Nzi,
Watanzania ni wavivu wa kujisomea na kujiendeleza. Mambo mazuri ya Azimio la Arusha yanapatikana katika documents nyingi duniani. Kwanini tusifunue upeo na kuangalia mambo mengine.
Zakumi. Naomba nikuulize, tatizo lako ni nini katika suala la Azimio la Arusha?! Maana naanza kuamini kana kwamba wewe hiyo document, bila kujali yaliyomo humo ndani hutaki kuisikia. Sasa kama unasema mambo mazuri ya azimio yanapatikana katika documents mbalimbali duniani, tatizo ni nini? Hayo mambo mazuri kuwemo katika azimio au azimio kuchukua mambo mazuri kutoka kwenye documents mbalimbali duniani?Nzi,
Kuhusiana na masuala ya kujitegemea na maendeleo ya walio wengi Azimio isn't a sound guidance. Kumwambia masikini maneno matamu haina kuwa unamsaidia.
Mkuu Willie,
Kwa yale niliyonayo Azimio la Arusha lilikuja kwa sababu za kisiasa. Lakini kwa mtanzania yoyote mwenye upeo mzuri na akili timamu hawezi kukaa na kulitetea Azimio hilo.
Tanganyika ilipokuwa inapigania uhuru, kulikuwa na mambo mengi ambayo TANU ilitoa ahadi kuyafanya mara baada ya kupata uhuru. Lakini mambo hayo yaliitaji pesa na viongozi wa TANU walikuwa hawajui kuendesha nchi wala bajeti.
Uhuru ulipopatikana, wananchi wakaanza kusubiri kutimiziwa ahadi zao. Lakini kutokana na uhaba wa pesa, TANU ilikuwa nyuma kutekeleza ahadi hizo. Lakini wakati huo huo TANU inashindwa kutimiza ahadi zake, viongozi wa juu walikuwa wanaishi maisha ya kifahari kama wakoloni.
Hivyo TANU kurudisha umaarufu wake kama ule uliopata wakati wa uhuru ilihamua kutangaza Azimio hili. Na vilevile hili serikali ya TANU ipate pesa ya kutimiza ahadi zake, ulihamua kutaifisha mali za wawekezaji. Mfano huu uliigwa kutoka nchi kama Misri iliyoweza kutaifisha Suez Canal hili kujiongezea mapato yake. Hivyo hakuna jipya ambalo Azimio la Arusha lilileta.
Kwenye vipengere vya haki za binadamu, hizo ni haki zilizopo kwenye Tangazo la umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu. Viongozi wa TANU hawakutoa chochote kipya zaidi ya ku-copy and paste.
Na wameshindwa vibaya kwenye haki hizo. Azimio linatoa haki ya kutoa mawazo. Haki za kumiliki mali. Haki ya kushiriki kwenye shughuli za kisiasa. Wakati huo huo viongozi waliotunga Azimio hilo walilazimisha watu kuhamia kwenye vijiji vya Ujamaa bila mapenzi yao na kupoteza mali zao.
Tukurudi kwenye mafanikio ya Azimio la Arusha. Ukweli data zote zinaonyesha kuwa halikuwa na mafanikio yoyote yale. Rasimali zilizotaifishwa kama vile mashamba ya mkonge yalishindwa kuendelea.
Mfanikio ya elimu, afya, na maji hayakuletwa na Azimio la Arusha. Ni mipango ya World Bank, IMF, and donor countries. Hata nchi ambazo hazikuwa na Azimio la Arusha zilipata misaada hiyo. Mojawapo Zambia.
Kuhusiana na viwanda vilivyomilikiwa na serikali, vilevile ni mipangoa ya World Bank, IMF, and donor countries. Zaire, Zambia, Kenya n.k zilikuwa na viwanda vinavyomilikiwa na serikali.
