Mhabarishaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2010
- 1,006
- 598
Wewe Lokissa, ni mbumbumbu wa maandiko, na wala humjui Yesu! Unajua miujiza aliyoifanya Eliya wakati alipokuwa anapambana na Wafalme? Hujui! Ngoja nikupe darasa! Soma katika Biblia, miujiza ya Eliya, alipokuwa akipambana na Mfalme Ahabu (1WAFALME 17:1; YAKOBO 5:17-18), na pia alipokuwa anapambana na Mfalme Ahazia (2WAFALME 1:1-18).
Unasema eti Kakobe aheshimu mamlaka "halali"! Mamlaka "halali", inayopingana na Mungu? Unajua kwamba, Yesu huyo, (unayefikiri unamjua) alimwita Mfalme Herode, "MBWEHA"? Hujui! Soma LUKA 13: 31-32, utaona! Unajua kwamba Meshaki, Shadraka na Abednego; walipingana na mamlaka ya Mfalme Nebukadreza, unayoiita wewe "halali"? Walipotupwa kwenye moto, unajua kwamba, "mtu wa nne", alikuja kuwatetea? Huyo, hakuwa "mwana wa miungu", bali Mwana wa Mungu, Yesu Kristo (DANIELI 3:1-30). Ilikuwaje basi Yesu, kuwatetea watu ambao "hawakuheshimu mamlaka halali", kama unavyodai? Kwenye maandiko, wewe bado ni chekechea! Kaa chini, ujifunze! Hujui neno lolote bado! (1WAKORINTHO 8:2).
Eti Kakobe asubiri kuaibika! Lini tena? Pole, bado unasubiri wa kuaibika, hadi sasa? Baada ya MIAKA MIWILI, wa kuaibika, amekwisha kuaibika tayari! Ni yupi? NI SERIKALI! Serikali iliyotumia bunduki, kung'oa mabango, kwa mbwembwe nyingi, ili kupitisha HARAKA, umeme wa 132 KV kwa ubabe, imeshindwa kuupitisha hadi leo, MIAKA MIWILI SASA! Hata kama leo Serikali ingefanikiwa kuupitisha umeme huo, IT IS TOO LATE! Bado tutawauliza, kwa nini imechukua MIAKA MIWILI? Kushindana na Mungu, na Watumishi wake, HAKULIPI! Serikali ijifunze kumuheshimu Mungu, na kuwaheshimu Watumishi wa Mungu!
Big Up gumegume, kwa kumkomesha Lokissa, na blabla zake za "kuheshimu mamlaka halali". Mamlaka "halali", inayoiba kura, ili kuendelea kuwepo madarakani? Serikali ya namna hii, ina uhalali upi? Shame upon you, MAGAMBA!