Maramla
JF-Expert Member
- Jan 8, 2014
- 581
- 642
Moja ya karata mbovu kuwahi kuchangishwa katika Siasa za Upinzani Nchini Tanzania ni kitendo cha Baadhi ya Vyama hivyo kusherehekea na kukebehi Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dr. John Pombe Magufuli.
Mbaya zaidi walianza kumfanyia husda Marehemu bila kujiridhisha nguvu ya upendo wa Watanzania wa daraja la chini kabisa katika maeneo mbalimbali ya Nchini.
Wakaanza kubeba chuki zao za kisiasa na kizifanya ndizo za Watanzania, bahati mbaya Umma umewaumbua.
Kupitia maoni mbalimbali yaliyorushwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari katika nyakati tofautitofauti yalionyesha namna Wananchi walivyoguswa na Msiba mzito wa Kitaifa na kuonesha masikitiko yao juu ya kuondokewa na kipenzi Chao.
Lakini wakati wa kuupeleka mwili Uwanja wa Taifa kwa ajili ya Ibada ya Kuaga, umati mkubwa wa watu ulioangusha vilio huku wakimwaga maua na kutandika nguo bararani, ilionyesha mapenzi yasiyo na shaka kwa Kiongozi wao.
Baadhi ya Wanasiasa wanaobeba sura ya Upinzani Nchini walionyesha namna walivyopungukiwa na maarifa ya kusoma nyakati na wakalibeba jambo hili kwa chuki zao, husda wao na uzandiki wao binafsi jambo liliwajengea hasara ya kupoteza heshima waliyoijenga kwa miaka mingi.
1. ZITTO KABWE.
Huyu analazimisha kuonyesha watu kuwa yeye ni Mpinzani haswa, ila ameshushu heshima yake kwa kuonyesha furaha hadharani, kwakuwa huyu ni Muislamu ngoja nimkumbushe..
"Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa), ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema
“Msiwatukane maiti. Kwani wameshayaendea yale waliyoyatanguliza.”.
Ameipokea Imaam Ahmad, al-Bukhaariy na an-Nasaa´iy.
Leo Zitto amekiruka na kukikwaa kiunzi cha Imani ni aibu.
2.TUNDU LISSU
Huyu ndio kajiondoa kabisa kwenye mioyo ya Watanzania.. Hata huruma alizowahi kuzipata hatokuja kuzisogelea tena, huyu amegeuza Msiba huu wa Watanzania kuwa karata ya kujiona kuwa ni Mtakatifu na mwenye haki.
Anashinda kukebehi, kuisema na kusherehekea Msiba huu.
Hili kwake ni anguko litakalomuadhibu katika Maisha yake yote ya Siasa.
Huyu ndiye Mpinzani namba moja ambaye thamani yake imeshuka na kupoteza mapenzi ya watu kutokana na husda wake kwa Marehemu, kwa kifupi ni mropokaji wa maandishi na mdomo.
Amekuwa akikebehi na kusherehekea Kifo hiki, lakini ni kwa vile aliokuwa akiwatetea kwenye wizi wa rasilimali zetu nao wanashangilia kwa kuamini kikwazo kimeondoka, (anajidanganya).
UPINZANI WA NCHI YETU SIO MBADALA WA MAISHA YATU KWAKUWA HAUTUONYESHI NJIA ZA UTU.