Azzan Zungu anamwaga darasa Bungeni

Azzan Zungu anamwaga darasa Bungeni

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,506
Reaction score
123,802
Mwenyekiti wa kikao cha bunge kinachoendelea saa hii, Azzan Zungu, (nna-declare interest) ni mbunge wa jimbo langu la Ilala.

Hivi sasa anamwaga darsa kwa kila anaechukuwa shillingi ya waziri, nimeona mpaka sasa wabunge wa upinzani kama watatu wa upinzani kila wanapochukuwa shillingi na kuing'ang'ania yeye anatoa darsa la maana na wanamuelewa na darsa linawaingia mpaka wanarudisha shillingi wenyewe bila makeke, na hili nimelishuhudia toka jana si leo pekee.

Huyu ndiye alifaa kuwa Speaker wa bunge, anakubalika kote kote.

Ahsante Zungu, unaionesha Tanzania kwanini Wilaya ya Ilala ndiyo wilaya tajiri Tanzania na haina shamba wala madini. Vichwa.

We are proud of you. Ukigombea tena Ubunge tunakupa bila kupingwa. Kudos.

Mussa Azzan Zungu
 
Huwa nakumbali sana anapokuwa hapo kwenye kiti , anajuwa mtizamo wa kila mchangiaji nia yake na madhumuni tija na manufaa ya hoja zao ,kwa mtu binafsi au kwa umma.
 
Ahsante Zungu, unaionesha Tanzania kwanini Wilaya ya Ilala ndiyo wilaya tajiri Tanzania na haina shamba wala madini. Vichwa.

We are proud of you. Ukigombea tena Ubunge tunakupa bila kupingwa. Kudos.
Je anatetea muundo wa serikali ngapi?
Je unajua kuwa Ilala ndio wilaya inyoongoza nchini kwa kuwa na idadi kubwa ya mafisadi?
Je unajua kuwa wilaya ya Ilala ndio makao makuu ya wauza unga?
Je unajua kuwa wilaya ya Ilala...kwa sasa ngoja niishie hapa.
 
Mwenyekiti wa kikao cha bunge kinachoendelea saa hii, Azzan Zungu, (nna-declare interest) ni mbunge wa jimbo langu la Ilala.

Hivi sasa anamwaga darsa kwa kila anaechukuwa shillingi ya waziri, nimeona mpaka sasa wabunge wa upinzani kama watatu wa upinzani kila wanapochukuwa shillingi na kuing'ang'ania yeye anatoa darsa la maana na wanamuelewa na darsa linawaingia mpaka wanarudisha shillingi wenyewe bila makeke, na hili nimelishuhudia toka jana si leo pekee.

Huyu ndiye alifaa kuwa Speaker wa bunge, anakubalika kote kote.

Ahsante Zungu, unaionesha Tanzania kwanini Wilaya ya Ilala ndiyo wilaya tajiri Tanzania na haina shamba wala madini. Vichwa.

We are proud of you. Ukigombea tena Ubunge tunakupa bila kupingwa. Kudos.

Kwa upande wa uwezo wa kuongoza bunge, hata mimi naunga mkono. Zungu yuko vizuri kuliko wale wapuuzi wengine.
Ila kwa hilo analofanya bungeni saa hizi, hapo kidogo kuna tatizo. Hiyo kimsingi siyo kazi yake. Ni kazi ya waziri mwenye dhamana yake. Yeye kwa pale alipo, kama mwongoza kikao hatakiwi kuingilia mjadala au kutoa maoni, anapaswa kusimamia kanuni na taratibu za bunge tu ili mjadala uende sawia.

Kwa upande mwingine kama mbunge, ni kazi yake kuihoji serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio yake kwa mwaka wa bajeti uliopita. Na siyo kazi yake kuitetea, au kuisaidia serikali kwa kuitolea ufafanuzi au Darsa kama mwenyewe unavyoita.

Summarily anachofanya, pamoja na kuwa kinawezakuwa kinasaidia , lakini siyo sawa kwani ni nje ya majukumu yake. Hivyo anaingilia majukumu ya serikali.
 
Ilala inaongoza hadi kwa ugonjwa wa KIPINDUPINDU, hakijawahi kuisha kule.
 
Tunahitaji BUNGE huru na lenye nguvu.Hakutakiwa kuitetea serikali bali kuiwajibisha serikali,hiyo ndiyo kazi yake kubwa.Kwa sasa inaonekana wazi kwa sasa Tanzania hatuhitaji Mawaziri Wabunge.
 
