Baada ya DSTV kujichanganya kwa bei kubwa ya World Cup, AzamTv ni nafasi yenu hii kututangazia World Cup bei chee

Gharama za kuonyesha world cup ni kiasi gani mpaka ufikie conclusion hiyo?
Nimeona bid ya qatar kuonyesha kombe la dunia ilikuwa
QAT (2022)US$220 billion

Sasa kwa uelewa wangu kama hizi figure ni sahihi, itakuwa ni very very expensive kupata haki za matangazo, kuonyesha, na kadhalika. Sababu lazima Qatar watataka returns on investment.
 
TBC wanawezaje kuonyesha world cup?
Unafahamu hakuna TV company hata moja yenye thamani hiyo hapa Africa?
 
Ni basi tuu umasikini unatusumbua, hapo ni sawa na mechi moja unalipia Tsh 875.

Sasa tuje kwenye vibanda umiza tutalipia buku kila mechi au tutanunua vinywaji vya zaidi ya buku kwa kila mechi?

Si watetei DSTV ila najaribu kuwaza kwa uhalisia wa bei iliyopo.
 
Kwa Africa nadhani dstv ni giant kwenye urushaji wa mipira live, pia ana wateja wengi ambao wanafikia milion 22 africa nzima, huku South Africa pekee ikiwa na wateja milioni 9.
Dstv ana cost advantage kubwa kutokana na pool ya wateja, hivyo maumivu ya kulipia haki yanapungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…