Baada ya DED Mkumbo wa Mkinga, afuate DC Hapi wa Kinondoni!

Baada ya DED Mkumbo wa Mkinga, afuate DC Hapi wa Kinondoni!

Nianze kwa kupongeza ujenzi wa nidhamu,umakini na heshima katika utumishi wa umma kwa njia ya utumbuaji majipu. Anayekwenda mrama,anatumbuliwa. Safi sana!

DED wa Mkinga kule Tanga ametumbuliwa kwa kutishia kwa bastola. Ametumbuliwa kwakuwa amekwenda kinyume na wajibu wake. Ametumbuliwa kwakuwa amevuka mipaka ya kazi yake na hata kumponza. Amekwenda na maji!

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ndugu Salum Ally Hapi naye ameenda mrama. Amemuagiza Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni lililo chini ya Mhe. Yose Mlyambina kusikiliza upya shauri lililokwishaamriwa.

Kwa mujibu wa nyaraka niliyoiona (barua ya tarehe 12/10/2016),Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza kesi ya
Bwana Venance isikilizwe upya kwakuwa tu bwana Venance hakuridhika. Akijua taratibu za kisheria,kwakuwa naye ni Mwanasheria,DC Hapi anajua kuwa hana mamlaka ya kuamuru hivyo.

DC Hapi anajua kuwa asiyeridhika na uamuzi wa Baraza anapaswa kukata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha Ardhi. Anajua kuwa yeye kama DC si mamlaka kimahakama. Anajua kuwa amri yake kwa Mlyambina ni batili. DC Hapi amekwenda kombo,atumbuliwe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Nina imani Rais wetu ataisoma hii na itafanyiwa kazi soon huyu ni Rais wa vitendo kama ni kweli wamekiuka maadili ya kazi kuwajibika kunamuhusu
 
Gambo apimwe akili yawezekana ana matatizo makubwa sana ila hajijui..kwa Hapi sheria ifate mkondo wake kama kaingilia kazi ya mahakama ilihali anajua ni kosa..
 
Niongeze kwamba RC Arusha Ndg. Gambo anafanya mchezo wa siasa unaokwamisha utekelezaji wa juhudi na dhamira ya Rais kimaendeleo, anapaswa kutumbuliwa.
 
..wengi wa hawa ma DC na ma RC ni makada wa ccm wanaofanya kazi kwa itikadi....na hili limefanywa makusudi strategically ili kudhoofisha maeneo yanayoongozwa na wapinzani...kwa kweli lazima wapinzani maeneo haya wapambane kweli na watawala...maana wanataka mwisho wa siku pasiwe na maendeleo maeneo haya ili wananchi wawachukie wapinzani...hili tayari linatokea arusha alipo huyo dogo mwingine gambo...kazi yao ni kuvuruga upinzani...
 
Labda akeshe kupata jeshi la malaika kutoka mbinguni lakini ndani ya CCM wasafi ni kama kuchagua maharage kwenye makande.
kWA HIYO KWA AKILI ZAKO ULIZOBAKISHIWA NA AIKAEL wewe unaona WASAFI wapo CHADEMA??????jiangalie wewe kwanza usafi wako ndipo utakapogundua wasafi wapo wapi
 
Ha haaaa kwani nani hajui kuwa maDC wa Magufuli na hata ma RC wanaishi kwa dili kama hizi za kulazimisha dhuluma ili wapate rupia. Mimi nasema Magufuli hakukesha kama anavyotuaminisha kuwapata hawa watu kwani wengi wao ni wasanii na wala rushwa kuliko wale waliotangulia. Wana kiu ya ajabu ya mali.
teh! teh!
 
Wote wanaotumbuliwa wanatumbuliwa kwa haki. Huyo Hapi hawezi kutumbuliwa kwa majungu ya PM
Kumbe unajua majungu hayana nafasi eeh! Sasa mbona wewe huachi? Maana wewe ni fundi wa kuyapika na kupakua!
 
Huwezi mtu una miaka 35 unaenda kuongoza watu wazima na changamoto za madiwani huzijui alafu unapewa cheo kikubwa hivyo
 
..wengi wa hawa ma DC na ma RC ni makada wa ccm wanaofanya kazi kwa itikadi....na hili limefanywa makusudi strategically ili kudhoofisha maeneo yanayoongozwa na wapinzani...kwa kweli lazima wapinzani maeneo haya wapambane kweli na watawala...maana wanataka mwisho wa siku pasiwe na maendeleo maeneo haya ili wananchi wawachukie wapinzani...hili tayari linatokea arusha alipo huyo dogo mwingine gambo...kazi yao ni kuvuruga upinzani...
unaweza kukuta aliyekwenda kulalamika kwa DC ni mwana ccm,kwa hiyo ukada ukatumika kumpa upendeleo dhidi ya aliyeshinda kortini
 
Yale yaliyotokea Arusha kati yao wa wili mmoja wapo angekuwa mtu mzima lazima busara ingetumika lakini wote kila mtu anataka sifa.
 
Back
Top Bottom