Azimio la Arusha: Kwanini shule za Seminari hazikutaifishwa?

Moja ya Nguzo za Azimio la Arusha la mwaka 1967 ni kutaifisha vyanzo vyote vya Uchumi ikiwamo Mabenki, Mashirika ya Bima, Vyuo & Shule binafsi.

Swali ni kwamba kwanini Shule za Seminari hazikutaifishwa?
Kwani walifunga Madras.Tofauti ni KWAMBA seminari wanakufundisha kila kitu na mengi muhimu
 
Nadhani mleta Mada umeshapata baadhi ya majina ya shule zilizotaifishwa wakati wa azimio la Arusha shule Kama Nganza,Tosamaganga,pugu,Nsumba,Milambo na nyingine nyingi tu zilikuwa za kanisa katoriki.
Shule nyingi zilikuwako za kiislamu.
 
Uzuzu wangu upoje??Kwanza mie sio Mwislam, Cha pili nimesoma Franciscan Seminary Maua Moshi. Azimio la Arusha alikutaifisha ata Seminary Moja kwa dini na Madhebu yote ya Dini hapa Tanzania.Humu JF kuna Vichaa wengi mno ikiwemo na Wewe fanya mpango upelekwe Milembe au Lutindi kupatiwa matibabu
Asante kwa kufafanua. Wengi hawajitambui. Watu hudhani shule inayomilikiwa na taasisi ya kidini tu basi imeshakua seminari.
 
Kigonsera,tosamaganga,kilakala,kibasila,forodhani(st Joseph)sasa hivi imerudishwa tena kwa mmiliki wa awali.
 
Sidhani kama hoja ya msingi ilikuwa ni kutaifisha kutaifisha tu...lengo kuu lilikuwa kuhakikisha kuwa hakuna Shule, Taasisi, huduma .n.k inayotolewa kwa kubagua, iwe ni kwa dini, kabila, rangi n.k.

Mfano pale Arusha kuna shule inaitwa Meru Primary ipo mpaka leo, mpaka miaka ya 80's ile shule ilikuwa karibia nusu au zaidi ni Wanafunzi wa Kihindi, na ni kwamba Shule ile ilikuwa maalumu kwa ajili ya Wahindi tu...kadri muda ulivyoenda ndio waliendelea kupungua na kuwaacha waswahili.

Na hicho ndio Mwalimu alitaka kuona, asibaguliwe Mtu kwa hali yoyote na wala sio dini peke yake.

Hivyo kutaifisha haukuwa msingi mkuu kama Taasisi au huduma haifanyi ubaguzi, hata kama inamilikiwa na kundi fulani.
 
Kanisa lilikua na shule mbalimbali kuendana na mahitaji. Seminari nyingi zilikua na lengo la kulea miito. Hizo mara nyingi ni moja kwa kila jimbo. Wakati wa kutaifishwa serikali ilichukua shule za kanisa kama Ilboru, Karatu, Tosamanga na nyinginezo zilizokua hazilei miito. Pia baadhi ya seminari zimeanzishwa baada ya serikali kutaifisha shule ili kulea miito ya watu wake. Kwa sasa kanisa lina shule nyingi maana lina juhudi ya kujenga.
 
Yalikuwa maamuzi magumu yaliyogusa nafsi ya aliyeamua kwa ajiri ya kuwabeba wengine. kosa maamuzi hayo hali ingekuwa mbaya sana kwa wengine. kuhoji kwanini ni kupoteza muda na kujaribu kuwapandikizia hasira wengine.
 
Seminary ukisema ipo kama Madrasa unakosea tena sana! Madrasa wanafundisha Kiarabu na Kusoma juzuu tu(msahafu)-Seminary zinafundisha Elimu ya Secondary form 1 to form 6+ Bible knowledge .
Acha ubishi kuna tofauti ya seminary na shule za seminary zipo seminary zinamiliki shule kama shule ila msingi wa seminary ni kutoa elimu kwa ajili ya kutumikia dini.
 
Back
Top Bottom