Azimio la Arusha ni beneficiary tu wa siasa za kidunia zilizokuwepo miaka ya 60, 70, mwanzoni mwa 80. Na bila kuwepo siasa hizi za kiduani, Azimio la Arusha lisingeweza kuendesha hata kiwanda cha miswaki ya vijiti. Na nashangaa msomi kama Shivji anatoa mfano wa kiwanda cha Urafiki kuonyesha mafanikio ya Azimio la Arusha. Wachina walijenga kiwanda hicho kueneza siasa zao za mambo ya nje. Na matokeo yake wamepata kiti katika baraza la umoja wa mataifa na kura ya veto.
Upo sahihi kabisa lakini kwa bahati mbaya sana, nchi yetu ilikuwa inaongozwa na katiba ya CCM kama ndio katiba ya nchi kwa miaka mingi sana mpaka umma/upinzani ulipoanza kuamka. Katiba ya nchi ilikuwa inapuuzwa. isitoshe, Tanzania ilikuwa haina katiba kwa kipindi cha miaka 12 i.e 1964 - 1977, katika kipindi hiki, tulikuwa na katiba ya mpito. Na hata hiyo katiba ya 1977 mara nyingi sana ilikuwa haifuatwi na kuheshimiwa kama katiba katiba ya CCM.
Ndahani,
You quote my post, but you don't take time to read it. If you had read it, you would have found that I didn't mention Nyerere or his descendants or disciples.
Brain is a terrible thing to waste. Miaka ya utekelezaji ya hizo siasa za Azimio la Arusha, watanzania mmepoteza muda mwingi kujifunza vitu vya kishambashamba na kushindwa kujenga capabilities za kuendesha nchi. Na haichangazi kwa viongozi wa sasa kushindwa kuendesha nchi. Kwani wakati nchi zingine zinafanya juhudi za kujenga capabilities zao, kazi zenu zilikuwa kuandamana na kukimbiza mwenge.
Mutuz,- Living document ni ile Constitution ya USA tu, maana siku zote ina majibu ya maswali magumu ya taifa kila yanapozuka, wanaikimbilia inawapa majibu unajua Why ni kwa sababu ilijikita kwenye Sheria zaidi, kuliko miiiko ya uongozi. A living document inatakwia itoe mwanga panapokuwa giza sio kutoa impossible theories kama za Aazimio la arusha, kwanza haikuweza kufanaya anything muanzilishi wake akiwa hai, sasa hivi kweli kuna aliyetegeema itatusaidia akiwa hayupo?
- I have a lot of respect na Mwalimu, as individual na siku zote ninatenganisha Azimio na yeye kama kiongozi, kwenye maneno ya Azimio la Arusha, hakututendea haki taifa hili na ninasikitika sana kwamba wasomi wanaotakiwa kutusiadia na wao hawana majawabu ya matatizo tuliyonayo sasa wamejikita kujificha kwenye maneno ya Azimio la arusha!
William.
