VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Nianze kwa kupongeza ujenzi wa nidhamu,umakini na heshima katika utumishi wa umma kwa njia ya utumbuaji majipu. Anayekwenda mrama,anatumbuliwa. Safi sana!
DED wa Mkinga kule Tanga ametumbuliwa kwa kutishia kwa bastola. Ametumbuliwa kwakuwa amekwenda kinyume na wajibu wake. Ametumbuliwa kwakuwa amevuka mipaka ya kazi yake na hata kumponza. Amekwenda na maji!
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ndugu Salum Ally Hapi naye ameenda mrama. Amemuagiza Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni lililo chini ya Mhe. Yose Mlyambina kusikiliza upya shauri lililokwishaamriwa.
Kwa mujibu wa nyaraka niliyoiona (barua ya tarehe 12/10/2016),Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza kesi ya
Bwana Venance isikilizwe upya kwakuwa tu bwana Venance hakuridhika. Akijua taratibu za kisheria,kwakuwa naye ni Mwanasheria,DC Hapi anajua kuwa hana mamlaka ya kuamuru hivyo.
DC Hapi anajua kuwa asiyeridhika na uamuzi wa Baraza anapaswa kukata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha Ardhi. Anajua kuwa yeye kama DC si mamlaka kimahakama. Anajua kuwa amri yake kwa Mlyambina ni batili. DC Hapi amekwenda kombo,atumbuliwe!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam