Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Uchunguzi wangu umebaini kuwa asilimia kubwa sana ya wanafunzi waliosoma shule za Masista hawawapendi Watawa hao na wala hawapendi kurudi kusoma shule hizo.
Aidha, wengi wa wanafunzi hao wanawapenda sana Ma-father (Mapadre) kuliko Masista.
Utasikia baadhi ya wanafunzi hususan wa kike wakisema "sina hamu na mtu anayeitwa Sister na wala sitamani kumuona kwa macho yangu kama siyo kukutana naye kwenye maisha yangu mazima, hata kwenye Misa nikienda sitamani kuwaona"
Mwanafunzi mmoja alimwambia mzazi wake kuwa "mimi siendi tena F5 shule ya Masista, ukilipa ada huko basi kasome mwenyewe, siyo mimi"
Humu jamvini kuna wadau waliosoma seminari na seminari ndogo za Kikatoliki tunaomba kupata maarifa kwenu yatayojibu maswali haya:
1. Mnadhani tatizo ni nini?
2. Kipi kibadilike kwa Masista au hata kwenye mtaala wa kuwaandaa Masista?
3. Je, Masista ni walezi wazuri au wabomoaji wazuri?
4. Kwanini Masista kama watumishi wa Mungu waonekane hawafai?
5. Ma-father wana kipi ambacho Masista hawana?
6. Kama Kanisa ni moja, shule moja kwanini mifumo ya malezi iwe tofauti kati ya Ma-father na Masista?
Tujadili kwa nia ya kupata maarifa yenye ufumbuzi na faida kwetu na kizazi kijacho.