Teh haa haa jamaa yangu yule Mbunge wa Dole Mzee wa Kuwashwawashwa Mh. Sylvester Mabumba sijui yuko wapi.
 
Je anatetea muundo wa serikali ngapi?
Je unajua kuwa Ilala ndio wilaya inyoongoza nchini kwa kuwa na idadi kubwa ya mafisadi?
Je unajua kuwa wilaya ya Ilala ndio makao makuu ya wauza unga?
Je unajua kuwa wilaya ya Ilala...kwa sasa ngoja niishie hapa.

Kwa research yepi??????
 
Zungu jumbo lake ndilo linaongoza kwa uchafu name Barbara mbovu. Nenda pale round pale shule ya Uhuru karibu na akiba. Mtaa alipokuwa anakaa yeye aggrei ndio unaongoza kwa Maji machafu.
 
Kwa upande wa uwezo wa kuongoza bunge, hata mimi naunga mkono. Zungu yuko vizuri kuliko wale wapuuzi wengine.
Ila kwa hilo analofanya bungeni saa hizi, hapo kidogo kuna tatizo. Hiyo kimsingi siyo kazi yake. Ni kazi ya waziri mwenye dhamana yake. Yeye kwa pale alipo, kama mwongoza kikao hatakiwi kuingilia mjadala au kutoa maoni, anapaswa kusimamia kanuni na taratibu za bunge tu ili mjadala uende sawia.

Kwa upande mwingine kama mbunge, ni kazi yake kuihoji serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio yake kwa mwaka wa bajeti uliopita. Na siyo kazi yake kuitetea, au kuisaidia serikali kwa kuitolea ufafanuzi au Darsa kama mwenyewe unavyoita.

Summarily anachofanya, pamoja na kuwa kinawezakuwa kinasaidia , lakini siyo sawa kwani ni nje ya majukumu yake. Hivyo anaingilia majukumu ya serikali.

Ukimsikiliza vizuri anawasaidia hao wabunge ndiyo maana wanakubali kurudisha shillingi, kwani ukizuwia shillingi, hoja inafikia kupigiwa kura na upinzani hawana majority wanashindwa kwenye kura. Anachofanya yeye ni kuiwacha wazi hiyo hoja ili ipate kuzungumzwa kwenye kamati maalum za bunge, anaipa hoja uhai. Unless niwe sijamuelewa darsa lake na wale wabunge wa upinzani wanaokubali kuvuta shillingi hawajamuelewa.

Kumbuka, hapo kwa sasa hivi yeye ni mwenyelkiti wa kamati ya bunge kwa hilo, kama mwenyekiti anaweza kuongelea mada hiyo. Bunge likikaa kama na yeye akikaa kama speaker ndio hawezi kuchangia zaidi ya kulitolea muongozo na kusimamia kanuni za kuendesha bunge, lakini si hapa lilipo sasa hivi kama kamati. Kumbuka hilo.
 
Zungu jumbo lake ndilo linaongoza kwa uchafu name Barbara mbovu. Nenda pale round pale shule ya Uhuru karibu na akiba. Mtaa alipokuwa anakaa yeye aggrei ndio unaongoza kwa Maji machafu.

Kwi kwi kwi teh teh teh, umeenda lini mara ya mwisho?
 
Je anatetea muundo wa serikali ngapi?
Je unajua kuwa Ilala ndio wilaya inyoongoza nchini kwa kuwa na idadi kubwa ya mafisadi?
Je unajua kuwa wilaya ya Ilala ndio makao makuu ya wauza unga?
Je unajua kuwa wilaya ya Ilala...kwa sasa ngoja niishie hapa.

Umekosa hoja unaanza kuhororoja.
 
Tunahitaji BUNGE huru na lenye nguvu.Hakutakiwa kuitetea serikali bali kuiwajibisha serikali,hiyo ndiyo kazi yake kubwa.Kwa sasa inaonekana wazi kwa sasa Tanzania hatuhitaji Mawaziri Wabunge.

Peleka mawazo yako kwa mbunge wako wa BMK.
 
Ahsante Zungu, unaionesha Tanzania kwanini Wilaya ya Ilala ndiyo wilaya tajiri Tanzania na haina shamba wala madini. Vichwa.

We are proud of you. Ukigombea tena Ubunge tunakupa bila kupingwa. Kudos.[/QUOTE]

Umeona barabara ya uhuru kuelekea kariakoo ilivyombovu...sasa
 
Back
Top Bottom