Asante mkuu kwa kuweka sawa hii hoja. Hatuna uhalali wa kulilaani Azimio la Arusha kama leo tunalifuja taifa. Why do we think we are better?I think tatizo halikua Azimio la arusha, tatizo kama kawaida ilikua ni ile process management
Mimi mara nyingi huwa najiangalia kama mtanzania na tabia yetu ya "easy way out" or "easy does it"
Ukichunguza hata ubepari ulipokuja, asilimia kubwa yetu ilikomalia yaliyo rahisi, this could a mindset, vizazi vilivyotangulia au hata genetic... haiwezekani wachagga wajue pesa halafu directly tuwaone wana tamaa na mmakua awe bize kwenye ngoma, ngono na majungu, then tusingizie ujamaa... KAMWE
As always, we tend to put blames on someoen else, and in many cases anakua either mtoto mdogo, marehemu au siyekuwepo
HII MADA NI NZURI, ILA IMEANZA NA BLAME GAME, DEAD END ETC!!! WE COULD USE IT POSITIVELY KAMA MCHAMBUZI NA WENGINE WANAVYOJARIBU KUTUSAIDIA
HATA UNGEKUA UBEPARI NDIYO SERA YA 1967, BADO WATANZANIA TUNGEISHIA KUULAANI, KUUTUKANA NA KUUKASHIFU, WE HAVE THAT CURSE SOMEHOW
Ndahani. Mkuu hapo ndipo umegonga penyewe. Sasa Zakumi na W. J. Malecela waje wajibu hoja.Zakumi,
Naona wewe ndio hujanielewa. Mimi nakubaliana kabisa na wewe kwamba zama zetu hatupo na Tanu wala ASP. Na kama tuna nia ya kusonga mbele basi tuyakabili matatizo yetu ya sasa. Kinachosumbua akili zangu ni mada yenyewe. Azimio la Arusha inawezekana lilikuwa na makosa. Lakini tumefanya jema gani ambalo leo linaweza kutumika kulihukumu Azimio la Arusha? Tunayofanya yanaonyesha wazi lile azimio lilikuwa la maana sana maana imagine wizi huu na matumizi mabaya ya madaraka na mali ya umma yangeanza enzi hizo, leo hili Taifa lingekuwa wapi?
Zakumi. Naomba nikuulize, tatizo lako ni nini katika suala la Azimio la Arusha?! Maana naanza kuamini kana kwamba wewe hiyo document, bila kujali yaliyomo humo ndani hutaki kuisikia. Sasa kama unasema mambo mazuri ya azimio yanapatikana katika documents mbalimbali duniani, tatizo ni nini? Hayo mambo mazuri kuwemo katika azimio au azimio kuchukua mambo mazuri kutoka kwenye documents mbalimbali duniani?
Kama msingi wa shida yako upo katika sentensi yangu ya mwisho hapo juu, mimi sioni tatizo lolote kama azimio lilikopi au kuchukua mambo mazuri kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Katika dunia hii ambayo vitu vingi vimeshagundulika na kuandikwa sana, hakuna ubaya wa ku-transfer hiyo knowledge na kui-mould katika mazingira ya nchi husika.
Suala la pili kwenye bluu hapo juu: kama azimio sio sound guidance katika masuala hayo, basi tujadili namna gani ya kuboresha kwa sababu angalau azimio lili-dare kuzungumzia hayo masuala. Ebu, niambie ni mpango au mkakati gani wa serikali ya sasa unaotilia mkazo hayo masuala seriously? Ni mafanikio yake yakoje?!
Kama suala ni utekeleza mbaya wa hayo yaliyo katika azimio, mkuu hiyo inakuwa ni fundisho, sasa tuangalie namna gani ya kutekeleza kwa uhakika na umakini zaidi hayo masuala.
Lakini tukiwa tunakandia azimio bila kuwianisha na "maazimio" yanayotumiwa sasa na taifa, pamoja na mafanikio yake, tutakuwa tunapiga kelele. Kandia huku ukionyesha azimio mbadala limefanikiwa vipi!!
Zakumi,
Naona wewe ndio hujanielewa. Mimi nakubaliana kabisa na wewe kwamba zama zetu hatupo na Tanu wala ASP. Na kama tuna nia ya kusonga mbele basi tuyakabili matatizo yetu ya sasa. Kinachosumbua akili zangu ni mada yenyewe. Azimio la Arusha inawezekana lilikuwa na makosa. Lakini tumefanya jema gani ambalo leo linaweza kutumika kulihukumu Azimio la Arusha? Tunayofanya yanaonyesha wazi lile azimio lilikuwa la maana sana maana imagine wizi huu na matumizi mabaya ya madaraka na mali ya umma yangeanza enzi hizo, leo hili Taifa lingekuwa wapi?
