamikia hizi kampeni za Chadema ni kuonesha uoga wa CCM
 
Ukiwa Baba wa familia ukaona wanao hawapendani unawaita kuwasuruhisha, Sasa Baba alishindwa kaingia Mama kwa madaha kuwa hapendi kuona ugomvi kafungulia radio stations, magazeti na online tv's ambazo Baba aliona ndio zinawangombanisha wanae.

Ila sasa mbona Mama hatuoni akifanya kuimarisha umoja? sasa kama nae Mama kashindwa naona watoto wameona kama mbwai na iwe mbwai mbaya zaidi wanajua kabisa kuna watoto wenzao ni vipenzi wa mzazi.
 
Kudai katiba na tume huru ni kuchochea chuki?

Huwezi kunilazimisha kumpigia kura diamond kama naona mziki wake sio mzuri kushinda wa Burna Boy.
kura ni siri ya mtu kinachokufanya uje uharishe hapa jukwaani ni kitu gani tumieni hata akili ndogo tu ya kuvukia barabara
 
Nimecheka kweli yani eti hasira zao zimeamia kwa Diamond,Ajabu ktk 90% ya wasanii walokua wanapiga kampeni Basi wamemchagua diamond kufuta hasira zao na jinsi walivyo mandezi wakiongozwa na viongozi wao Bila aibu eti wanampigia kura msanii ambaye si mtanzania eti kuwakomesha.

Hapo ndo napata tabu Hawa watu wakichukua nchi visasi na umwagaji damu ndo vitataradadiii
 
Back
Top Bottom