Mkuu wangu Marekani ni Marekani wao walipitia historia ya mambo tofauti kabisa na sisi, kwanza walikuwa wazungu waingereza waliotawaliwa na Malkia na hawakupenda kuwa chini ya Malkia na utawala wake. Pengine naweza kusema kama leo sisi tukiazimia kuiangusha CCM na utawala wake tukaandika Azimio jipya dhidi ya CCM, ndivyo unaweza linganisha kwa uchache na Decralation of Independence. Again, kila nchi ina WATU na MAZINGIRA tofauti hivyo wanakabiriana na maswala tofauti na hata kuweka malengo tofauti.Kwanza ni lazima tuamini kuwa the best of the country is ahead of us. Siku zote kizazi kilichopo kinajaribu ku-shape maisha ya kizazi kinachokuja. Lakini siku zote kizazi kipya kinachagua maisha yake.
Chukua mfano wa Azimio la Uhuru wa Marekani na Katiba yao. Katika documents hizo mbili hakuna sehemu inayosema Marekani ni nchi ya wakulima. Na hakuna sehemu inayosema Marekani ifanye juhudi kuwa nchi ya viwanda au kusaidia wengi vijijini.
Azimio la Arusha is so specific kana kwamba Tanzania itakuwa nchi ya wakulima na wafanyakazi milele. Je mfuga nyuki au ng'ombe sio mtanzania. Je mvuvi, mfanyabiashara sio watanzania. Je watunzi wa vitabu, wasanii sio watanzania?
Watanzania wanahama vijijini na hatuwezi kuzuia mass migration. Azimio linafikiri kuwa uti wa mgongo ni kilimo, ukweli wa mambo sekta ya utalii na madini zinazidi sekta ya kilimo.
Kuhusu mbadala wa Azimio la Arusha, ukweli wa mambo Tanzania ni nchi ya vyamba vingi. Utawala wa kikatiba na kisheria ndio mwelekeo uliobaki.
----Ninaomba kusema tena na tena, we were Dead wrong na idea za Azimio La Arusha, infact ndilo limetufikisha hapa tulipo yaani tumekwama hili taifa, hatujui tunakokwenda wala tulikotoka. Halafu wanatokea wasomi wanaodai eti turudi kwenye Azimio, hilo Azimio limetushinda mwanzoni kwa nini kuna wanaoamini tutaliweza sasa?
.........Recently, nimeona wale wengi walioachwa kwenye uongozi wa juu yaani kwenye mlo, wakililia Azimio, halafu ninachukizwa sana ninapoona media inawapa free lunch hawa waliokosa mlo, sijawahi kuwasikia wakisema Azimio liliwahi kumfunga kiongozi gani wa juu mwizi, sijawasikia wakisema Azimio lilifanya nini cha maaana mpaka wanalilia!
Kwanza ni lazima tuamini kuwa the best of the country is ahead of us. Siku zote kizazi kilichopo kinajaribu ku-shape maisha ya kizazi kinachokuja. Lakini siku zote kizazi kipya kinachagua maisha yake.
Chukua mfano wa Azimio la Uhuru wa Marekani na Katiba yao. Katika documents hizo mbili hakuna sehemu inayosema Marekani ni nchi ya wakulima. Na hakuna sehemu inayosema Marekani ifanye juhudi kuwa nchi ya viwanda au kusaidia wengi vijijini.
Azimio la Arusha is so specific kana kwamba Tanzania itakuwa nchi ya wakulima na wafanyakazi milele. Je mfuga nyuki au ng'ombe sio mtanzania. Je mvuvi, mfanyabiashara sio watanzania. Je watunzi wa vitabu, wasanii sio watanzania?
Watanzania wanahama vijijini na hatuwezi kuzuia mass migration. Azimio linafikiri kuwa uti wa mgongo ni kilimo, ukweli wa mambo sekta ya utalii na madini zinazidi sekta ya kilimo.
Kuhusu mbadala wa Azimio la Arusha, ukweli wa mambo Tanzania ni nchi ya vyamba vingi. Utawala wa kikatiba na kisheria ndio mwelekeo uliobaki.
Mkuu wangu unaona sasa ulivyopotea. Hizo sekta za Utalii na Madini zinaajiri watu wangapi?..Hivi kweli Utaifa kwako unatokana na pato la nchi hata kama pato hilo ni dogo kiasi gani maadam ndilo linaongoza?... ama unatokana na ukweli kwamba hawa wazawa ni watu wa aina gani. Ikiwa asilimia 80 ya nguvu kazi yetu ni wakulima na wafanyakazi unafikiri wakiwezeshwa hawa watazidiwa na huo Utalii wa wanyama pori na madini ambayo mmeshawakabidhi wazungu hadi yaishe?..Watanzania wanahama vijijini na hatuwezi kuzuia mass migration. Azimio linafikiri kuwa uti wa mgongo ni kilimo, ukweli wa mambo sekta ya utalii na madini zinazidi sekta ya kilimo.
Duh! Mkuu Zakumi, naona wewe hutaki kuelewa au huelewi kweli. Mimi sijasema kama azimio halina mapungufu, linalo. Lakini vile vile lina mazuri pia ambayo yanatufaa, ni kiasi cha ku-mould hayo mazuri ili yaweze kuendana na hali ya sasa. Sasa ukiwa unang'ang'ania hoja yako kwa kutumia maneno kama hayo, nakushangaa. Hivi huwezi kuona zaidi ya ulivyoona katika hayo? Vile vile wakati linaandikwa, wafanyakazi na wakulima ndiyo walikuwa uti wa mgongo wa taifa. Wao ndiyo walikuwa walipa kodi na chanzo kikubwa cha mapato; hivyo lengo likawa katika kuhakikisha wanapewa kipaumbele ili waweze kusaidia katika gurudumu la maendeleo. Ila kama azimio lilikuwa so specific, kuna ubaya gani sasa, tukilirekebisha na kuzingatia makundi mbalimbali ya watanzania?
Kwenye suala la pili, mzee hata hilo nalo huelewi? Hivi asimilia kubwa ya watanzania wapo katika sekta gani? Jibu ni kilimo, hivyo azimio lilitilia mkazo katika sekta ambayo watanzania wengi wapo na wanaitegema kwa maisha yao na maendeleo ya taifa kiujumla. Ulitaka liseme madini ndio uti wa mgongo wakati watanzania wengi sio wachimba madini?!
Vile vile tukija katika hali ya sasa, ambapo misingi kama hiyo ya azimio imetupiliwa mbali, hizo sekta ulizozisema (utalii na madini) licha ya kuwa zinaongoza katika pato la taifa, sekta hizo hazijaweza kuleta tija ya moja kwa moja kwa watanzania walio wengi. Wawekezaji wa nje na "wenye mamlaka" ndiyo wananufaika. Si ajabu kuona takwimu zikisema uchumi wa nchi unakuwa, wakati mifuko ya watanzania wengi inazidi kutoboka.
Mkuu tutazunguka na kumaliza dunia yote, mwishowe tutarudi pale pale, kwamba taifa limepoteza dira na mwelekeo toka lilipoamua kulitupilia mbali Azimio la Arusha.
Upo sahihi kabisa lakini kwa bahati mbaya sana, nchi yetu ilikuwa inaongozwa na katiba ya CCM kama ndio katiba ya nchi kwa miaka mingi sana mpaka umma/upinzani ulipoanza kuamka. Katiba ya nchi ilikuwa inapuuzwa. isitoshe, Tanzania ilikuwa haina katiba kwa kipindi cha miaka 12 i.e 1964 - 1977, katika kipindi hiki, tulikuwa na katiba ya mpito. Na hata hiyo katiba ya 1977 mara nyingi sana ilikuwa haifuatwi na kuheshimiwa kama katiba katiba ya CCM.
Ni muhimu ukatenganisha NIA, MCHAKATO na MATOKEO when it comes to discussing success and failures za Azimio la Arusha. Katika hoja zako, aidha kwa makusudi au bahati mbaya, umejikita zaidi kwenye MATOKEO huku ukigusia gusia kidogo MCHAKATO. NIA ni suala ambalo haujaligusa kabisa, hivyo kukosesha uzito hoja zako kwanini azimio la arusha was a failure. Kaka yangu William Malecela pia ni victim wa mapungufu haya. Inawezekana hoja zenu zingekubaliwa na wadau wengi humu lakini mnapoanguka ni pale mnapodharau "NIA".
Kiukweli sijui sana kuhusu Azimio la Arusha ila ninachojua ni kuwa kwa mujibu wa Mzee Nyerere halikuwa na mawaa kiasi hicho kama ambavyo Willy anataka tuamini. Ninapomsoma Willy napata picha kuwa kuna mambo kaambiwa (in a wrong way) na watu fulani kuwa Azimio lilikuwa si sawa. Ningemwelewa kama aheweka hoja za msingi kama ambavyo Mchambuzi ameainisha, tena kwa upeo sana ni jinsi gani ya kupangua dhana, hoja ama jambo fulani na ukaonekana wa maana kuliko kutumia jazba katika kupingana na jambo ambalo huna utafiti nalo wala data za kukusaidia kuwasilisha hoja yako.
Ni sawa na mshabiki kulalama kuwa mchezaji fulani kapewa 'red card'. Utakapomhoji ni kwa vipi asipewe utasikia akisema, ,ah! Refa kanunuliwa!' Hayo ndio mapungufu ya Willy. Ningependa ajibu na kuleta mada yake kwa namna ambayo Mchambuzi kaainisha, ndipo tuwe na ujasiri wa kuungana nae ama la
Mkuu wangu kuna mengi ambayo Thomas Jefferson mwandishi wa Declaration of Independence hakuweza kuyamaliza wala kuyafanya wakati akiwa madarakani au uhai wake, lakini mengi leo yamefikiwa. Slave trade iliekuwepo na weusi hawakuchukuliwa kama raia wa nchi ile lakini maudhui ya Azimio hili bila kupindishwa yamewaweka weusi kuwa katika kundi la Azimio hilo. Hili ni swla la kiimani zaidi na sio technical ila ni kama unavyoamini juu ya YESU ktk utawala wa mbinguni, hapa pia una uzima wako kama mwananchi mzawa kiutawala.- Interesting, unasema katiba ilikuwa inaapuuzwa, ok nani aliyekwua anaipuuuza wakati the author wa katiba na Azimio alikuwepo, tena kwenye power ni kwasababu hata yeye mwenyewe aliona ameunda something that is imaterial, I mean ni vyema kama na wewe unakubali kwamba katiba na Azimio vilikuwa vinapuuzwa hata the author alipokuwepo, sasa tutaliweza leo akiwa hayupo?
William.
Hakuna anaesema kwamba utawala wa Nyerere haukuwa na mapungufu, lakini sio sahihi kusema Azimio la Arusha halikuwa na mazuri. Hoja ya msingi hapa ya kuijadili ni je, Yepi yalikuwa ni mazuri na yepi yalikuwa na mapungufu when it comes to Azimio La Arusha? More importantly, tukijaribu kujadili separately kabla ya kuyajumuisha masuala matatu - NIA, MCHAKATO na MATOKEO YA SERA YA AZIMIO LA ARUSHA, ili kujenga msingi mzuri wa kutuongoza katika mjadala huu.- Interesting, unasema katiba ilikuwa inaapuuzwa, ok nani aliyekwua anaipuuuza wakati the author wa katiba na Azimio alikuwepo, tena kwenye power ni kwasababu hata yeye mwenyewe aliona ameunda something that is imaterial, I mean ni vyema kama na wewe unakubali kwamba katiba na Azimio vilikuwa vinapuuzwa hata the author alipokuwepo, sasa tutaliweza leo akiwa hayupo?
William.